Melki the Storyteller
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 5,700
- 9,778
Hakika wanawake si binadamu, ni viumbe wa ajabu sana kulinganishwa na majini au hata nyoka. TUISHI NAO KWA AKILI
Mwaka 2017 huyu binti alikuwa kidato cha nne. Kwa bahati mbaya alipata ujauzito mwezi wa tatu. Juhudi za kumtafuta mhusika zilimwangukia kijana aliyekuwa anachukua diploma ya unesi katika college X.
Tulimshambulia kwa maneno makali na laana za kutosha kwa dhambi ya kuzikatisha ndoto za binti wa baba wa rafiki yangu ambaye familia yetu na yake zinaheshimiana na zina historia ndefu kidogo huko nyuma.
Kama ilivyo ada, sheria ilifuata mkondo wake. Baada ya mchakato kukamilika, kijana alihukumiwa kifungo cha miaka 30.
Nami kwa mara ya kwanza nilihudhuria hukumu hiyo mahakamani na ndipo kuthibitisha kuwa kumbe kifungo cha kumbebesha ujauzito mwanafunzi huwa kipo, na ndipo nilipoanza kuwaogopa watoto wa kike wanaovaa sketi zenye marinda.
Ujauzito wa binti ulilelewa na familia yake japo baba wa binti alikuwa tayari kashamfukuza binti yake ambaye alitoweka kwa kipindi cha takribani wiki mbili nyumbani, lakini baadae aliamua kupunguza hasira. Binti alifanikisha kujifungua kitoto cha kiume.
Mwaka 2018 mwezi wa tatu/ wa nne, kama sijasahau ilikuwa ni wiki ya pasaka, alijitokeza kijana akatangaza nia ya kumuoa, inavyosemekana walifahamiana wakiwa kanisani anaposali binti! Huyu kijana alifanya kazi ya kuuza matunda.
Familia ya binti iliamua kukubaliana na matokeo ili kupunguza mzigo nyumbani na kuepusha ile hali ya binti kubeba ujauzito wa pili akiwa nyumbani. Basi, ndoa ikapangwa, hatua zikafuatwa, binti akaolewa pasi na mahari.
Mwezi mmoja baadae, familia ya binti ikajipanga, ikachanga pesa kwa ajili ya mtaji ilikusudi binti yao aishi maisha mema akiwa na mmewe huyo. Walifungua biashara ya maana tu. Maisha yakasonga, kukawepo ushemeji, tukasahau tukio kabisa.
Mwezi June mwaka huu (2022) kulitokea sintofahamu katika ndoa ya binti kiasi cha kutengana kabisa, yeye na mumewe, ila ni baada ya kipigo kitakatifu alichoambulia binti.
Mume alitokomea kusikojulikana akiwa na mapato karibu yote ya biashara waliyokuwa wanaendesha na mtaji juu, kilichobaki kwenye duka lao hilo la jumla ni bidhaa tu.
Binti aliamua kurejea nyumbani kwa wazazi wake ili kutuliza akili, lakini tokea kufika kwake nyumbani pale, wazazi wake wamekuwa wakitutaarifu kuwa binti yao akili haitulii, hajatulia kabisa na amekuwa kama mtu aliyeathiriwa kisaikolojia. Muda mwingine huzungumza peke yake, kulia lia tu, kuzubaa. Istoshe hapo alipo ana ujauzito wa miezi miwili.
Katikati ya mwezi huu wa nane, baadhi ya watu muhimu kutoka familia yetu ukiniongeza mimi ambaye sielewi ni kwanini wameona ni vyema kushiriki mipango hiyo tuliitwa kwenye kikao cha dharura cha familia yao, ndipo baba wa binti alivyotueleza kuwa, binti yake amekili kuwa kijana aliyefungwa jela siye mwenye mtoto wa kwanza wa binti.
Bali mwenye mtoto ni huyo mwanaume aliyemuoa binti! Inavyosemekana katika mahusiano yao, walijikuta wakipeana ujauzito kimasihara. Kwa kuwa binti alimpenda sana mhusika, alikubali kusikiliza ushauri wake aliopewa wa kumtafuta mwanaume mwingine na kumbambikizia ujauzito ili kumnusuru mwanaume huyo kwenda jela ili mtoto apate malezi ya baba aliye sahihi.
Kwa kuwa binti alimpenda mwanaume huyo, hakuona tatizo kufuata ushauri huo
Mpaka sasa hakuna mchango wa maana wa mawazo uliotolewa!
Nimekuwa nikijiuliza, hivi kuna uwezekano wowote wa ku cancel kifungo? Kwa kuwa binti kakili kuwa yule kijana si mhusika?
Kila siku huwa nawakumbusha kuwa wanawake sio watu wazuri, mnaniona kuwa ni mtu mwenye chuki binafsi! Mnaona sasa?