Afande Sele kugombea ubunge 2015

Afande Sele kugombea ubunge 2015

Acha roho mbaya wewe, na kama ndio fikra zako zipo hivyo hautaendelea ng'o!!!!!!
 
BAghe na Mitungi kaacha? agombea kwa tiketi ya Kile chama Cha Dovutwa
 
Mh! Tanzania na mustakabali wa kizazi kijacho!!.... Majibu ya watoto wetu yatakuwa hivi: Mzazi,.... "wanangu bangi na sigara havifai, kwani vinaharibu mfumo wa ubongo na hudhoofisha mwili..." WATOTO: "...dingi acha mbwembe, mbona mlisema kina sugu, afande sele na wengine walivuta bangi ila sasa ni WAHESHIMIWA SANA BUNGENI!? Bangi haina noma wala nini, madingi mnatuzingua tu!!
 
Hii nchi sasa ishakuwa kichwa cha mwendawazimu, kila mtu akishapata umaarufu mitaa miwili anataka mpaka urais. Ndiyo matatizo ya uongozi mbovu, kila mtu anajiona anaweza kwa sababu the bar is set too low.

Tungekuwa na merit based system wengine wangeogopa wenyewe joto la kikaango. Lakini sasa hivi wanaona mpeto tu.
 
usirushe mawe wakati unakaa kwenye nyumba ya vioo. bangi kitu gani wewe mbona karibu nusu ya wabunge wa sasa ni wavuta bangi na watumiaji wa madawa ya kulevya?

Hapa ndipo tunafikia mahali wengine tunaoma Mungu aiangamize nchi hii kama alivyofanya kwa Sodoma na Gomora!!!Wewe na bangi zako upo tayari kuwa na mbunge Afande Sele?Mnadhalilisha watanzania!!!!yale yale ya kina Vicky Kamata na wakina Sugu!Pelekeni mambo yenu Ghetto au Leaders!!!
 
Ni kweli Afande Sele anafaa kuwa Mbunge.
afande_sele4.jpg


Sipati picha apeke hoja binafsi bungeni ya kutetea bangi ikataliwe alafu zimpande kichwani, bi ki.roboto lazima aingie chini ya meza....
 
Naamini sele anajutia kuliko kitu kingine staili yake hii ya kulipamba jukwaa, Itamgharimu maisha yake yote yaliyosalia. Namshauri aachane kabisaaaaa na siasa, itamuondoa na kwenye fani ya kughani. Kama anaangalia mafanikio ya sugu, akumbuke "si kila king'aacho ni dhahabu"

ktk hii dunia,kuna jambo unaweza kulifanya pasi kujuwa ama kwa kukusudia na likaja kukugharimu daima milele
hii ndio itakavyokuwa kwa afande sele kwani hili la kuvua nguo jukwaani hata kama atagombea ubunge ni kwamba picha hiyo ndio itakayo mharibia
 
bora kabisa kuliko magamba waendelee kupeta moro.atasaidia 2weze kuuza majani katika nchi zanazoruhusu majani.cyo kila kukicha manjagu wamechoma hekari 50 za majani mara.bora 2iuze huko nje
 
enzi za mwalimu watu waliotaka kuwa viongozi kabla wananchi hawajaamua yeye alishafanya uchunguzi na tathmini ya kutosha juu ya uwezo wa mtu huyo, heshima na dira yake binafsi alipogundua mtu huyo hawazi alimpotezea tu, na kumwambia asubiri muda ukifika. uongozi ulikuwa kitu muhimu na cha thamani wale walioa na nia ya dhati ndio waliojitokeza sasa hivi uongozi umekuwa business kama dini.
haya bwana tukisema tutaambia mbona schwaznegger anatawala. nafunga bakuli langu.
 
Ni kweli Afande Sele anafaa kuwa Mbunge.
afande_sele4.jpg

Hakika hii ni gharama kubwa ambayo hataweza kuilipa kisiasa. Hili ukichanganya na lile la kuwasaliti vinega dhidi ya mapambano ya Wafu FM litamtafuna. Ana kazi ngumu kujisafisha
 
Ni mimi Msanii x 2 Kioo cha Jamii!!!!! Halafu cheki hapo chini Mtarajiwa mbunge kwenye Kandambili!
combinenga4.JPG
 
Back
Top Bottom