Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,318
- 33,125
Mwanamke mmoja raia wa Poland ameifungulia mashtaka hoteli moja ya nchini Misri kwa kusababisha binti yake mwenye umri wa miaka 13 kupata ujauzito kutokana na mbegu za kiume alizokumbana nazo wakati akiogelea kwenye bwawa la kuogelea la hoteli hiyo.
Mama wa binti huyo aliyejulikana kwa jina la Magdalena Kwiatkowska alirudi Poland na binti yake huyo mwenye umri wa miaka 13 kutoka vakesheni nchini Misri binti yake huyo akiwa tayari ameishapata ujauzito.
Magdalena alidai kuwa binti yake alipata ujauzito baada ya kujitosa kuogelea kwenye bwawa la kuogolea la hoteli hiyo ambalo wanawake na wanaume walikuwa wakichanganyika.
Magdalena alisisitiza kuwa binti yake alipata ujauzito baada ya kukumbana na mbegu za kiume wakati akiogelea kwenye bwawa la kuogelea la hoteli hiyo.
Magdalena ameifungulia kesi hoteli hiyo akidai alipwe fidia.
Chanzo kimoja cha habari kilisema kuwa mama huyo anasisitiza kuwa ana uhakika wa asilimia mia moja kuwa binti yake hakufanya mapenzi na mvulana yoyote wakati alipokuwa hotelini hapo.
"Magdalena amedhamiria kuendelea na kesi yake ya kudai fidia" kilisema chanzo hicho.
Mamlaka ya utalii ya Poland jijini Warsaw ilithibitisha kwamba imepokea taarifa ya kesi hiyo ambayo haijawahi kutokea duniani.
http://www.nifahamishe.com/NewsDetails.aspx?NewsID=2463986&&Cat=2