Afisa Elimu Msingi (W) Magu, rekebisha uongozi wa Shule ya Msingi Magu

Kaji Bagome

Member
Nov 5, 2019
15
21
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kazi iendelee, sawa; moja kwa moja kwenye Mada.

DEO Msingi (W) Magu, napenda kukujulisha kwamba, uongozi wa Shule ya Msingi Magu umepwaya, kiasi kwamba mshikamano wa waalimu shuleni hapo haupo; waalimu wamegawanywa na Mwalimu Mkuu EZEKIEL NJALLA; kiasi kwamba waalimu walio wengi shuleni hapo wameelekea kutokufungamana na Mwalimu Mkuu huyo kwa sababu ni mnyanyasaji, iwe ofisini kwake, ofisi za waalimu, vikaoni na hata mbele ya wanafunzi.

Ana waalimu wake wapendwa wawili tu (majina kapuni) kati ya waalimu wote walioko shuleni hapo; lakini wengine wote hawaonekani kama wanastahili mbele ya Mwalimu Mkuu Njalla.

Waalimu wake wapendwa hao, sasa hivi wameachiwa wao wawili tu moja ya ofisi za waalimu mbili zilizopo shuleni hapo; na waalimu wengine wote wamabanana kwenye ofisi moja (isipokuwa yeye Mwalimu Mkuu ambaye ana ofisi yake).

Kebehi, vitisho na kudhalilisha waalimu ndio umekuwa utaratibu wa uongozi kwa Mwalimu Mkuu huyo.

Waalimu wananyimwa ruhusa za kutoka shuleni wanapokuwa na dharula, ziwe za kuuguliwa, kuhudhuria mazishi n.k; mambo ambayo kijamii yana athari; maana waalimu wanaishi miongoni mwa jamii.

Mwalimu Mkuu EZEKIEL NJALLA na hao wapendwa wake wawili, waliwachangisha watoto wa darasa la nne shs. 5,000/= kila mmoja; ambapo walikusanya zaidi ya shs 600,000/=; kwa maelezo kwamba pesa hizo zingetumika kuwapa posho waalimu wa darasa hilo la mtihani wakati wa likizo ya sensa.

Matokeo yake, waalimu hao wa darasa la mtihani wasiozidi watatu (majina kapuni) waliambulia shs. 20,000/= kila mmoja; jumla kama shs. 60,000/=, na kiasi kilichobaki kikahodhiwa na Mwalimu Njalla na waalimu wapendwa wake wawili.

Jambo hilo lilichochea mtafaruku zaidi, ambapo waalimu walikwenda kulalamika kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Shule Bwana Omedi aliyemkabili Mwalimu Mkuu Njalla, ndipo akawaongezea waalimu hao posho hiyo na kuwa shs. 60,000 kila mmoja na akatoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Shule kwamba fedha zingine kiasi cha shs. 200,000/= amelipia kuchapisha mitihani; jambo ambalo siyo la kweli, kwa sababu watoto hao wa darasa la nne HAWAKUFANYA MTIHANI WOWOTE, zaidi ya mitihani ambayo wazazi wao walikuwa wanachangia kila mwezi kama walivyokubaliana kwenye kikao kati yao na Mwalimu Njalla, Mwalimu wa Taaluma Madam Aisha, na Mwalimu wa Fedha Madam Msaki; ambapo pia palikuwa na makubaliano ya wazazi kuchangia chakula kwa ajili ya watoto hao wa darasa la nne ili wabaki shuleni muda mrefu.

Kwa mtafaruku huo waalimu waligoma kuwafundisha watoto wakati wa likizo ya sensa; pesa shs zaidi ya 600,000/= zikawa zimeliwa bure tu na Mwalimu Njalla na waalimu wake!

Hili linavunja moyo wa wazazi kujitolea, maana wanaona kama wanachanga ili kuwanufaisha tu waalimu. Wazazi wanachangia Ulinzi shuleni, Bill ya Maji shuleni, japo bomba la maji kwenye Shule ya Msingi Magu maji hayatoki.

