Afande Sele atashtakiwa kwa kosa gani baada ya kumtukana Mungu?

MWINY WETU

Member
Dec 14, 2015
16
16
Huenda bwana Selemani Msindi amefanya makosa lakini ni lipi kosa lake kisheria? Nani wakumshtaki? Nani aliefanyiwa kosa?

Tukianza na kosa lake kisheria, kifungu namba 129 cha kanuni ya adhabu sura ya 16 kinaeleza kuwa Nikosa kuumiza hisia za imani ya kidini ya mtu mwingine kwa kuweka maneno,Ishara au picha mbele ya mtu huyo ambayo itaumuumiza hisia zake za kidini.

Hivyo kukashifu dini ya watu wengine ni makosa. Kifungu hicho hakisemi kukashifu Mungu.

Labda tunaweza kusema kuwa dini zinaamini Mungu, hivyo ukikashifu Mungu umekashifu dini.

Swali la pili litakuwa ni nani amekosewa? Hata kama tutasema kukashifu Mungu ni kukashifu dini na nikuumiza hisia za kidini za watu au mtu fulani.

Swali litakuwa ni dini ipi? Kuna dini zaidi ya 360 Duniani na kwenye baadhi ya dini kama wahindu na dini za kimila kuna Mungu zaidi ya mmoja. Swali linakuja kuwa ni Mungu yupi wa dini ipi alietukanwa na Selemani?

Kumbuka kuwa Kuna watu husema kuwa wao Mungu wao ni hela, hawa wana Mungu ila hawana dini.

Kufikia hapo tunagundua kuwa Selemani hana kosa lolote kisheria.

Pia soma>
Ujumbe wa Afande Sele akimlilia Magufuli
 
Kwani alisemaje,kama kuna kizibiti tunaomba kiwekwe ili tufahamu dalili za mtu aliyvuta bangi zikoje pia tupate pa kuanzia kumsulubu Huyu mvuta bangi hodari
 
Kwani alisemaje,kama kuna kizibiti tunaomba kiwekwe ili tufahamu dalili za mtu aliyvuta bangi zikoje pia tupate pa kuanzia kumsulubu Huyu mvuta bangi hodari
Walaa c bangi n akili yake ya kufikiri ilifikaa mwisho,wañgap wanavuta bangi na hawajafanya huo ujinga aliofanya afande
 
Kwani alisemaje,kama kuna kizibiti tunaomba kiwekwe ili tufahamu dalili za mtu aliyvuta bangi zikoje pia tupate pa kuanzia kumsulubu Huyu mvuta bangi hodari
Amemtukana Mungu.Hivi kiumbe unawezaje kumtukana Muumba wako?.Nenda YouTube mcheki,Mimi sitaki hata kumsikia tena.
 
Swala hapa ni huyo Mungu kujitetea... huyu Mungu yy hana nguvu za kujitetea hadi wanadam ndio wamtetee!!! Kimsungi hoja ya Afande inamashiko sema aliwasilisha katika lugha ya matusi
 
Swala hapa ni huyo Mungu kujitetea... huyu Mungu yy hana nguvu za kujitetea hadi wanadam ndio wamtetee!!! Kimsungi hoja ya Afande inamashiko sema aliwasilisha katika lugha ya matusi
Ni Ajabu kubwa kuona Mungu anaongozwa na binadamu badala ya Mungu Kuongoza Binadamu! Nadhani Kwa Hili la Afande sele, Mungu mwenyewe alitakiwa Kumjibu Afande sele. Ila jambo la kushangaza Wanadamu wanaanza kumuongoza Mungu kwa Kumuomba Amjibu Afande sele! Kwani Mungu Hana Macho ya kuona afande sele alilofanya ajibu mwenyewe? Au Mungu Hana masikio ya kumsikia Afande sele.
 
Back
Top Bottom