Nakataa kuwa adui wetu namba moja ni umasikini,
Tatizo letu kubwa ni mfumo kandamizi usiotumia busara katika kutatua kero za mwananchi wa kawaida. Umasikini ni matokeo na katika mbinu za kutatua matatizo (problem solving techniques) yatupasa kwenda kwenya CHANZO, umasikini tulionao siyo chanzo bali ni MATOKEO, ambayo yamesababishwa na mfumo mfu wa wale ambao tunaendelea kuwapigia kura na kuwaweka madarakani kwasababu ya kutokujua kwetu (Ujinga).
Watu, siasa safi, ardhi, uongozi bora ambayo Mwalimu Nyerere alihimiza (Among others) ni mambo ambayo tunapaswa kuyaangalia kwa undani zaidi.
1. Watanzania kwa maana ya Watu, wapo na nzuri zaidi ni wakimya (wapenda amani walio wengi)
2. Siasa Safi, hapa ndipo penye shida. Hatuna siasa safi hapa nchini kwa maana ya malengo mahususi ya kumkomboa Mtanzania. Wale tuliowaweka madarakani wamekiuka miiko ya uadilifu na kuanza kutenda kunyume cha viapo vyao. Unapomuona Mbunge badala ya kukosoa yale mabaya yaliyo ndani ya serikali yeye anasimama na kujadili mapendekezo ya upinzani kwa maana ya kupotosha huwezi kusema tuna siasa safi. Unapoona Katiba ya Tanzania inasema "Tanzania ni Nchi Moja ya Ujamaa na kujitegemea (Katiba ya sasa, sura ya 1:3a), Kimsingi, Uchumi wa kijamaa ni ule wa NATIONALIZATION OF NATURAL RESOURCES, leo hii tumehamia kwenye PRIVATIZATION (Ambao ni mojawapo ya features za Capitalism, utasema siasa yetu ni safi. Kujiteemea wakati kila mwaka Mkopo wa Serikali unaongezeka bila vivid na evident initiatives za kulitatua hili?
3. Ardhi: Hili kila mtu analijua kuwa tunalo INGAWA kwasababu ya mfumo MFU tumeamua kuabudu miungu WAWEKEZAJI na kumfanya Mtanzania wa kawaida kuwa mkimbizi ndani ya nchi yake.
4. Uongozi bora; Hapa ndipo tulipojikwaa, HATUNA uongozi bora kabisa, uongozi usiofikiri hata kidogo, wenye muono finyu (Shortsightedness).
Ahadi ni Trillion 96 wakati budget ya serikali ni Trillion 15 kwa maana kuwa kwa kipindi chote cha miaka mitano, serikali ikiamua kutekeleza ahadi za chama kilichoiunda bila shaka itakuwa ni Trillion 75, bila kufanya jambo jingine?
Narudia tena, tatizo la nchi yetu tutake tusitake SIYO umasikini bali mfumo mfu uliotengenezwa na serikali inayokufa. Wapenda madaraka kwa njia yoyote ile wala siyo MASIKINI katika UMASIKINI wao bali MATAJIRI katika UBINAFSI wao.
Siungi mkono hoja