Afande Sirro tafadhali mtake radhi Afande Mambosasa

Dickson Ng'hily

JF-Expert Member
Joined
Oct 22, 2010
Posts
473
Reaction score
508
Tufike mahala tuseme ukweli hata kama ni mchungu, IGP Simon Sirro alijua fika kuwa mkutano wake umehudhuriwa na waandishi wa Habari na kwamba chochote akisemacho kitaufikia umma.

Yako mengi ameyasema ambayo ni ya maana sana but kuna moja nadhani kateleza. Ni kweli dressing code ya Polisi Tanzania inapashwa kufuatwa, Hata hivyo; kitendo cha IGP Sirro kumshambulia Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Afande Mambosasa, sio cha kiungwana.

Mavazi aliyomsema ndo na yeye amewahi kuyavaa na sio kwamba alikuwa porini au kwenye operation, aliyavaa kwenye “Press.” Swali je! Kajua umuhimu wa dress code leo, au ilikuwa ni nia ya kurudisha mashambulizi kwa Afande Mambosasa ambaye kimsingi ameonekana kufanya “vizuri” zaidi yake wakati akiwa Kamanda wa Kanda hiyo!

Nadhani kwa uungwana, ni vema na ni busara kwa Afande Sirro kumuomba msamaha Afande Mambosasa. Kama kweli anahuburi umoja ndani ya polisi, basi hakupaswa kutaja jina la Afande Mambosasa; angekemea kwa ujumla na ndo hapo nasema IGP Sirro kateleza.

Katika picha, ni vazi la kipolisi (jungle) ambalo ni maalum kwaajili ya oparesheni, na IGP Sirro kakemea kuwa halipaswi kuvaliwa wakati wa “press,” hata hivyo, katika uchunguzi wangu mdogo mitandaoni, umeonyesha kuwa yeye mwenyewe Afande Sirro, ni mvaaji mzuri wa vazi hilo nje ya oparesheni.
0DDF9479-5183-4971-8134-B16589C6F082.jpeg
C90844A2-1FBB-4ADB-A1E8-2A33A25BF3F7.jpeg
09D22DAC-2563-47AD-9A36-7CE094E31E35.jpeg
7307492B-6558-4492-A885-0B2C3563610F.jpeg
95180D6D-1F66-45E4-A3C4-39A4F916D8C2.jpeg
 
Sema utakacho, lakini IGP Sirro amesema jeshi la polisi linatumika kisiasa na ndio hasa linaloibeba ccm. Na ameonyesha kujutia dhambi ya kuingilia siasa na kuwa mbeleko ya kuibeba ccm mpaka makada wa ccm wamegeuka kuwadhalilisha polisi. Uzuri ni kwamba amekiri yanayofanywa na jeshi la polisi wakiingia mitandaoni wanakutana na ukweli kuhusu huo ujinga wao, ambao kwa dhamira yake unamsuta. Kwa hiyo kama Sirro sio mnafiki, ccm wajiandae kushindana kisiasa kwani mbeleko inaanza kujitambua.
 
Yani kuna watu siasa zilishawafanya mjifanye mnajua na hamjui kitu...kila tukio ni siasa,kila kitu kidogo cha watu na mambo yao ni ccm,siku je mkija kujua hata Mbowe ni ccm sijui mtafanya nini.jengeni hekima na busara kufanya kazi zenu na ya watu muyaache yaendelee..kimbele mbele wakati mwingine kinaweza kukufedhehesha
 
Tufike mahala tuseme ukweli hata kama ni mchungu, IGP Simon Sirro alijua fika kuwa mkutano wake umehudhuriwa na waandishi wa Habari na kwamba chochote akisemacho kitaufikia umma.

Yako mengi ameyasema ambayo ni ya maana sana but kuna moja nadhani kateleza. Ni kweli dressing code ya Polisi Tanzania inapashwa kufuatwa, Hata hivyo; kitendo cha IGP Sirro kumshambulia Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Afande Mambosasa, sio cha kiungwana.

Mavazi aliyomsema ndo na yeye amewahi kuyavaa na sio kwamba alikuwa porini au kwenye operation, aliyavaa kwenye “Press.” Swali je! Kajua umuhimu wa dress code leo, au ilikuwa ni nia ya kurudisha mashambulizi kwa Afande Mambosasa ambaye kimsingi ameonekana kufanya “vizuri” zaidi yake wakati akiwa Kamanda wa Kanda hiyo!

