Jaji Mfawidhi
JF-Expert Member
- Feb 20, 2016
- 14,173
- 20,645
Tanganyika tuna msemo ulioanzishwa na wanawake wana -harakati katikati ya miaka ya 90' hasa 1995 baada ya Zakia Meghji na kundi lake kutoka mkutano wa Beijing wa kutaka usawa na wanaume.
Wanawake waliohudhuria walirudi Tanganyika na mtazamo mpya, wakitaka kila kitu sawa na wanaume ama kuwazidi wanaume , tukumbuke pia ndio habari za lady pepeta zilipoanza.
Kama haitoshi ndio walianza kushajihisha sheria za kazi zibadilishwe na kuwa nusu kwa nusu na pia kutaka viti maalum Bungeni, by then alikuwa mbunge wa Moshi mjini -Mama Clementina au mama kamm-akiwa mkuu wa shule ya Weruweru ambaye pia alikuwa mbunge wa East Arica.
Kauli ya Ummy kusema Adui wa Mwanamke ni mwanamke inafikirisha sana wanaume, wanaume hao wanaodai usawa tena kwenye imani zao za dini hawaruhusiwi hata kukaa meza moja na wanaume, hawaruhusiwi kutoa mhadhara wala kuhubiri madhabahuni, hawaruhusiwi kuoga kwenye public beach, hawaruhusiwi karibu kila jambo afanyaalo mwanaume , ni utumwa full ila sasa hao hao wanapigania mambo wanayonyimwa na waume zao na dini zao yawe implimented kwenye dini zingine.
Tuna Rais Mwanamke Samia Suluhu Hassan, Tuna Spika wa Bunge Mwanamke Tulia Akson,, Tuna waziri wa afya mwanamke Ummy Mwalimu, ila ndio wakati Toto Afya imefutwa na wanawake kufia hospitali kwa kukosa 150,000 ya kupata huduma za kujifungua.
Tunajiuliza kama kwa kipindi hiki miimili imeshikiliwa na mwanamke lakini badala ya kumteua Jaji Mugasha kuwa CJ wakamuongezea Ibrahi Juma, Badala ya kumteua Advela Chesco kuwa IGP wakamwachia aliyepo japo ameboronga kwa mengi, wameshingwa sehemu nyingi kuwapa wanawake sasa sijui kama 2025 Rais mtarajiwa Makonda ataweza rudisha wanawake kwenye nafasi zao.
Ummy amevumilia imebidi aseme tu ukweli toka kifuani mwake!