Africa itachukua miaka 500 kuwa kama America na Ulaya- Bill Gates

mkuu mi sishangai...
Ukiangalia hizo nchi nyingi(za ulaya na america) hazikuibuka tu kwa cku 1 kuwa matajiri
Ukiangalia hizo nchi zimeanza kusaka maendeleo tangu mwishoni mwa karne ya karne ya 15...kipindi hicho ndicho uingereza ina anza mapinduzi ya kilimo(agrarian revolution) na baadae baada ya uhuru wakawa tayari wamefanya mapinduzi ya viwanda(industrial revolution)
Hapo ni kwa bi mkubwa Elizabeth pale uingereza.
Ukiangalia kwa umakini utaona bwana mapesa(Bilgate) alichosema ni cha kweli kabisa mkuu kwamba baada ya miaka 500 ndo tunaweza kufika level walipo wao!
 
Tatizo wasomi wengi wa africa wametimkia ughaibuni hivyo bara kubakia na illiterate people wengi na wasomi wachache ambao wamekubali kukandamizwa na utawala dhalimu wa viongozi wa africa. Hamna ile morale ya kufanya kazi kujenga nchi.

Pia wataalam wengi Africa wameacha fani zao manake hazilipi na kuwa wanasiasa, kunamaendeleo kweli hapo?
Mkuu, kuna kamsemo kuwa " if Leonado can't go to the mountain, shall take the mountain to Leonado"...linapokuja suala la wasomi kutafuta fursa ughaibuni, ni jambo lisilokwepeka. wasomi wengi hawatambuliki na serikali zao na huonekana threat sometimes. ndo maana badala ya kusubiri maendeleo yatufikie, tunaamua kuyafikia huko yaliko!
 
mkuu mi sishangai...
Ukiangalia hizo nchi nyingi(za ulaya na america) hazikuibuka tu kwa cku 1 kuwa matajiri
Ukiangalia hizo nchi zimeanza kusaka maendeleo tangu mwishoni mwa karne ya karne ya 15...kipindi hicho ndicho uingereza ina anza mapinduzi ya kilimo(agrarian revolution) na baadae baada ya uhuru wakawa tayari wamefanya mapinduzi ya viwanda(industrial revolution)
Hapo ni kwa bi mkubwa Elizabeth pale uingereza.
Ukiangalia kwa umakini utaona bwana mapesa(Bilgate) alichosema ni cha kweli kabisa mkuu kwamba baada ya miaka 500 ndo tunaweza kufika level walipo wao!
Kweli. Ila umesahau jambo moja. Wakati nchi za Ulaya zinaendelea, hakuna na mazingira rafiki kama yaliyopo sasa: uelewa wa kisayansi na kitaaluma (skilled human resource), uwepo wa teknolojia ya hali ya juu, ubora wa huduma za afya na matibabu, uwepesi wa usafiri na usafirishaji n.k. Hivyo hatuhitaji kutumia muda mrefu kama waliotumia Ulaya. Na nchi kama Korea ya Kusini na Singapore zimeonyesha dhahiri hilo linawezekana. Korea miaka 50 iliyopita ilikuwa hoe hae. Singapore miaka 30 tu iliyopita ilikuwa hoe hae. Sasa zinatupa misaada watanzania!!
 
Africa ina refference ya kutosha linapo kuja swala la maendeleo, shida ipo kwenye kuitumia.
Tunalo weza ni lipi? kuuwa zeruzeru ili tutajirike???
 
Kweli. Ila umesahau jambo moja. Wakati nchi za Ulaya zinaendelea, hakuna na mazingira rafiki kama yaliyopo sasa: uelewa wa kisayansi na kitaaluma (skilled human resource), uwepo wa teknolojia ya hali ya juu, ubora wa huduma za afya na matibabu, uwepesi wa usafiri na usafirishaji n.k. Hivyo hatuhitaji kutumia muda mrefu kama waliotumia Ulaya. Na nchi kama Korea ya Kusini na Singapore zimeonyesha dhahiri hilo linawezekana. Korea miaka 50 iliyopita ilikuwa hoe hae. Singapore miaka 30 tu iliyopita ilikuwa hoe hae. Sasa zinatupa misaada watanzania!!
Ulichoongea ni ukweli mtupu mkurugenz tiger countries nyingi kipind cha hapo nyuma tu tulikuwa sawa kimaendeleo na nyingine tulizipita lakini leo tazma India ina watu muhimu sana ulimwenguni pote kwenye sector mbali mbali....ulichosema ni sahihi kabisa mkuu!
 
Wakuu nilikuwa nawatch CNN ya Marekani, nikamkuta yule tajiri number 2 duniani (Bill Gates) akiwa analiongelea bara la Africa kwa ujumla. Mwandishi wa CNN alimuuliza Bill Gates....kwa nini bara la Africa liko nyuma kwa kila kitu? tatizo ni nini?....Eti Bill akasema matatizo yako mengi sana, lakini makubwa sana ni -:

1.Kwanza walitawaliwa kwa mda mrefu

2.Elimu duni

3.Viongozi wa Afrca wanapenda kung'ang'ania madarakani

4.Demokrasia yao ni mdomoni tu.... na si matendo

5.Na vita za wenyewe kwa wenyewe zisizoisha.

Na mwisho akasema eti itachukua takribani miaka 500 bara la Africa kuwa kama America (Marekani) na Ulaya. Akaendelea kusema miaka 500....Africa watakuwa na siasa safi na uongozi bora, watu watakuwa educated, kutakuwa na viwanda vikubwa vya kutengeneza kila kitu, huduma safi za afya, barabara za juu, viwanja vizuri vya michezo yote, kutakuwa na timu kama Arsenal, Manchester, Real madrid nk. na vita za kung'ang'ania madaraka hazitakuwepo tena.

Kusema kweli mimi binafsi nilichoka na almanusra nidondoke chini kwa maneno ya huyu Bill Gates.....Yaani yameninyong'onyesha kabisaaa!.....miaka 500?
Hebu wanaJF tusaidiane tusaidiane kutafakari maneno ya huyu tajiri.... Je, kaongea kweli au uongo? - Nawasilisha
Ni ukweli kabisaaa hata hiyo 500 mbona bado ni kidogo. Asilimia kubwa sana ya watanzania hawana elimu hata ya darasa la kwanza.
 
1.Kwanza walitawaliwa kwa mda mrefu

2.Elimu duni

3.Viongozi wa Afrca wanapenda kung'ang'ania madarakani
4.Demokrasia yao ni mdomoni tu.... na si matendo

5.Na vita za wenyewe kwa wenyewe zisizo isha.
Hiyo vita ya wenyewe kwa wenyewe haiko mbali si mda mrefu itatokea. Na sijui mtaanzia wapi kutafuta amani baada ya hapo. Kama somalia ni nchi yenye dini na kabila moja lakini wako kwenue vita miaka yoooote hii.
 
Back
Top Bottom