Mbunge Jafari Chege Ahoji Wakurugenzi Waliosababisha Upotevu wa Fedha Wamechukuliwa Hatua Gani?

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
May 16, 2020
1,902
945

MBUNGE JAFARI CHEGE AHOJI WAKURUGENZI WALIOSABABISHA UPOTEVU WA FEDHA WAMECHUKULIWA HATUA GANI?

"Nampongeza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa namna anavyowajibika kuhakikisha anadumisha na kuridisha uzalendo na uimara katika fedha za Serikali kwenye miradi mbalimbali. Ofisi ya CAG ametimiza wajibu wake" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya.

"Nashauri tupitie mapendekezo ya Bunge ya taarifa ya CAG kwa miaka miwili au mitatu iliyopita kabla hatujaanza kupitia mapendekezo ya mwaka 2023. Tutakuwa tunadhibiti na kuimarisha mapendekezo ya Bunge, Bunge linapotoa mapendekezo kwenda kufanyiwa kazi uimara wa taarifa uweze kufanyika" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya.

"Mwaka 2022 taarifa ya CAG ilionekana fedha za Mikopo kwa Vijana, Wanawake na wenye ulemavu zaidi ya Shilingi Bilioni 47 zilienda mahali ambapo pana utata hazieleweki. Mwaka 2023 taarifa ya CAG inazungumzia zaidi ya Shilingi Bilioni 88 matumizi yake hayaeleweki" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya.

"Kujadili upotevu wa Shilingi Bilioni 88 tukaacha kupata maelekezo ya Serikali na Wizara husika hatua walizochukua kwa Wakurugenzi, Maafisa Maendeleo na Wakuu wa Idara waliosababisha hasara ya Bilioni 77 maana yake tunaacha kiporo. Mwaka 2024 tunaweza kujadili zaidi ya Bilioni 88, uendelevu huu ni lazima tuhakikishe tunausimamia" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya.

"Bunge tumetunga sheria, mwananchi akinunua bidhaa adai risiti na asipoomba risiti mwananchi mnyonge wa Kijijini anatakiwa kulipa million 3. Serikali imefanya malipo zaidi ya Shilingi Bilioni 10 na hawajaomba risiti ya Kielektroniki lakini wamelipa fedha. Nani anayewajibika hapa, Waziri atuambie Wakurugenzi waliolipa fedha bila risiti za Kielektroniki wako wapi, Wamefukuzwa au wako kwa mujibu wa sheria Mahakamani" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya.

"Fedha ya POS Shilingi Bilioni 11 hazikupelekwa benki, Wakurugenzi na Wakuu wa Idara wamezipelekq wapi. Waziri aseme hawa Wakurugenzi waliosababisha upotevu wa fedha nyingi wapo wapi na usiseme umewahamisha kutoka sehemu A kwenda sehemu B" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya.

"Ni chombo gani kinachowasimamia TAKUKURU? Mkuu wa Wilaya, Mkuu wa Mkoa, Mawaziri na Waziri Mkuu wakienda kukagua miradi na kukuta ubadhirifu wanasema hili liende TAKUKURU. Tuacha yaliyopo kwenye taarifa ya CAG, nani anayesimamia TAKUKURU? TAKUKURU ni kichaka cha taarifa mbalimbali. Chombo kinachosimamia TAKUKURU hakitimizi majukumu yake" - Mhe. Jafari Chege Wambura, Mbunge wa Jimbo la Rorya.


 
Back
Top Bottom