Kama Bill Gates ataamua kwa siku moja awe anatumia USD milioni 1 itamchukua miaka zaidi ya 279 kumaliza utajiri wake

TEAM 666

JF-Expert Member
Dec 7, 2017
4,330
8,420
#UNAAMBIWA Kama Bilionea wa Dunia Bill Gates ataamua kuwa kwa siku moja awe anatumia USD MILIONI 1 ( Tsh . Bilioni 2.3 ) basi itamchukua miaka zaidi ya 279 kumaliza utajiri wake.

Bill.JPG

Bill Gates ambaye ni Mwanzilishi wa Microsoft , mwaka 2017 alirudi juu na kushika nafasi ya kwanza katika Watu tajiri Duniani baada ya kuongeza utajiri wake kutoka USD 75 Bilioni hadi USD 86 Bilioni , ingawa kwa sasa namba moja inashikiliwa na Jeff Bezos , mmiliki wa Amazon ambaye utajiri wake unakadiriwa kuwa USD 171 Bilion

Je hapo ulipo ukisema utumie Elfu 50 kila weekend kufanya shopping PALM VILLAGE MIKOCHENI kapu lako litadumu kwa muda gani ?
 
Kipindi tu cha corona nilikaa nyumbani miezi miwili nakula tu bila kuingiza mia, niliishiwa nikakopa sana... wiki ijayo ndo natarajia kumalizia kulipa madeni.

Wengi wetu tunaishi around the number line, leo unaingia chanya kesho upo hasi.
 
Hizo pesa hewa tu aisee. Tanzania tuna kila kitu. Nilitegemea nchi yenye watu kama hao usingetegemea kukuta vichangamoto vidogo kama vilivyo katika nchi za ulimwengu wa tatu. Sasa faida iko wapi??? Kovidi-19 inalamba watu zaidi ya 3000 kwa siku! Bure kabisa. Afadhali mtu awe maskini kama Matonya lakini kuna hope ya kesho.
 
Ila hizo pesa ni katika mfumo wa hisa tu, leo akitaka kugeuza assets na hisa zake into tangible cash at once, basi thamani ya hisa zake na assets zitashuka pengine to 30 billion dollars, stock markets hucheza accordingly kitu kikiuzwa kwa wingi. Hana hiyo pesa, muangalie Mo dewji anavyoganga njaa huku mshahara wake ukiwa haumtoshi hata kidogo, ndio utaelewa
 
Jaribu kua serious
 
Ndo maneno ya maskin haya.siku zote...maneno ya mtu ambae amesha surender
 
Acha uwongo...hapo aweke hiyo yote kwenye betting
Man city vs majimaji fc
alafu ampe Majimaji anashinda 3+
 
Ila hizo pesa ni katika mfumo wa hisa tu, leo akitaka kugeuza assets na hisa zake into tangible cash at once, basi thamani ya hisa zake na assets zitashuka pengine to 30 billion dollars, stock markets hucheza accordingly kitu kikiuzwa kwa wingi. Hana hiyo pesa, muangalie Mo dewji anavyoganga njaa huku mshahara wake ukiwa haumtoshi hata kidogo, ndio utaelewa
Mkuu ahsante kwa kunifungua macho,Nlikua sijui Kama Mo dewji analipwa mshahara.
 
Back
Top Bottom