Afrika leo tunasimama na Mexico kombe la dunia

Afrika leo tunasimama na Mexico kombe la dunia

Ukiangalia kwa umakini, sheria, kanuni, na katiba ni makaratasi tu; hazina uzima ndani yake zenyewe. Kama kiongozi hana ile mindset (mtazamo wa ndani) wa kutumikia watu na kuwa na hofu ya kushindwa kuwajibika, atatafuta kila namna ya kupenya katikati ya hizo sheria au atazipuuza kabisa. Huwezi kuongoza kwa ufanisi kwa kutumia "fimbo ya sheria" pekee kama ndani ya moyo wa kiongozi hakuna uzalendo au utu.
Bahati mbaya sana, Tunaishi katika taifa ambalo lina viongozi wasio na accountability mindset.
 
South Africa wako sawa,kika mtu abaki kwao ajenge nchi yake,wakiruhusu kilq mtu aende kwenye nchi yao,kesho wenyeji watakuwa wageni kwenye nchi yao
kuwa kwao sawa au kutokuwa sawa haiwapi uhalali wa kufanya mauaji kwa wa-Africa wenzao, we could have murdered them as well when they came to us seeking to make freedom fighting camps, we didnt. Kama hawatutaki watuondoe kwa kufuata sheria na sio kwa mauaji.
 
Bahati mbaya sana, Tunaishi katika taifa ambalo lina viongozi wasio na accountability mindset.
Duh, mkuu, hapo umegusa kidonda ambacho kimekuwa kikitutesa kwa muda mrefu sana. Huo ndio uhalisia mchungu ambao unarudisha nyuma fikra za watu wengi wanaoamua kuacha kufuatilia mambo ya nchi na kuamua "kula maisha" ili kulinda afya zao za akili.

Inasikitisha sana unapoona nchi ina rasilimali kila mahali na watu wenye vipaji, lakini mfumo wa uongozi umekaa kwa namna ambayo mtu anashika dhamana kubwa ya umma lakini anajiona yeye ni "mungu mtu" badala ya kuwa mtumishi wa wananchi. Ile hofu ya "nikiboronga nitawajibishwa au nitaondolewa" haipo kabisa kwenye akili zao. Wanajua kabisa kuwa, iwe jua au mvua, nafasi zao ziko salama ilimradi wanajua jinsi ya kucheza na mfumo
 
kuwa kwao sawa au kutokuwa sawa haiwapi uhalali wa kufanya mauaji kwa wa-Africa wenzao, we could have murdered them as well when they came to us seeking to make freedom fighting camps, we didnt. Kama hawatutaki watuondoe kwa kufuata sheria na sio kwa mauaji.
Waliokuja kutafta msaada wa ukombozi ni viongozi wao,na hawakuja kuloea huku,walikuja na kurudi kwao,sasa kwann sisi tunakuwa vinga'nganizi kwenye nchi yao? Na hata hao waliokwenda huko,wengi ni wazamiaji hawakufuata sheria,leo hii unataka waafrika kusini wafuate sheria kwa kuwaondoa? Waondoke kama walivyokuja kwa kuzamia.
 
Haihalalishi wao kufanya mauaji.
 
Back
Top Bottom