Watoto wa Shule ya Msingi Magu kutwa wanazurura na vidumu au vikopo wakiombaomba maji ya kunywa kwenye miji ya jirani na shule; wakati bomba liko shuleni lakini halitoi maji kwa sababu ya bill, wakati wazazi wanachangia, hii ni aibu!

Mbona bomba la maji pale Nyalikungu Shule ya Msingi maji yanatoka mpaka vyooni? Hii ni dhahiri kwamba uongozi wa Shule ya Msingi Magu hauko serious.

Sijui Kama hata huyo mlinzi kweli huwa analipwa pesa yake ya ulinzi au tusubiri mgogoro mwingine. DEO chukua hatua; unao waalimu wengi Sana wenye uwezo kwenye Wilaya hii.

Najua hapo ofisini kwako wapo watu wanaokukwamisha, usikubali kukwamishwa, ng'oa hivyo vigingi ili usonge mbele; vinginevyo utang'olewa wewe, maana utasomeka kuwa "hutoshi" kuwa DEO wakati siyo kweli; unafanya kazi nzuri Sana kwenye wilaya hii; na waalimu wengi wanakukubali; shida ni hapo ofisini kwako na kwa baadhi ya ma-AEK.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Kazi iendelee.
 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...Kazi iendelee, sawa; moja kwa moja kwenye Mada.

DEO Msingi (W) Magu, napenda kukujulisha kwamba, uongozi wa Shule ya Msingi Magu umepwaya, kiasi kwamba mshikamano wa waalimu shuleni hapo haupo...
Duuh
 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...Kazi iendelee, sawa; moja kwa moja kwenye Mada.

DEO Msingi (W) Magu, napenda kukujulisha kwamba, uongozi wa Shule ya Msingi Magu umepwaya, kiasi kwamba mshikamano...
Cc. Afisa Usalama wa Wilaya, Takukuru Wilaya, Mkurugenzi wa Wilaya, DHRO
 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...Kazi iendelee, sawa; moja kwa moja kwenye Mada.

DEO Msingi (W) Magu, napenda kukujulisha kwamba, uongozi wa Shule ya Msingi Magu umepwaya, kiasi kwamba mshikamano wa waalimu shuleni hapo haupo; waalimu wamegawanywa na Mwalimu Mkuu EZEKIEL NJALLA; kiasi kwamba waalimu walio wengi shuleni hapo wameelekea kutokufungamana na Mwalimu Mkuu huyo kwa sababu ni mnyanyasaji, iwe ofisini kwake, ofisi za waalimu, vikaoni na hata mbele ya wanafunzi.

Ana waalimu wake wapendwa wawili tu (majina kapuni) kati ya waalimu wote walioko shuleni hapo; lakini wengine wote hawaonekani kama wanastahili mbele ya Mwalimu Mkuu Njalla.

Waalimu wake wapendwa hao, sasa hivi wameachiwa wao wawili tu moja ya ofisi za waalimu mbili zilizopo shuleni hapo; na waalimu wengine wote wamabanana kwenye ofisi moja (isipokuwa yeye Mwalimu Mkuu ambaye ana ofisi yake).

Kebehi, vitisho na kudhalilisha waalimu ndio umekuwa utaratibu wa uongozi kwa Mwalimu Mkuu huyo.
Waalimu wananyimwa ruhusa za kutoka shuleni wanapokuwa na dharula, ziwe za kuuguliwa, kuhudhuria mazishi n.k; mambo ambayo kijamii yana athari; maana waalimu wanaishi miongoni mwa jamii.

Mwalimu Mkuu EZEKIEL NJALLA na hao wapendwa wake wawili, waliwachangisha watoto wa darasa la nne shs. 5,000/= kila mmoja; ambapo walikusanya zaidi ya shs 600,000/=; kwa maelezo kwamba pesa hizo zingetumika kuwapa posho waalimu wa darasa hilo la mtihani wakati wa likizo ya sensa.

