CHADEMA kumtafuta Mdude kwenye nyumba za Polisi

CHADEMA kumtafuta Mdude kwenye nyumba za Polisi

Elias Msuya

Platinum Member
Joined
Dec 23, 2011
Posts
264
Reaction score
1,010
Gp7AhG2XEAAdYuM-1024x892.jpg

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimesema kitamtafuta kada wake, Mdude Mpaluka Nyagali aliyetoweka tangu usiku wa kuamkia Mei 2, 2025 mkoani Mbeya.

Chadema pia wamempa Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Camillus Wambura saa 72 kuzungumza na Taifa kuhusu matukio ya utekaji na watu kupotea, huku pia wakitenga Sh10 milioni kwa mtu yoyote atakayetoa taarifa za anakoshikiliwa Mdude.

Mdude alichukuliwa na watu wanaodaiwa kuwa maofisa wa polisi waliovamia nyumbani kwake usiku na kumjeruhi na kisha kuondoka naye.

Soma pia: Mdude Nyagali adaiwa kukamatwa na kupigwa na watu waliojitambulisha Polisi

Kwa mujibu wa mke wake, Sije Mbugi (31), wavamizi hao, ambao alidai walikuwa maafisa wa polisi waliokuwa na silaha, walivunja mlango na kuanza kumshambulia Mdude, ambaye alikuwa amelala nyumbani kwao huko Mbeya. Picha zilionyesha madoa ya damu sakafuni, zikionyesha kuwa mwanaharakati huyo maarufu wa kisiasa alijeruhiwa.

Soma pia: Mke wa Mdude: Tusifiche na tusisingizie mtu, waliomchukua mume wangu ni Polisi! Wana roho mbaya sana

Hata hivyo, kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga alikanusha jeshi hilo kuhusika na tukio hilo.

Pia Jeshi hilo lilitoa taarifa kuwa linafuatilia taarifa za maofisa wa Polisi kuhusishwa na kupotea kwa Mdude.

Taarifa hiyo ya polisi ilikuja kufuatia madai ya kada wa Chadema aliyetajwa kwa jina la Ezekiel Sheyo aliyedai kukutana na maofisa wa polisi waliomtaka awaonyeshe nyumbani kwa Mdude siku moja kabla ya tukio la kutekwa.

Soma pia: Jeshi la polisi linachunguza tuhuma za kuhusika askari katika kupotea kwa Mdude Nyagali

Chadema walia na Polisi
Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya Chadema, Mikocheni Dar es Salaam, Naibu Katibu Mkuu (Bara), Amani Golugwa amesema licha ya chama hicho kutoa ushirikiano kwa polisi lakini hawaoni jeshi hilo likichukua hatua.

“Chadema hatujaridhishwa na namna Jeshi la Polis linavyoshghulikia jambo hili, wanatushangaza na wanatupa fadhaa. Tunapohoji kwa nini hawamtafuti Mdude wanawekeza nguvu nyingi kumpata shahidi wa kwanza Ezekiel Sheyo.

“Taarifa zote Ezekiel alizisema mbele ya vyombo vya habari, akaonyesha namba walizompigia. Lakini tunasikitika kwamba Jeshi la Polisi hawaonyeshi kabisa kuhangaika kuwatafuta hao watu, kuanzia kwenye namba ya simu kwamba huyu ndiye aliyempigia simu washughulike kuwapata hao, lakini hawaonekani kushufhulikia jambo hilo,” amedai.

Kutokana na hali hiyo, amewataka wanachama wote nchi nzima na raia wema wasiofurahishwa na mwenendo mzima, kusaidiana na Jeshi la Polisi, kutafuta nyumbani kwa askari wote waliotajwa kuhusika na utekaji huo, licha ya RCO kukana kuwafahamiu.

“Fikeni kwenye majumba zao, kwa utaratibu tu, nendeni kwa wazazi wao mkawaulizie na kwa ndugu zao kwa sabau wanajulikana na polisi wamewakana. Tunafikiri kuna uwezekano mkubwa, huenda kuna uwezekano mkubwa huenda wamemfucha Mdude nyumbani kwao,” amesema.

