Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 92,231
- 113,594
Naomba nizungumzie kiujumla, licha ya kwamba kati yetu binafsi, wapo ambao wako tofauti na walio wengi.
Watanzania wengi ni wajinga [wasiozijua haki zao] na ni waoga sana.
Mchanganyiko wa hizo sifa mbili ni kikwazo kikubwa sana katika maendeleo ya jamii.
Huwezi kupata maendeleo yoyote yale ya maana endapo idadi kubwa ya watu kwenye hiyo jamii wana hizo sifa za ujinga na uoga.
Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu, pale mtu asiye na mamlaka ya kukupora haki zako anapokupora, na wewe humpingi huyo mporaji kwa nguvu na uwezo wako wote, ni kitu gani kingine utakachoweza kukipigania kwa hali na mali?
Watanzania tumeshuhudia kuporwa baadhi ya haki zetu kwa miaka ya hivi karibuni kuanzia takriban 2016 mpaka hivi sasa. Na tumekuwa wapole na wanyonge mno.
Alianza Rais Magufuli kukiuka katiba na kuvikataza vyama vya upinzani kufanya shughuli zao za kisiasa, kikubwa kikiwa ni mikutano ya kisiasa.
Magufuli kaondoka, kaja Rais Samia naye akaendeleza huo uvunjaji wa katiba.
Wote hawa wawili wamevunja katiba waziwazi kabisa. Na sisi wananchi wenye nchi hakuna lolote la maana tulilolifanya kuwapinga hao wawili!
Tunaburuzwa buruzwa tu. Juzi hapa Samia eti katoa ruhusa ya vyama vya siasa kuanza kufanya mikutano ya kisiasa!
Hiyo ruhusa kaitoa kwa msingi gani wa mamlaka aliyonayo kisheria na kikatiba?
Sisi ni banana republic. Hatuongozwi na sheria wala katiba. Tunaongozwa na hisia, hisani, na matakwa ya mtu ambaye kimsingi ni mtumishi wetu, lakini kiuhalisia ni kama vile sisi ndo tunamtumikia yeye na si vinginevyo.
Kuna wakati kule Marekani, kipindi ambacho Donald Trump alikuwa Rais, kulikuwa na mjadala kuwa endapo angetoa agizo kwa jeshi la nchi hiyo, agizo lililo haramu kisheria na kikatiba, viongozi wa jeshi walikuwa wako tayari kabisa kulikaidi hilo agizo. Hawakuwa tayari kutekeleza agizo lolote linaloenda kinyume na sheria na katiba yao.
Hao ni watu wanaojitambua. Ni watu wasio waoga. Ni werevu na ni majasiri pia.
Hapa kwetu jambo kama hilo bado sijaona kama linawezekana.
Magufuli na Samia walipaswa kupingwa vikali sana.
Maagizo yao haramu ya kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani yalipaswa kukaidiwa na watekelezaji wa sheria.
Mtu kama kweli unajitambua, si mjinga wala muoga, kwa nini utekeleze amri ambayo si halali?
Kwani ukikataa kutekeleza amri ambayo si halali, nini kitakutokea?
Ije katiba mpya au isije, hii tuliyonayo sasa hivi inayotupatia haki tulizonazo sasa hivi, inakiukwa waziwazi kabisa na hatufanyi chochote kulinda hizo haki zetu, hiyo mpya tunayoitaka tutailinda kweli?
Kwa sasa nimeshahitimisha kuwa tatizo letu kubwa wala siyo katiba mpya. Tatizo ni sisi wenyewe. Bado tupo wajinga sana, wapole sana, na waoga sana.
Kwa hizi sifa, hata ije katiba mpya, hakutokuwa na tofauti yoyote ile. Tutaendelea kuburuzwa tu hadi pale tutapobadilika.
Na kwa kizazi hiki kilichopo, sitegemei tubadilike.
Adui wetu mkubwa ni sisi wenyewe!
Rais Samia hastahili pongezi yoyote ile kwa ‘kuruhusu’ vyama vya siasa kufanya mikutano ya kisiasa.
Hakuwa na haki ya kukataza hiyo mikutano. Hivyo hana haki ya kuruhusu mikutano hiyo.
Hastahili kabisa pongezi.
Anachopaswa kufanya ni kuomba radhi. Aombe radhi kwa kukiuka katiba.
Akiomba radhi kwa hilo, mimi nitakuwa wa kwanza kumpongeza kwa kuona kosa lake na kuamua kujirudi.
Nje ya hapo, siwezi kumpongeza mporaji aliyeamua kunirudishia kilicho changu.