Nadhani kwa uungwana, ni vema na ni busara kwa Afande Sirro kumuomba msamaha Afande Mambosasa. Kama kweli anahuburi umoja ndani ya polisi, basi hakupaswa kutaja jina la Afande Mambosasa; angekemea kwa ujumla na ndo hapo nasema IGP Sirro kateleza.

Katika picha, ni vazi la kipolisi (jungle) ambalo ni maalum kwaajili ya oparesheni, na IGP Sirro kakemea kuwa halipaswi kuvaliwa wakati wa “press,” hata hivyo, katika uchunguzi wangu mdogo mitandaoni, umeonyesha kuwa yeye mwenyewe Afande Sirro, ni mvaaji mzuri wa vazi hilo nje ya oparesheni.View attachment 1216030View attachment 1216031View attachment 1216032View attachment 1216034View attachment 1216035

Mkuu kumbuka Mambosasa alienda kunywa chai na Mo baada ya kutekwa?
 
Yani kuna watu siasa zilishawafanya mjifanye mnajua na hamjui kitu...kila tukio ni siasa,kila kitu kidogo cha watu na mambo yao ni ccm,siku je mkija kujua hata Mbowe ni ccm sijui mtafanya nini.jengeni hekima na busara kufanya kazi zenu na ya watu muyaache yaendelee..kimbele mbele wakati mwingine kinaweza kukufedhehesha

Unaweza kulitenganisha jeshi hili au vyombo vyetu vya dola na siasa? Kama rais mwenyewe aliona jeshi nalo liko kisiasa mpaka akapokea wanaccm kwenye kamisheni ya jeshi, ndio itakuwa hiyo press ya jeshi la polisi? Hebu niambie unaweza vipi kulitenga jeshi la polisi na siasa, hasa siasa za ccm?
 
Tufike mahala tuseme ukweli hata kama ni mchungu, IGP Simon Sirro alijua fika kuwa mkutano wake umehudhuriwa na waandishi wa Habari na kwamba chochote akisemacho kitaufikia umma.

Yako mengi ameyasema ambayo ni ya maana sana but kuna moja nadhani kateleza. Ni kweli dressing code ya Polisi Tanzania inapashwa kufuatwa, Hata hivyo; kitendo cha IGP Sirro kumshambulia Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, Afande Mambosasa, sio cha kiungwana.

Mavazi aliyomsema ndo na yeye amewahi kuyavaa na sio kwamba alikuwa porini au kwenye operation, aliyavaa kwenye “Press.” Swali je! Kajua umuhimu wa dress code leo, au ilikuwa ni nia ya kurudisha mashambulizi kwa Afande Mambosasa ambaye kimsingi ameonekana kufanya “vizuri” zaidi yake wakati akiwa Kamanda wa Kanda hiyo!

Nadhani kwa uungwana, ni vema na ni busara kwa Afande Sirro kumuomba msamaha Afande Mambosasa. Kama kweli anahuburi umoja ndani ya polisi, basi hakupaswa kutaja jina la Afande Mambosasa; angekemea kwa ujumla na ndo hapo nasema IGP Sirro kateleza.

Katika picha, ni vazi la kipolisi (jungle) ambalo ni maalum kwaajili ya oparesheni, na IGP Sirro kakemea kuwa halipaswi kuvaliwa wakati wa “press,” hata hivyo, katika uchunguzi wangu mdogo mitandaoni, umeonyesha kuwa yeye mwenyewe Afande Sirro, ni mvaaji mzuri wa vazi hilo nje ya oparesheni.View attachment 1216030View attachment 1216031View attachment 1216032View attachment 1216034View attachment 1216035
Ile clip ninayo hapa, nimetazama kwa umakini, Sirro anasema watu wanavaa Jango kila kona, kila muda utadhani muda wote wako operation, na kibaya zaidi wanavaa na staff shoes huu ni ushamba sana.

Sasa nenda kamwambie Mambo sasa aache ushamba wa kuvaa Jango na staff shoes.

Kama Sirro nae aliwahi kuvaa Jango na staff shoes leta picha hapa.

Kingine uwe na adabu huwezi kusema IGP amuombe samahani Mambo sasa, protocol ya jeshi gani hiyo? Au ukiwa na bando unaandika tu?
 
Back
Top Bottom