Advocate Joe Mbuna afariki dunia

My hear is with his remaining family.
May God shelter them with peace at this very hard time.
 
Ni mkwe au vijana wao ndio wameoana? Poleni wafiwa wote.

Naona hakuna aliyena jibu kwa swali lako. Ila ulivyosema ndo sahihi. Mtoto wa Mkapa kaoa wa huyo Mbuna hivyo basi Mbuna hawezi kuwa mkwe wa Mkapa labda kama tunaongea lugha nyingine na si Kiswahili.
 
KIFO NI KUTUKUMBUSHA TU NA NI MFANO KWA WALIO HAI KWAMBA MAISHA YA HAPA DUNIANI NI MAFUPI TU, UMRI ALIOISHI MFALME SELEMAN SI MREFU KAMA MUDA ALIOKUFA KWA HIYO HUKO TUENDAKO NDIO KUREFU ZAIDI, HIVYO TUACHE UFISADI NA KUJILIMBIKIZIA MALI AMBAZO HATUTAZITUMIA KWA MUDA MREFU,

RIP Adv Mbuna
 
Huyu ndio the man behind KCPL (Kiwira Coal Power Limited)

Habari ndio hiyo.

Nafikiri mambo mengine ni ya Mungu,wengine wataona labda mola anawalipia wanyonge.Hayo ndo yaliyowapata kina Ditto.
Sasa ndugu yangu Mbuna ndo kaondoka labda na wengine ambao ni greedy wangejifunza kuwa tulikuja duniani uchi na tutarudi uchi(watupu).
Poleni wafiwa.
 
RIP Ndugu yangu Joe. Mwili wa marehemu unaletwa leo kwa Emirates toka Hyderabad India.Nyepesi nyepesi zinasema kabla hajafariki ali sign off kurudisha Kiwira serikalini,kuna mdau anayeweza kutudhibitishia jambo hili?
 
kwa kuwa alishahukumiwa sawa sawa na matendo yake basi wengine tufunge midoma au kuifungua kwa kuimba kuwa : BWANA UTUFUNDISHE KUZIHESABU SIKU ZETU AU BWANA HUKUMU ZAKO WEWE NI ZA ADILI
 
kwa kuwa alishahukumiwa sawa sawa na matendo yake basi wengine tufunge midoma au kuifungua kwa kuimba kuwa : BWANA UTUFUNDISHE KUZIHESABU SIKU ZETU AU BWANA HUKUMU ZAKO WEWE NI ZA ADILI

Mwakimbi,
Umesema jambo la maana sana. Watu hawajui kuwa mtu anapokufa tu anahukumiwa sawasawa na matendo yake aliyotenda wakati wa uhai wake.

Hili suala la kuwaombea marehemu kwamba MUNGU awapumzishe kwa amani hata kama walikuwa wenye dhambi ndo limetufanya tuwe na watu wa ajabu ajabu wakiwemo hawa mafisadi tunaowapigia makelele kila kukicha. Watu wenye kujikinai wasiojali wengine. Wenye mapesa ya wizi kiasi cha kutisha huku wenzao wakilala wakiamka hawajui watakula nini. Maana wana mawazo kuwa wakifa wataombewa walale pema peponi. Kama viongozi wetu wa dini wangeacha unafiki na kuwaambia hadharani watu ukweli huenda ingesaidia watu kumwogopa MUNGU.

Sisi tulio hai yatupasa tutengeneze njia zetu na MUNGU kwani hatujui siku wala saa ya kuondoka kwetu hapa duniani.

Nawapa pole wafiwa MUNGU awatie nguvu.

MUNGU atusaidie tuijue kweli.
 
Last edited:
Back
Top Bottom