Matokeo yake, waalimu hao wa darasa la mtihani wasiozidi watatu (majina kapuni) waliambulia shs. 20,000/= kila mmoja; jumla kama shs. 60,000/=, na kiasi kilichobaki kikahodhiwa na Mwalimu Njalla na waalimu wapendwa wake wawili.

Jambo hilo lilichochea mtafaruku zaidi, ambapo waalimu walikwenda kulalamika kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Shule Bwana Omedi aliyemkabili Mwalimu Mkuu Njalla, ndipo akawaongezea waalimu hao posho hiyo na kuwa shs. 60,000 kila mmoja na akatoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Shule kwamba fedha zingine kiasi cha shs. 200,000/= amelipia kuchapisha mitihani; jambo ambalo siyo la kweli, kwa sababu watoto hao wa darasa la nne HAWAKUFANYA MTIHANI WOWOTE, zaidi ya mitihani ambayo wazazi wao walikuwa wanachangia kila mwezi kama walivyokubaliana kwenye kikao kati yao na Mwalimu Njalla, Mwalimu wa Taaluma Madam Aisha, na Mwalimu wa Fedha Madam Msaki; ambapo pia palikuwa na makubaliano ya wazazi kuchangia chakula kwa ajili ya watoto hao wa darasa la nne ili wabaki shuleni muda mrefu.

Kwa mtafaruku huo waalimu waligoma kuwafundisha watoto wakati wa likizo ya sensa; pesa shs zaidi ya 600,000/= zikawa zimeliwa bure tu na Mwalimu Njalla na waalimu wake!!.

Hili linavunja moyo wa wazazi kujitolea, maana wanaona kama wanachanga ili kuwanufaisha tu waalimu.
Wazazi wanachangia Ulinzi shuleni, Bill ya Maji shuleni, japo bomba la maji kwenye Shule ya Msingi Magu maji hayatoki.

Watoto wa Shule ya Msingi Magu kutwa wanazurura na vidumu au vikopo wakiombaomba maji ya kunywa kwenye miji ya jirani na shule; wakati bomba liko shuleni lakini halitoi maji kwa sababu ya bill, wakati wazazi wanachangia, hii ni aibu!!

Mbona bomba la maji pale Nyalikungu Shule ya Msingi maji yanatoka mpaka vyooni? Hii ni dhahiri kwamba uongozi wa Shule ya Msingi Magu hauko serious.

Sijui Kama hata huyo mlinzi kweli huwa analipwa pesa yake ya ulinzi au tusubiri mgogoro mwingine.
DEO chukua hatua; unao waalimu wengi Sana wenye uwezo kwenye Wilaya hii.

Najua hapo ofisini kwako wapo watu wanaokukwamisha, usikubali kukwamishwa, ng'oa hivyo vigingi ili usonge mbele; vinginevyo utang'olewa wewe, maana utasomeka kuwa "hutoshi" kuwa DEO wakati siyo kweli; unafanya kazi nzuri Sana kwenye wilaya hii; na waalimu wengi wanakukubali; shida ni hapo ofisini kwako na kwa baadhi ya ma-AEK.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania...Kazi iendelee.
Tafuta hela dogo, chuki, majungu hazitakupeleka popote. Kama kweli mwlimu ana mapungufu kwa nn usimpeleke kwa viongozi wake
 
Mwandishi wewe ni mwalimu WA hiyo shule hivyo ulipaswa kwanza utangaze maslahi yako kwanza ndipo utoe hiyo habari.

Sasa kwanamna ulivyoiweka kwamba ionekane mwandishi ni mzazi kaandika hayo wakati ukiisoma hiyo habari vzr Kuna sehemu unajionesha ni wewe mwalimu.Hapo ndipo inapokosa credibility ya habari yako na kuonekana unapiga majungu.
 
Back
Top Bottom