Afande Sele kugombea ubunge 2015

TIQO

JF-Expert Member
Jan 8, 2011
13,787
2,078
afande-sele.jpg

MFALME wa Rhymes nchini Seleman Msindi 'Afande Sele' ameweka wazi mpango wake wa kugombea ubunge katika uchaguzi wa mwaka 2015.

Akizingumza hivi karibuni Sele alisema ameamua kugombea ili kuweza kuwatetea wanyonge ambao wamekosa watetezi bungeni.

Hata hivyo Msindi ambaye amekuwa akiimba nyimbo zenye 'mguso' kwa jamii zikiwemo 'Mtazamo' aliowashirikisha Solothang na Prof.J, Karata Dume na nyinginezo hakuweka wazi kuwa atasimama kwa tiketi ya chama gani.
 
Mh,Ni haki yake kama mtanzania.Atumie haki yake ya kuchagua na kuchaguliwa
 
Ni haki yake kikatiba kugombea popote pale anapo taka pasipo kuvunja sheria.
Aanze mapema kujipanga
Tunamtakia kila la kheri.
 
Safi sana Jembe Sele nilimsikiliza kweli alisema ana mpango na yeye kuchukua jimbo coz ana iman mwanasiasa yeyote atakayesimama nae lazima akae!
 
Sina shaka nae hata kidogo hasa nikizingatia haya madudu ya wabunge wa CCM Mfalme anaweza lakini akigombea kwa tiket ya CDM tu tatizo sio yeye kama akigombea kwa tiket ya magamba tatizo ni mfumo atalazimika kuufuata mfumo mbovu ulioko ccm
 
Ubunge wa jimbo la Bangi labda! Kuiga iga kila kitu kunawaponza..eti kisa Sugu ni Mbunge naye anataka Ubunge..wasanii bwana! Mara kanumba anataka ubunge, mara Langa anataka ubunge, Professa Jay naye nasikia katangaza nia, ooh sijui Jay Moe naye anagombea! hawa watu bwana!

usirushe mawe wakati unakaa kwenye nyumba ya vioo. bangi kitu gani wewe mbona karibu nusu ya wabunge wa sasa ni wavuta bangi na watumiaji wa madawa ya kulevya?
 
Wanaiga kwa vile waliopewa ridhaa wameshindwa kuwawakilisha ndo maana wameamua kuingia wenyewe front line huko huko mjengoni wakapambane
 
usirushe mawe wakati unakaa kwenye nyumba ya vioo. bangi kitu gani wewe mbona karibu nusu ya wabunge wa sasa ni wavuta bangi na watumiaji wa madawa ya kulevya?
Kwahiyo unaona kuwa ni sahih tukaongeza idadi ya wavuta kitu Bungeni?
 
Nashindwa kuacha kumfananisha Afande Sele na Zitto Kabwe. Wote wanataka mambo makubwa kuliko uwezo wao. Nchi hii uongozi umedhalilishwa kiasi hiki kwasababu ya viongozi tulionao.
 
ni kweli afande sele anafaa kuwa mbunge.
afande_sele4.jpg

ndiba mchezo gani tena huu
loh kumbe bora nisubiri 2015 kutangaza mapema kumuiga zitoo tunaishia na kashfa za ukweli kama hizi
sijui atamuuzia nani miskoto kule bungen sugu ashaachana nazo analinda afya sikuhizi...sijui anataka kumuuzia nani majani
 
Mkuu Basiasi nilikuwa najaribu kumnadi mgombea mtarajiwa pengine atakubalika.
 
Kawaida ya wabongo, mtu akiona biashara ya nyanya imemlipa mwenzie kila mtu anaagiza tenga la nyanya. Mwageni vijisenti vyenu subiri, naona hamjui siasa vizuri.
 
Back
Top Bottom