ADVICE: Ninunue gari aina gani?

napingana na mawazo yako ya kusema 7m haitoshi kwa mtaji!!..mm nilianzisha mpesa,tigo pesa,airtel money just for the capital of 5m na sasa imezaa imekua 10 within a year!!,kibusness changu kinanizalishia kati ya laki8 mpaka 1m kwa mwez kwa capital hiyo ya 5m nloanza nayo!!jaman ujasiriamali hauhitaji mtaji mkubwa ni akili tu,hata 1m ni mtaji wa kutosha na ukiimanage vzr baada ya mwaka inakua 5m hiyo!

Na ndio maana huwa tunashindwa kufanya biashara kwa kuwa wengi wetu ukituambia biashara tunafikiria mtaji mkubwa sana ambao ni zaidi ya 10 milioni tunasahau kwamba biashara ni zaidi ya mtaji kwani kuna issue ya ujuzi na uzoefu before investment hivyo unahitaji kuanza kwanza na kile ulichonacho karibu ili unafikiria namna ya kutanua biashara yako in future wakati huo tayari unakuwa na ujuzi na uzoefu. Nakubaliana na Kamanda Moshi kwenye kipengele kingine cha usimamizi
 
na starehe zitawaua, yaani ni sawa na mtu hana hata vyumba viwili lakini anawaza gorifa kwa nini mtu usife kwa depression,kisukari,presha vidonda vya tumbo na mengineyo

Sometime maisha ni magumu kweli ila kuna mazingira maisha sio magumu ila tunayafanya yawe magumu kwa kuishi maisha ya kujifananisha na wengine na mwisho wa siku tunafanya maamuzi ya kuridhisha nafsi za watu wengine ili na sie tuonekane tumo mjini, tunasahau kwamba kumbe kila mtu ana stahili yake ya maisha mjini na namna ya kuingiza kipato maana kuna mwingine anaweza akawa ana trip kibao za nje ya ofisi na posho za safari na anajibana kwa hizo hizo posho na ndio zinakuwa zakunywea na ku-socialize (wenzangu na mie tunashindana na hao huku tukijisahau tunatumia salary zetu tu)
 
Njoo nikuuzie corona premio, gari ngumu, mafuta kiduchu, spear cheap, fundi yoyote anatengeneza siyo hadi mafundi wa kuelekezwa.
 
kaka avator yako inasadifu akili yako sasa kama ni 2010, hata nikikwambia nilisoma cheti mwaka mmoja utabisha wapi, pili unakurupuka nishakwambia,ebu soma kwa umakini pachiko langu la kwanza, hivi nimeandika nilikuwa nilikuwa k.6 au?

kwa mara nyingine jipange.



jibu maswali
1.Chuo umeanza lini mwaka na mwezi?
2.chuo umemaliza lini mwaka na mwezi?
3.Umesoma kozi gani?

Kumbuka hzo i10 zilitolewa mwaka 2010 wkt wewe upo kidato cha 6,Je hicho chuo umesoma miaka miwili? Au umeanza kazi kabla ujamaliza chuo?
 
Kwahiyo bado ukiongeza na ile 35,000/= ulioainisha kule mwanzo inakuwa jumla 67,000/= ambayo ni appromately na 70,000/= aliyofanyia ram, all in all gharama za service huwa zina range between 50,000/= mpaka 70,000/= hata 80,000/= but kihakikisha kwamba zikifika 3000km unakwenda kufanya service maana vitu vingine huwa wana vicheck tu kama vipo poa hawavibadilishi, na ndio maana unaweza ukafanya service mwezi huu 70,000 zikiisha hizo kilometre ukija mara ya pili inashuka kwa kuwa kuna baadhi ya vitu vinakuwa checked.

kama fuel filter na air filter hazibadilishwi kila service.....kitu ambacho kinabadilishwa kila service ni oil filter na engine oil....ila jitahidi kwa mwaka ufanye major service hata mara moja ambayo unaservice hadi brake system,drain radiator,ATF
 
mkuu upo sahihi kabisa,tatizo vijana sikuiz tunapenda sn starehe ilhali uwezo hautoshi!!hiyo 7m kama ataiinvest kwenye biashara namuhakikishia baada ya 1 or2 yrs ananunua hata rav4 sio tu vits,huku mtaji wake ukiwa unaendelea kuproduce profits!!,ok ila kwakua ni bint huenda ameolewa na anahudumiwa kila kitu hadi mafuta na services hua wanasaidiwa hao bana na mashemeji zetu,namshauri anunue vitz!!

Tatizo watu mnaogopa kuchagua,kila mtu anataka awe mjasiriamali kwa kufanya biashara iliyo stationed sehemu,what if huyo anaenunua gari anataka limsaidie kwa misele yake ya kutafuta kipato? Still mna mentality kuwa gari ni starehe na sio means ya usafiri tu? Mwachen dada anunue gari hivyo vingine vitapangika afta kulinunua,likimshinda si ataliuza na kurudisha pesa yake!! Msiwe na mawazo mgando kuwa gari ni starehe, watu wanayatumia magari hayohayo kupatia deals mjini.
 
