Msanii mkongwe wa muziki wa 'HipHop' nchini Selemani Msindi @afandesele1976 amesema hivi karibuni amekutana na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Jaji Francis Mutungi ambapo miongoni mwa mambo aliyomweleza ni mashaka yake ya uwepo wa namba ndogo ya wananchi inayoweza kujitokeza kupiga kura kutokana na uwepo wa masuala mbalimbali yanayoashiria kukosekana kwa uwazi na usawa miongoni mwa wadau wa siasa
@afandesele1976 ambaye pia ni kada wa Chama cha Mapinduzi @ccmtanzania amesema mtazamo wake unaamini kuwa hata oparesheni 'No Reforms, No Election' inayoendeshwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo @chadematzofficial imepewa nguvu na kuongeza uelewa zaidi kwa jamii baada ya kukamatwa na baadaye kufunguliwa kesi kwa Mwenyekiti wa chama hicho Taifa Tundu Lissu jambo ambalo yeye anaona lingeweza kudhibitiwa kama Lissu asingekamatwa
"Kwa sababu naamini kwamba Msajili ni mtu mkubwa, lakini pia nikamwambia kwamba hata wale watu wa chini kabisa hawakuwa na mpango kabisa na Lissu wala CHADEMA, lakini baada ya tukio hilo nikamwambia hali ya mwamko wa wananchi kujitokeza kwenda kujiandikisha nchini hamasa yake imeshuka"