Afisa uhamiaji Mwanza aliyenusurika kuuawa na polisi ashambuliwa kwa nondo!

matongo manawa

JF-Expert Member
Apr 6, 2011
336
79
Habari nilizozipata punde ni kwamba Yule afisa uhamiaji aliyekoswa koswa na kijana wa marehemu Barlow kwa risasi, usiku wa kuamkia leo alishambuliwa na watu wasiokulikana na kupigwa nondo kichwani.

Afisa huyo kwa sasa amelazwa ktk hosp ya Bugando na Hali yake si nzuri sana.

Ikimbukwe kwamba juzi baada ya kunisurika kuuawa alimtupia lawama afisa wa polisi Abuu kuhusika na mipango Ya kumwua kutokana na kuwa na mahusiano yasiyofaa na mke wake hali iliyopelekea kuwa na Kesi ya kutalakiana.

Lakini pia ikumbukwe kwamba baada ya kulituhumu jeshi La polisi, kamanda Barlow Alipinga na kukanusha tuhuma hizo kwa nguvu zote akidai kuwa aliingia kwenye mtego wa Polisi muda ule ule na gari lile.

Kamanda Barlow aliuawa jana majambazi kwa kupigwa risasi alipokuwa akimrudisha nyumbani dada yake wakitokea kwenye kikao cha harusi Kati ya saa saba na saa nane usiku.

Nitawajuza zaidi.
 
Maafisa usalama hebu lishughurikieni jambo hili la Mwanza na matukio mengine kwa umakini vinginevyo ni aibu kwa system nzima.
 
Mwanza imeanza kuniogopesha kuja huko na mai wife wangu
mapolisi wa uko wanachukuwa wake za watu kinguvu au mke anakwenda mwenye?
duuu inatisha watu wanachukuliana utazani wanakaa kota za polisi
 
Nanyanyua mikono juu!!! Hivi hii ni ile Tanzania ya amani na usalama? Mtukufu Rais upo?
 
Mwanza imeanza kuniogopesha kuja huko na mai wife wangu
mapolisi wa uko wanachukuwa wake za watu kinguvu au mke anakwenda mwenye?
duuu inatisha watu wanachukuliana utazani wanakaa kota za polisi

mwenye nia na nchi yake atarudi tu, huna nia ya kurudi wala nini... unatafuta excuses tu
 
Habari nilizozipata punde ni kwamba Yule afisa uhamiaji aliyekoswa koswa na kijana wa marehemu Barlow kwa risasi, usiku wa kuamkia leo alishambuliwa na watu wasiokulikana na kupigwa nondo kichwani.

Afisa huyo kwa sasa amelazwa ktk hosp ya Bugando na Hali yake si nzuri sana.

Ikimbukwe kwamba juzi baada ya kunisurika kuuawa alimtupia lawama afisa wa polisi Abuu kuhusika na mipango Ya kumwua kutokana na kuwa na mahusiano yasiyofaa na mke wake hali iliyopelekea kuwa na Kesi ya kutalakiana.

Lakini pia ikumbukwe kwamba baada ya kulituhumu jeshi La polisi, kamanda Barlow Alipinga na kukanusha tuhuma hizo kwa nguvu zote akidai kuwa aliingia kwenye mtego wa Polisi muda ule ule na gari lile.

Kamanda Barlow aliuawa jana majambazi kwa kupigwa risasi alipokuwa akimrudisha nyumbani dada yake wakitokea kwenye kikao cha harusi Kati ya saa saba na saa nane usiku.

Nitawajuza zaidi.

mkuu 2nashukuru sana endelea ku2pa tarifa zaidi zinazo endelea
 
Back
Top Bottom