Mkuu nakuunga mkono sana! Ingawa uwepo wa hii mahakama ya ICC itasaidia kuwazuia viongozi kutumia madaraka yao vibaya wawapo madarakani lakini tumeshuhudia mahakama hii ikiwashughulikia viongozi pekee wa nchi za Afrika! Mbona Bush hajashtakiwa? Blair na Sarkozy? Kwa vitendo vyao vya kuvamia Iraq kwa kisingizio cha matumizi ya kemikali lakin baadae wakamuua Sadam ikafahamika baaadae kuwa hapakuwepo na chemical weapons! Wameua raia wengi sana wasio na hatia! Kwanini hawa hawafikishwi kule ICC? Kwanini Kenyatta, Rutto, Albashir, Laurent Bagbo na yule wa Liberia?
Mimi siwatetei hao viongozi wasishitakiwe kwa makosa waliotenda but kwann Afrika tu? Mimi ningetegemea viongozi wa AU, wangeshinikiza usawa na haki itendeke kwa nchi zote vinginevyo ni sawa wakijitoa!
Ndiyo mkuu,Mnatumiwa na mabeberu kuja hapa JF,mnafurahia Viongozi wenu kudhalilishwa na mfumo wa kikoloni? Blair na Bush wali ua maelufu ya watu hawakwenda hata ICC! Marekani haija saini hata mkataba wa Rome! Enyi waafrika wajinga mna ona kama jambo la kawaida viongozi wenu kudhalilishwa??? Mmelogwa na nani enyi kizazi masikini wa fikra na kutambua utu na thamani yenu????
CC CHUAKACHARA
...
After the resolution made in the Ethiopian capital Addis Ababa, the AU wrote to the United Nations Security Council, notifying it of their decision and asking the body to grant the same by directing the ICC to adjourn all cases against African leaders until they complete serving their term in office.
...
Azimio la ajabu sana hili.
Yaani mtuhumiwa wa uhalifu aachwe hadi amalize muda wake wa utumishi kisa kwa kuwa ni rais. Na wengine ndio kabisa hawatakaa "wamalize" huo muda wao, kwanza wanaweza kufariki wakiwa madarakani; pili watang'ang'ania hizo nafasi ikibidi hata kubadili katiba zao.
Pia kuna hatari kubwa ninayoiona hapo kwenye underlined; mtuhumiwa (rais) atahakikisha MASHAHIDI WOTE WANATOWEKA "before completing his term". So, tutegemee "kupotea" kusiko kwa kawaida kwa baadhi ya wananchi endapo rais aliyepo madarakani ni mtuhumiwa wa ICC.
Sikubaliani na hili azimio.
Mkuu mimi sioni kama barua ambayo Viongozi wa Africa wanataka kuwasilishwa UN kama haitaishia kwenye trash can, Dunia nzima imekwisha shitukia mbinu za baadhi ya viongozi wa Kiafrica waharifu na wapenda madaraka kupindukia, hapa wengi wao wana gang up kwa kuwa wanajuwa nao wana madhambi yao, hivyo the Hague inaweza kuwa halali yao siku za usoni ni hilo tu, sio kwamba wanawaonea huruma/watetea wakina Rutto na Mwenzake - kinacho fanyika pale ni mchezo wa kuhigiza tu.Mambo mengine yanashangaza sana - kabla ya Rutto na Kenyatta kuingia madarakani walikuwa recorded kwenye kanda za sauti na Video wakisema wako tayari kwenda the Hague kujitetea, ikumbukwe walishtakiwa kama Rutto na Kenyatta na sio Rais na makamu/Waziri mkuu wake, si hilo tu hata Watu wenye hekima zao waliwaonya wapiga kura kutumia busara katika uchanguzi wao, wakichagua watu wanaotuhumiwa kwa makosa ya jinai basi wategemee kwamba muda wao mwingi utapotea katika kusikiliza kesi, na hakuna ambaye anaweza kutabiri hukumu itachukuwa mkondo gani, sina shaka raia wengi walizingatia ushauri huo - tatizo likawa si nani alipigaji kura bali ni nani alihesabu kura - wakaweka msemo wa dikteita wa Taifa la URUSI ya zamani kwenye MATENDO 4 a reason - sasa hivi wamebadirisha kauli wanasema huwezi kushtaki Rais aliye madarakani that means vurugu zote za matokeo ya kura shabaha yake ni kujenga mazingira ya kuwahokoa watuhumiwa kwa visingizio vya kitoto nayo ni: Wako madarakani hawawezi kushtakiwa!! Wanaogopa kitu gani? Kama hawana makosa kwa nini hawataki kwenda kujitete? Kama leo hii Dunia nzima inawatafuta magaidi walio husika na vifo vya watu 67 kwenye supermarket nchini Kenya, inakuwaje Kenya hiyo hiyo na baadhi ya Viongozi wa Africa wanataka kuwakingia kifua watuhimiwa walio husika na vifo vya Raia wa Kenya zaidi ya elfu moja na ushee na wengine zaidi ya 300K. wanaendelea kuishi kwenye makambi ya makeshift mpaka leo - Viongozi wa Africa wanataka kutueleza nini? Kwamba damu za Foreigners na a few Kenyans waliopoteza maisha yao hivi juzi juzi kwenye Supermarket damu yao is more precious kuliko damu ya Wakenya elfu moja na ushee waliokufa kwenye machafuko ya 2008/9! Kwa bahati mbaya baadhi ya Viongozi wetu wa Kiafrica save Botswana hilo hawalioni kabisa, as far as they are concern ma Rais na Viongozi wengine ni wa maana zaidi, raia wa nchi zao ni expendable.Azimio la ajabu sana hili.Yaani mtuhumiwa wa uhalifu aachwe hadi amalize muda wake wa utumishi kisa kwa kuwa ni rais. Na wengine ndio kabisa hawatakaa "wamalize" huo muda wao, kwanza wanaweza kufariki wakiwa madarakani; pili watang'ang'ania hizo nafasi ikibidi hata kubadili katiba zao.Pia kuna hatari kubwa ninayoiona hapo kwenye underlined; mtuhumiwa (rais) atahakikisha MASHAHIDI WOTE WANATOWEKA "before completing his term". So, tutegemee "kupotea" kusiko kwa kawaida kwa baadhi ya wananchi endapo rais aliyepo madarakani ni mtuhumiwa wa ICC.Sikubaliani na hili azimio.
Kukosa umakini wa ICC, kuonyesha upendeleo wa Wazi kwa viongozi wa mabara mengine waliofanya makosa kama waliyofanya viongozi wa kiafrika na mengine kama hayo ndiyo hasa yameifanya ICC ikose credibility miongoni mwa nchi za kiafrika.....
Pia kuna hatari kubwa ninayoiona hapo kwenye underlined; mtuhumiwa (rais) atahakikisha MASHAHIDI WOTE WANATOWEKA "before completing his term". So, tutegemee "kupotea" kusiko kwa kawaida kwa baadhi ya wananchi endapo rais aliyepo madarakani ni mtuhumiwa wa ICC.
Sikubaliani na hili azimio.