Afariki kwa ajali ya 'ungo' jioni hii

Afariki kwa ajali ya 'ungo' jioni hii

Hii kitu ya ungo ni imagination haiwezekani hata kidogo eti mtu apande kwenye ungo.

1. Serikari ifanye uchunguzi wa kina yawezekana watu wamefanya mauaji halafu waka plot scene ili kufunika uovu wao

2. Kwa kuwa jamii ilishalishwa dhana ya uongo ya watu kusafiri na ungo wamekuwa obsessed na illusion hiyo na hivyo kufunika hata uwezo wao wa kufikiri nje ya box na kubakia wakiamini kile wanachokiona na macho ya kawaida.

3. Ni mara nyingi watu wameshambuliwa na wengine hata kuuawa kwa imani za kijinga kama hizo pale ambapo waganga matapeli wa kienyeji wanapo kula deal na mtu kwa kumpaka mazizi na kumbebesha ungo na kujifanya eti amemtungua kwa nguvu zake ili apate wateja.

Hivyo , mtu huyo achunguzwe ni wawapi, ndugu zake, mara ya mwisho alionekana na nani au aliwasiliana na nani au alikuwa na uadui na nani.
Hakuna darasa litakalokufundisha mambo ya rohoni. Usipende kubisha mambo usiyoyajua kwa kuwa huyajui na hakuna maabara ya kuthibitisha.
 
Hiyo ndege itakuwa imedunguliwa na waasi au hakutoa taarifa kama atapita eneo hilo.
 
Huyu alikutana na nguvu za maombi Ungo ukakosa mwelekeo.
 
MCHAWI MWENYEWE ALIKUWA MVIVU WA KUNYOA,.NAONA KICHAKA CHA ZIVU AU MACHO YANGU?
 
Unaweza kujuta mzee wa watu 'kalewa' kutokana na 'herbs' alizokunywa/nusa wakati wa kutambika, kisha kupoteza fahamu na kuanguka (trip not fall), wabongo wanadai kadondoka kutoka angani. Kuna aliyemuona?

Kiranga vipi hii?
Huyo tena na ungo wanamtafutia na kumbambikia kabisa kutimiza imani zao.

Bongo kila daktari mmoja ana wananchi 40,000 wa kuwahudumia, hao ni madaktari tu wa kawaida.

Siwezi kushangaa nikiambiwa ratio ya qualified mental health professionals kama kina Prof. Kilonzo wale ni 1:400,000

Halafu watu wepesi kukimbilia uchawi kabla hata ya kuchunguza vitu.
 
Inashangaza sana Watanzania wengi haraka sana kuamini mambo ya "kijinga" kwelikweli. Hao watu wanaodhaniwa "wamedondoka na ungo" ukichunguza vizuri utagundua si kweli. Noma sana hii jamii yetu.
 
nimecheka sana thread hii hasa comments
 
Mzee asiejulikana ameanguka na ungo maeneo ya Kijichi, pichani maiti ya mzee huyo ikishushwa ktk Gari ya polisi na kuihifadhi maiti ktk mortuary ya TMK Hospital
7d19334e3f10c6f1486b0e0b240b65d8.jpg
 
Back
Top Bottom