Africa itachukua miaka 500 kuwa kama America na Ulaya- Bill Gates | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Africa itachukua miaka 500 kuwa kama America na Ulaya- Bill Gates

Discussion in 'International Forum' started by mshikachuma, Mar 17, 2011.

 1. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #1
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Wakuu nilikuwa nawatch CNN ya Marekani, nikamkuta yule tajiri number 2 duniani (Bill Gates) akiwa analiongelea bara la Africa kwa ujumla. Mwandishi wa CNN alimuuliza Bill Gates....kwa nini bara la Africa liko nyuma kwa kila kitu? tatizo ni nini?....Eti Bill akasema matatizo yako mengi sana, lakini makubwa sana ni -:

  1.Kwanza walitawaliwa kwa mda mrefu

  2.Elimu duni

  3.Viongozi wa Afrca wanapenda kung'ang'ania madarakani

  4.Demokrasia yao ni mdomoni tu.... na si matendo

  5.Na vita za wenyewe kwa wenyewe zisizoisha.

  Na mwisho akasema eti itachukua takribani miaka 500 bara la Africa kuwa kama America (Marekani) na Ulaya. Akaendelea kusema miaka 500....Africa watakuwa na siasa safi na uongozi bora, watu watakuwa educated, kutakuwa na viwanda vikubwa vya kutengeneza kila kitu, huduma safi za afya, barabara za juu, viwanja vizuri vya michezo yote, kutakuwa na timu kama Arsenal, Manchester, Real madrid nk. na vita za kung'ang'ania madaraka hazitakuwepo tena.

  Kusema kweli mimi binafsi nilichoka na almanusra nidondoke chini kwa maneno ya huyu Bill Gates.....Yaani yameninyong'onyesha kabisaaa!.....miaka 500?
  Hebu wanaJF tusaidiane tusaidiane kutafakari maneno ya huyu tajiri.... Je, kaongea kweli au uongo? - Nawasilisha
   
 2. fangfangjt

  fangfangjt JF-Expert Member

  #2
  Mar 17, 2011
  Joined: Apr 25, 2008
  Messages: 571
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 33
  kwa kasi ya ufisadi na uvivu wa watu hapa nchini, ongezea Tanzania miaka kama 100 zaidi
   
 3. Nyunyu

  Nyunyu JF-Expert Member

  #3
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 9, 2009
  Messages: 4,370
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 160
  Wewe kweli mshikachuma!!! Sasa cha ajabu hapo ni nini?

  Anza tu na kwako mwenyewe mkuu, hivi ulipiga kura kweli?
   
 4. The Prophet

  The Prophet JF-Expert Member

  #4
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 17, 2011
  Messages: 682
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  problemo ya ba-afirika ni rushwa umezidi sana. poja na rushwa afrika hibiwezi ku-developee kabisa.
   
 5. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #5
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Duuuh....mshikaji miaka 500 ni mingi sana! sasa kama ni hivyo ni bora kufa tu kuliko kuishi maisha haya ya moto....kwani miaka hiyo hatutaiona
   
 6. macho_mdiliko

  macho_mdiliko JF-Expert Member

  #6
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 10, 2008
  Messages: 6,434
  Likes Received: 2,303
  Trophy Points: 280
  1.Kwanza walitawaliwa kwa mda mrefu
  2.Elimu duni
  3.Viongozi wa Afrca wanapenda kung'ang'ania madarakani
  4.Demokrasia yao ni mdomoni tu.... na si matendo
  5.Na vita za wenyewe kwa wenyewe zisizo isha.
   
 7. A

  Alpha JF-Expert Member

  #7
  Mar 17, 2011
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 614
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Bila Elimu amna maendeleo.

  Korea was as poor as us less than 50 years ago now they are an advanced economy and among the top 10 economies in the world. They have no minerals, no oil, little land, no world class tourist attractions, etc.. What they have done is invest in their people. They work hard and they value education. TZ cannot develop without an educated hard working populace, it will not happen.
   
 8. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #8
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0

  Nimekukubali mkuu...... Ila hiyo namba 5 hata mie nashindwa kuitathimini kwa Tanzania
   
 9. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #9
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0


  Mkuu hapo kwenye red ndiyo tatizo kubwa..... i agree with u   
 10. M

  MILKYWAY GALAXY JF-Expert Member

  #10
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 12, 2008
  Messages: 201
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Mhhh!

  He could be right!

  kama tunawapa na tutaendelea kuwapa dhamana ya uongozi wa taifa letu watu dizaini ya hawa waliopo na wachumia tumbo wengine wanaowasapoti for sure hii ni sababu kubwa kuendelea kuogelea na kuzama kwenye lindi la umasikini, kukata tamaa na hatimaye kifo!
   
 11. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #11
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Sawa mkuu...... Lakini ni kweli miaka 500? au kaizidisha sana? mmh......
   
 12. B

  Babuyao JF-Expert Member

  #12
  Mar 17, 2011
  Joined: Jun 6, 2009
  Messages: 1,734
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  Nakubaliana Gates!

  Shida yetu kubwa ni ubinafsi katika yote. Mpaka tuje kupigana na mdudu huyo ndipo tutakapopiga hatua. Nakumbuka siku moja nilikuwa naongea na rafiki yangu mmoja (mzungu), tukawa tunaongelea matatizo yaliyopo barani la afrika kv rushwa/ufisadi, udikteta, matabaka katika jamii, uduni wa hudma za jamii.

  Yule jamaa akaniambia mpaka afrika ije kuendelea itahitaji kupigana vita vingi sana vya wenyewe kwa wenyewe; ndipo ije ifikie mahali sasa watawala na watawaliwa walazimike kukaa chini na kujenga mfumo unaojali raia wote. Jamaa aliongea haya akitolea mfano wa nchi yao: kwamba walipigana vita vingi sana na mwisho wakachoka ikabidi wakae na kutafuta suluhu kwa faida ya wote. Na matokeo yake ndiyo haya: kuna demokrasia, na kila raia anaheshimiwa na kuhudumiwa inavotakiwa.
   
