Tufike mahala tuseme ukweli hata kama ni mchungu, IGP Simon Sirro alijua fika kuwa mkutano wake umehudhuriwa na waandishi wa Habari na kwamba chochote akisemacho kitaufikia umma.
Yako mengi ameyasema ambayo ni ya maana sana but kuna moja nadhani kateleza. Ni kweli dressing code ya Polisi Tanzania inapashwa kufuatwa, Hata hivyo; kitendo cha IGP Sirro kumshambulia Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Afande Mambosasa, sio cha kiungwana.
Mavazi aliyomsema ndo na yeye amewahi kuyavaa na sio kwamba alikuwa porini au kwenye operation, aliyavaa kwenye “Press.” Swali je! Kajua umuhimu wa dress code leo, au ilikuwa ni nia ya kurudisha mashambulizi kwa Afande Mambosasa ambaye kimsingi ameonekana kufanya “vizuri” zaidi yake wakati akiwa Kamanda wa Kanda hiyo!
Nadhani kwa uungwana, ni vema na ni busara kwa Afande Sirro kumuomba msamaha Afande Mambosasa. Kama kweli anahuburi umoja ndani ya polisi, basi hakupaswa kutaja jina la Afande Mambosasa; angekemea kwa ujumla na ndo hapo nasema IGP Sirro kateleza.
Katika picha, ni vazi la kipolisi (jungle) ambalo ni maalum kwaajili ya oparesheni, na IGP Sirro kakemea kuwa halipaswi kuvaliwa wakati wa “press,” hata hivyo, katika uchunguzi wangu mdogo mitandaoni, umeonyesha kuwa yeye mwenyewe Afande Sirro, ni mvaaji mzuri wa vazi hilo nje ya oparesheni.
View attachment 1216030View attachment 1216031View attachment 1216032View attachment 1216034View attachment 1216035