Amesema wamechukua hatua hiyo kwa kuwa Jeshi la Polisi halionyeshi dhamira ya kuwatafuta Mdude, licha ya taarifa walizopewa na juhudi zilizofanyika kumtafuta.

“Chadema tumetoa Sh10 milioni tumeziweka pembeni kwa mtu yoyote atakayetoa taarifa za uhakika kuhusui anaposhikiliwa Mdude Nyagali,” amesema.

Chadema pia imewaomba watumishi wa umma wakiwamo wahudumu wa afya hospitalini, magereza na mipakani kufanikisha taarifa za kupatikana kwa Mdude.

Amesema kutokana na taarifa za kupotea kwa Mdude, amedai kuna magenge ya uharamia yaliyomo ndani ya polisi, hivyo akamtaka Afande IGP Camillus Wambura kutoa kauli.

“IGP Taifa linahitaji kusikia kauli yako, kwa matukio yaliyotokea. Matendo yanayotokea halafu Polisi wanakana kwamba hawajui, hawa watu wanaoshika silaha wakijitambulisha kuwa ni polisi halafu Polisi wanakana, bila shaka kuna magenge ya uharamioa ndani ya polisi,” amedai.

Ameunganisha hatua ya makada wa Chadema kudaiwa kukamatwa na polisi waliokuwa wakihudhuria kesi ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu Aprili 24, 2025 na kisha kupigwa na kwenda kutupwa maeneo mbalimbali jijijini humo, akisema ni sehemu ya uharamia huo.

Hata hvyo, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro alikanusha polisi kuwakamata makada hao.

“Tunakusihi afande IGP ndani ya saa 72, tunakusihi sana uzungumze masuala haya kwamba kuna magenge ya uharamia. Wanapiga watu halafu wanaema hawajapoiga watu, sisi tunawaona recorded on camera, on uniform na wengine with ID.

“Usipozungumza tutakushangaa, kwani jambo gani kwako ni muhimu? Mambo yanayohusu maisha ya watu, usalama wa watu?” amehoji.

Amegusia kauli za viongozi wa CCM na Serikali akisema zimekuwa zikichochea matukio ya utekaji na ushambuliaji wa watu ikiwemo kauli ya Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais (Tamisemi,) Mohamed Mchengerwa aliyoitia Aprili 26 akiwa soko Matola jijini Mbeya akidai kuwa ilichangia matukio ya watu kupotea.

Katika kauli hiyo, Mchengerwa aliwataka wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama yaani wakuu wa mikoa na wilaya kuwadhibiti watu wanaochochea uvunjifu wa amani.

“Kila mtu amepewa mipaka katika maeneo yenu, yule ambaye atashindwa kushughulikia migogoro na chokochoko zinazoendelea katika wilaya yake huyo maana yake kazi imemshinda. Itakuwa ni wajibu wangu kumshauri mheshimiwa rais kumweka pembeni mara moja,” alisema Mchengerwa.

“Siku nne tu baada ya kauli hiyo, mpigania haki na kada wa chama chetu, Mdude Nyagali akaanza kuwindwa na mpaka tunapozungumza hivi leo hajulikani alipo,” amedai Golugwa.
 
Mdude ndio amekwenda hivyo!

Ben Saanane ilikuwa hivi hivi.,......!
Azory Gwanda ilikuwa hivi hivi........!
Soka naye ilikuwa hivi hivi...................!

Je, nani anayefuatia kwenye mfululizo huu?
 
Mwili wa Mdude utakuwa kwenye shallow grave Rukwa au Katavi tunachotaka ni mwili ili tumzike Mdude kwa heshima zote.
 
Kuna methali zililetwa ili zitupumbaze na kututia umasikini

Eti aliye juu mngoje chini?

Hii methali naichukia sana,

Sasa utamngoja mpaka lini ilihali umepigwa kimaisha?
 
Back
Top Bottom