Afisa Manunuzi anaandika kununua Vitu ambavyo Vipo Stoo

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,909
945
AFISA MANUNUZI ANAANDIKIA KUNUNUA VITU AMBAVYO VIPO STOO

"Hospitali ya Wilaya Rorya imejengwa kwa miaka 10, na inashindwa kukamilika kwa sababu ya utaratibu wa manunuzi waliouweka. Na utaratibu huu wanaoufanya Hospitali maana yake ni nini, mtu wa manunuzi ni yuleyule, engineer ni yuleyule ambae anasimamia miradi mingine ambayo Serikali inaweka fedha. Kwa tulichokiona hapa tusipoweka macho nina wasiwasi na miradi mingine yote" - Mhe. Jafari Chege, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Nafikiri ilikuwa mwezi wa 4 au wa 5 Baraza la madiwani tulimsimamisha Afisa manunuzi na Engineer na ndio nikaja na hio hoja kumuomba Mhe. Waziri wa TAMISEMI akatazame. Serikali imetoa zaidi ya Milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa jengo la mama na mtoto lakini halijakamilika ila Wilaya nyingine wamekamilisha majengo yao" - Mhe. Jafari Chege, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Nilipokuwa nachangia hoja Wizara ya TAMISEMI katika Bunge la Bajeti la mwezi wa 6, nilimuomba Mhe. Waziri wa TAMISEMI kama anaweza kufanya ziara moja kujiridhisha na utaratibu wa manunuzi unaofanywa na aina ya Ujenzi unaofanywa Hospitali ya Wilaya ya Rorya" - Mhe. Jafari Chege, Mbunge wa Jimbo la Rorya

"Nilitoa mfano kuwa manunuzi yanayofanyika pale unakuta stoo kuna mifuko 50 au 200 ya Cement lakini bado watu wa manunuzi wanafanya tena taratibu za kununua Cement nyingine tofauti na ile iliyopo stoo au kuna mradi A ambao zilibaki ndoo au madumu 200 ya rangi wakienda kwenye mradi mwingine wanaandika manunuzi upya" - Mhe. Jafari Chege, Mbunge wa Jimbo la Rorya.

 
Back
Top Bottom