George Jinasa
JF-Expert Member
- Sep 14, 2010
- 399
- 52
Mkuu kwanza kabisa kifo ni kwamba kila mtu atakufa siku moja hakuna atakakimbia hii destination..; Pili kazi ngumu na mateso yanaweza yakawa makali kwa mtu hadi akatamani afe...; kuliko kuendelea kuishi (au hii haiwezekani) kwahio sisemi hawa watu wapewe kazi tu, bali kazi ngumu na faida ya hizo kazi kama ipo irejeshwe kwenye jamii husika.
Sisemi kabisa an eye for an eye..., sababu ukirejea maneno ya Gandhi anakwambia will make the all World go Blind..
Kuhusu dini kukubaliana na kwamba ukiua na wewe wakunyonge sidhani kama ni kweli labda sijarejea maandiko vizuri, nadhani maandiko mengi yanasema kusamehe au labda nikumbushe ni wapi maandiko yanasema mtu akiua na yeye anyongwe..
Uhakika ninao kwamba vitabu vya dini zote vinasema hivyo japo siwezi kunukuu vifungu. Naamini wapo miongoni mwetu wenye ufahamu mkubwa wa mambo ya dini watatujulisha. Ni kweli kifo hakiepukiki kila mmoja kimamsubiri. Hoja ni kuna hata mmoja anaependa kufa? Ukweli wa kaiawaida utasema hapana. Adhabu ngumu za kazi zinatesa ni sawa laikini haziwezi kuogopwa kama kifo.
Jamii kufaidika kiuchumi ni sawa lakini lengo la adhabu sio kunufaika kiuchumi bali kuzuia makosa mengi kama hayo kujirudia na kuathiri jamii isiyokuwa na hatia. Hata hivyo, mwisho wa siku kama adhabu hiyo bado inafaa katika mazingira yesu ni watanzania walio wengi ndio wataamua.
Kichwa cha maneno hapa ni adhabu ya kifo kupitwa na wakati. Hiyo inaashiria kuna wakatii ilikuwa inafaa. Ni mabadiliko gani ya msingi katika maisha ya mwanaadamu yanayomfanya mwanaadamu wa leo kutokuwa mhalifu samna kama wa zamani ili tuseme kwamba kwa leo imepitwa na wakati. Mimi naona kadili muda unavyozidi kwenda binaadamu tunakuwa wakatili sana na kuongeza tekinologia ya kuuwana. Ningekuwa mimi ningesema adhabu ya kifo ni muafaka zaidi kwa sasa kuliko enzi za manabii au enzi za ujima