Walioshindwa wana maneno mengiiii Kutwa nzima kujadili ya wenzao.... lakini yao yamewashinda
akuu shost nitakuwa mtu wa mwisho kukujadili duniani humu... hayanihusu hata....ila ujumbe umeupata....laki tatu na gari wapi na wapi? hata ufanye calculation na calculator ya mbinguni jibu litakuwa negative tu
 
Nunua mkoko mzee,fuata mawazo ya wazoefu wa mgar achana na waoga wa matumiz.tafuta gar simple inayo kufaa kwa kaz yako itakusaidia.kufanya kaz kwa ufasaha.mark II nipoa sana
 
Mkuu nunua hii cc80 tu na inakufaa sana hapo bongo.
01s.jpg
 
Nina
kiasi cha shilingi 7mil na ninataka kununua usafiri wangu binafsi.
Naombeni wenye uzoefu na magari mnishauri ni aina gani ya gari naweza
kuipata kutoka show room kwa kiasi hicho cha fedha.

Binafsi nilikuwa napendelea toyota mark II ila sasa sijui bei yake
ikoje.

Then naomba kujua gharama za utunzaji gari zikoje kwa mfano inatakiwa
ifanyiwe service mara ngapi kwa mwezi.

Mshara wangu ni lak 3 kwa mwezi sina familia je nitaweza kuzimudu gharama za utunzaji gari?

Mpendwa kwa bajeti ndogo au ya ukubwa huo, nunua gari kwenye mtandao, browse Be Forward na utapata gari zuri, la bei nzuri na kwa uhakika zaidi. Kama unataka gari rahisi kutunza ulizia Toyota family lakini magari madogo, ila hata Suzuki Swift nayo ni economic. with 2.3 USD CIF dari liko Dar es Salaam Port. Usihofu
 
Mi nadhani ungefungua buzness ya 5M, baada ya mwaka tunakusahau! ni dalili ya umaskini kuwaza kuongeza matumizi badala ya kuongeza kipato

Aisee ni biashara gani ya 5m hadi kwa mwaka tumsahau? Funguka ndugu.
 
mtu anaomba ushauri juu ya ununuzi wa gari mtu anaanza kuhoji amepata wapi m7 au atalihudumia vp gari lake? mtu unaleta matatizo yako kwa mwingine.Mtoa mada hajaomba msaada WA kulitunza..kama amepata m7 ya kununua gari hatakosa hela ya kulihudumia..nunua miss mengine yatajulikana mbeleni...kama upo kwako
huna majukumu laki 3 inatosha kabisa...salary is just the figures..
 
akuu shost nitakuwa mtu wa
mwisho kukujadili duniani humu... hayanihusu hata....ila ujumbe
umeupata....laki tatu na gari wapi na wapi? hata ufanye calculation na
calculator ya mbinguni jibu litakuwa negative tu

sawa Smile you win I loose
 
Last edited by a moderator:
Tatizo watu mnaogopa kuchagua,kila mtu anataka awe mjasiriamali kwa kufanya biashara iliyo stationed sehemu,what if huyo anaenunua gari anataka limsaidie kwa misele yake ya kutafuta kipato? Still mna mentality kuwa gari ni starehe na sio means ya usafiri tu? Mwachen dada anunue gari hivyo vingine vitapangika afta kulinunua,likimshinda si ataliuza na kurudisha pesa yake!! Msiwe na mawazo mgando kuwa gari ni starehe, watu wanayatumia magari hayohayo kupatia deals mjini.

km umesoma vzr coment yangu,mwisho nlimshauri anunue Vitz na wala siikumkataza km unavyodai ww!nimkataze kwan pesa nlimpa mm?
 
Duu kweli vijana kazi tunayo vijana una mshahara wa laki 3 unataka kununua gari? Jijenge kwanza dogo kununua gari la matumizi binafsi ni kujipunguzia speed ya kukua kiuchumi.Zungusha hizo mil 7 zako ili kuja kununua gari ukiwa una raha zako zote na uwezo wa kununua fuel



hahahhaha hiyo pesa yenyewe ya gari, alimdanganya baba yake hapati boom chuo, so pesa ya mkopo yote katunza ndo anataka kununua gari, huyu kama hatalazimika kupata pedeshee mjini la kununua mafuta sijui kwa kweli, achana na magari dear pesa yako ndogo sana ya kulimantain litakutia majaribuni tu
 
hahahaha

hii sredi nimejifunza mengi sana

Cha msingi mdada keshakata shauri anataka kununua gari kwa 7M na sio kitu kingine. Amesema mshahara wake laki tatu sawa kwa mwezi, inawezekana ana vyanzo vingine vya mapato pia ambavyo vitasubsidise matumizi mengine ikiwemo mafuta.

Ni kweli kwamba gari inatumia mafuta lakini sidhani kwamba ni lazima atumie mafuta 10,000 kila siku kwa siku 30 maana sidhani kama siku zote hizo anaenda kazini including jumamosi na jumapili

Zaidi, ni kwamba huenda hata gharama za kutokuwa na gari kwa mwezi zikawa karibu sawa na za kuwa na gari....
Mfano, pale ubungo agombee zile za 1000-1500 hapo unazungumzia elf 60-90 kwa mwezi kwenda na kurudi. tufanye inabidi apande boda boda hadi anapokaa, 2000 kwenda na kurudi ni wastani wa 120,000 kwa mwezi, hapo hajachukua tax labda ameenda kwen send off au harusi au kitcheni party tufanye wastani wa 50,000 kwa mwezi, unakuta ni almost 250,000 kwa mwezi....sasa hapo anakuwa amesave nini...hatujazungumzia usumbufu, kubanana, jasho, joto, maji ya madimbwi, nk.

Halafu hivi mtu kwa milioni 7 unafanya biashara gani hasa espeially kama huna ujuzi wa biashara.......

Mdada gor for what ypu need now then itakupa changamoto ya kupata mengine pia au tuseme kukurahisishia shughuli zako
 
Back
Top Bottom