Adhabu za wanajeshi

Kabisa kabisa kaka. Ila si rahisi kuacha kazi ya jeshi, unatuchora tu wewe ili tujue you are now not a soldier
Mkuu nina watu tunafahamiana humu hawapungui 20 nikiongea uongo najiharibia...niamini huwa sina sababu ya kudanganya..
 
Ujinga huo haupo tena mkuu.
 
😂😂😂
 
Dah,Kumbe mkuu wewe ni bakabaka?

Nina kisa changu pia..

Siku moja nimetoka zangu home (enzi hizo Dar)mida ya saa moja usiku naelekea ubungo kutuma mzigo fuani nyeti uende Mkoa fulani kwa jamaa yangu mmoja enzi zile stendi Ni ubungo. Nafika pale nikawa sielewi elewi maana wapiga debe wananisumbua alafu limebaki gari moja tu linatoka nje..Lilikuwa BM,nikasema wacha nisepe nalo tu badala ya kutuma Kama parcel.

Tumefika Moro mida Kama ya saa tano usiku,nikamcheki bodaboda nikamuuliza Sasa hivi hadi kbi fulani ya jeshi Ni Bei gani? Boda akastuka,kwanza akaniangalia anaona mtu mwenyewe bwana mdogo early 20s. Akaniuliza uliza maswali nikamwambia mzee,maswali ya nini kama polisi niambie Kama unaenda au huendi. Nikampa hela, kinyonge akawasha chombo tukasepa.

Tumefika getini tumewakuta bakabaka pale wameshika mijegeja wanatukazia macho,hiyo Kama saa sita usiku Sasa. Kosa la boda boda si akapiga honi!! Bwana wee!!

Afande mmoja "Asee nyie raia mnajiamini nini kuingia maeneo haya mida hii,na mbaya zaidi mnatupigia Hadi honi?"

kilichonisaidia ni jina. Nilipotaja jina la mtu fulani kidogo wakapunguza kutuwashia Moto ila ilikuwa balaa,walishatuweka kwenye kanyampasila.

Hata hivyo bodaboda hawakumwacha bure bure kwa kitendo Cha kupiga honi kambini,tena saa sita usiku.

Jamaa watu wema ila ukijichanganya Sasa.
 
Labda akuue, lakini kama hujafa, na ukakomaa na hiyo ishu ya uonevu na kuhakikisha unaifikisha mbele ya vyombo vya nidhamu za kijeshi Askari aliyekuwa Lindo siku hiyo msala anao. Labda kama jeshi limegeuka kikundi cha Kihuni, lakini kama kweli ni jeshi lenye nidhamu, huyo afande au hao maafande msala wanao, tena si mdogo!
 
Ukiwatii ndo umeumia kwa sababu utafanya adhabu ambazo siyo haki kwa mujibu wa sheria. Usiwatii kabisa ili option yao iwe ni wakupige wakuumize au wakuue, halafu waje waone kama Jeshi litawakingia kifua. Itakula kwao!.

Baadhi ya Wanajeshi hasa vijana wanaendeshwa na Mob psychology. Hizi tabia za kihuni huwezi kuzikuta kwa wanajeshi ambao ni matured!.
 
Na tuliotoa adhabu tunaruhusiwa kusimulia?
Mungu anisamehe tu
Kumbe wewe ni soldier mkuu??? Uwiiiii jambo afande
 
Hawakupi adhabu km huna kosa, uwe unaelewa
 
Mtu yeyote anayekuonea na kukufedhehesha kwa makusudi, huyo naamini unatakiwa kufa naye kabisa, hatakiwi kusamehewa pasipo kuadhibiwa.
Ndio maana wanajeshi hawapendi kuzinguliwa kwenye himaya yao eneo la Jeshi, we mtambie kote Ila usiende kumtambia kwenye himaya yake hatoangalia wewe ni raia au wewe ni nani utachangamshwa kidogo ili siku nyingine ujifunze na uwe mfano kwa wengine
 
Askari wa Tanzania wengi - ingawa sio wote- hawana adabu, wanapenda kutumia uaskari wao kuonea watu.

Hizi habari zinanikumbusha mbali sana.

Kuna siku tulikuwa tumekaa maskani Upanga, muda wa jioni vijana wanakutana maskani. Mara paap, tukawa tumeaona askari kibao wanakuja kutoka mbali, wako doria kundi zaidi ya ishirini, wamebeba bunduki na marungu.

Basi nikawaambia madogo tuliokuwa tumekaa nao maskani, kama hamjiamini, ondokeni kabisa, wale wanakuja kutaka kututingisha hapa.

Basi kuna madogo wakaondoka, wengine tuliojiamini tukabaki.

Wakaja wakafika maskani, sisi kama kumi, wao zaidi ya ishirini. Mmoja akatuuliza "Haroo, mnafanya nini hapa?".

Basi hawakujua wanaongea na watu wa aina gani, jamaa mmoja wa maskani akamjibu "Afande hivyo ndivyo ulivyofundishwa kusalimia watu?". Ikabidi yule askari astuke kwanza. Alitegemea watu wataogopa, hakutegemea kujibiwa vile.

Sasa akaja askari mmoja, nafikiri ndiye alikuwa mkubwa wao yule, akaanza kuuliza watu, mmoja mmoja, "Wewe unakaa wapi?" Mtu anamwambia hapo, "Wewe unakaa wapi?" Mtu anamwambia hapo. Wakamfikia jamaa mmoja.Wakamuuliza "Wewe unakaa wapi?" Akajibu kwa Baba Ben.

Askari akauliza, "Kwa Baba Ben? Baba Ben gani?" Jamaa akajibu "Kwa Ben huyo huyo wa Jamhuri ya Muungano, kwani wewe unamjua Ben gani mwingine Tanzania?" (Hapo kipindi cha urais wa Ben Mkapa).

Yule Polisi akawa kastuka, kama hajaamini hivi, sasa kumbe kuna wenzake huwa walikuwa wanaenda kulinda kwa Mkapa, wakawa wamemjua yule kijana wa kwa Mkapa. Ikawa kama wanamwambia yule mkubwa wao kwamba huyu tunamjua anakaa kwa Mkapa, tunamuona tukienda kulinda pale.

Basi hapo hapo nikaona wale polisi wanabadilika mara moja, wanasema unajua wazee ni suala la kufahamiana tu, tulikuwa tunajuana tu, hamna tatizo, hamna tatizo tulikuwa tunatambuana tu.

Kuanzia siku hiyo mpaka kituoni kwao kile kijiwe walikiwekea alama ya X kisiguswe, wakasema hapa kuna watoto wa Mkapa huwa wanakaa.

Nikasema hapa ingekuwa wamewakuta watu wasio na majina wangewasumbua sana.
 
Mambo ya Seminari hayo, ukisema uliepigwa na aliekupiga wote mnafukuzwa Seminari, kwa hio mnayamaliza chini kwa chini tofauti zenu mnaziweka sawa chini kwa chini hakuna kusemeleana hapo father asijue km ulipigwa na fulani
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…