 13. LINCOLINMTZA

  LINCOLINMTZA JF-Expert Member

  #13
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 15, 2011
  Messages: 1,640
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Ninavyomuelewa Gates kwamba kwa matatizo yaliyopo Afrika, maendeleo ni ndoto aka hayatatokea kabisa ndo maana ya miaka 500. Ila tukishughulikia matatizo yetu kama uongozi ambao ndo shina la matatizo yote, elimu na mengine yote, miaka hamsini ni mingi mno.

  Obama alipotembelea Ghana alisema kwamba nchi za Afrika nyingi zilipata uhuru miaka ya sitini kama Indonesia, lakini Indonesia leo hii ni matajiri na wanasaidia baadhi ya nchi za Afrika. We shall refute the dream of Gates immediately we get good governances.

  Chek hii

   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 14. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #14
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0

  Mkuu nimeicheck hizo video,......kweli tunakazi kubwa sana kufikia kilele cha mafanikio
   
 15. A

  Ame JF-Expert Member

  #15
  Mar 17, 2011
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 3,352
  Likes Received: 659
  Trophy Points: 280
  Mengine yote ni matokeo; lakini uongozi fake na ung'ang'anizi ndiyo kisa hasa cha matatizo ya bara hili. Hatuna ustaarabu wakukubali kushindwa na kuwaacha wengine wajaribu. Tunapenda sana kuwa maboss kuliko ku share talents na kila mmoja aka express tallent yake kuleta maendeleo. Utumwa umesaidia hii culture ya uboss maana ukifanyakazi kwaajili ya welfare unaonekana wewe ni kijakazi na huna thamani...Thamani ya utu wetu inatokana na majina zaidi kuliko utendaji ndiyo maana ukikosea ukamwita mwanasiasa jina lake bila kutanguliza 'Mheshimiwa, Profesor, Doctor, Engineer etc issue inaweza kufika bungeni ikawa kitu cha kujadiliwa badala ya kujadili real engineers, drs and the way they can improve the quality of their outputs...

  Tunaweza kuendelea kwa haraka zaidi kama tutapata comitted, abbled and principled leaders; ambao wako tayari kuachia vipaji kujitokeza na matendo yakawa identity ya ku qualify raia wetu bila kujali social status zao kuanzia wanasiasa, professionals na commoners..Mambo muhimu katika haya ni viongozi ambao wata dare ku enforce leagal measures kwa offenders huku benchmark ikiwa output na siyo statistics na documentations. Valuation na accounting yetu ifanywe kwenye physical assets na measurable indicators na siyo risiti za ku forgie pamoja na madocument yenye luga za kilagai.
   
 16. Selwa

  Selwa JF-Expert Member

  #16
  Mar 17, 2011
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 278
  Likes Received: 145
  Trophy Points: 60
  thats an awful lot, lakini kwa tuliyofanya kwa miaka hii 50 kadhaa....nasita mshua kakosea...mbona naitafuta hii statement siioni? wekeni link basi
   
 17. Nanren

  Nanren JF-Expert Member

  #17
  Mar 17, 2011
  Joined: May 11, 2009
  Messages: 1,739
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  And we have HARD TALKING populace.
  Talking about others,
  Talking about religions
  Talking about English premier league,
  Talking about sex,
  Talking about Loliondo,
  Hard talking always, instead of hard working.
  That is our TZ.
   
 18. L

  Leornado JF-Expert Member

  #18
  Mar 18, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Tatizo wasomi wengi wa africa wametimkia ughaibuni hivyo bara kubakia na illiterate people wengi na wasomi wachache ambao wamekubali kukandamizwa na utawala dhalimu wa viongozi wa africa. Hamna ile morale ya kufanya kazi kujenga nchi.

  Pia wataalam wengi Africa wameacha fani zao manake hazilipi na kuwa wanasiasa, kunamaendeleo kweli hapo?
   
 19. Ehud

  Ehud JF-Expert Member

  #19
  Mar 22, 2011
  Joined: Feb 12, 2008
  Messages: 2,696
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 0
  Mi naona katupendelea kama tutaendelea kuwa na aina ya viongozi tulionao itatuchukua miaka 2000 kuwa sawa na EU au America
   
 20. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #20
  Mar 22, 2011
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  lol. Swala ni, USA, EU watakuwa wapi.. Naomba niwasilishe mawazo ya waandishi wa futuretimeline.com based on current scientific research lines and political dynamics.

  Onyo: Maendeleo hasa yakiteknolojia yanakua kwa mwendo ambao ni exponential rather than linear. Msishangae sana baadhi ya mawazo humu ndani (ikitokea kushagaa sana jaribu kukumbuka dunia miaka 100 iliyopita ama 200)

  2050... http://www.futuretimeline.net/21stcentury/2050-2059.htm

  2100... Mind Uploading | Terraforming Timeline | Space Elevator | Femtoengineering | Femtotechnology | Technological Singularity | 22nd century | Future | Timeline | 2050 | 2100 | 2150 | 2200

  2150... Mind Uploading | Terraforming Timeline | Space Elevator | Femtoengineering | Femtotechnology | Technological Singularity | 22nd century | Future | Timeline | 2050 | 2100 | 2150 | 2200

  2200... http://www.futuretimeline.net/23rdcentury/2200-2249.htm


  This is only 200-250 years into the future. Look beyond utacheka. But by this time people may acquire virtual immortality through things like mind uploading and other trans humanist activities.
   
Loading...