Ada elekezi shule binafsi tayari

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
TUME ya wataalamu waliokuwa wanakusanya maoni ya wadau wa elimu na kukokotoa ada elekezi kwa shule za msingi na sekondari zisizo za Serikali, wamemaliza kazi yao na tayari wamekabidhi ripoti hiyo kwa Serikali.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Sifuni Mchome amethibitisha kukamilika kwa kazi hiyo na sasa kinachofuata ni uchambuzi wa ripoti pamoja na kuangalia miongozo ya Serikali kabla ya ada elekezi kutangazwa na kuanza kutumika kwa majaribio mwakani Januari.

Wataalamu hao walipewa kazi na Serikali kuandaa ada elekezi baada ya kupata maoni ya wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wazazi, wananchi, wamiliki wa shule binafsi, walimu, asasi zisizokuwa za kiserikali, taasisi mbalimbali za umma na wadau wengine ambao wanaweza kusaidia katika ukokotoaji huo wa ada.

Katika ukokotoaji huo, wizara inaandaa mchanganuo wa gharama za kumsomesha mwanafunzi kuanzia elimu ya awali, darasa la kwanza hadi kidato cha sita kwa nia ya kutoa ada hiyo elekezi ambazo zitaendana na huduma itolewayo kwa shule zisizo za Serikali.

Alisema shule zitakazoteuliwa kuanza kutumika kwa ada hizo zitatangazwa pia na wizara hiyo baada ya kukutana na wamiliki wa shule hizo na kufanya nao mazungumzo.

Alisema majaribio hayo yatafanyika katika baadhi ya shule Tanzania nzima na sio katika baadhi ya mikoa tu.
 
Alisema shule zitakazoteuliwa kuanza kutumika kwa ada hizo zitatangazwa pia na wizara hiyo baada ya kukutana na wamiliki wa shule hizo na kufanya nao mazungumzo.
 
Alisema shule zitakazoteuliwa kuanza kutumika kwa ada hizo zitatangazwa pia na wizara hiyo baada ya kukutana na wamiliki wa shule hizo na kufanya nao mazungumzo.
Kwa hiyo wazazi/ walezi nasubiri wasilipe?
 
Eti MAJARIBIO....

Majaribiooooo.... 😨😨😨💀👊👌

Watoe Amri tu, hakuna majaribio...!!

Priveta schools fees... eg

Ada kwa day... Max. 500,000

Boarding, Max... 1,500,000

Hakuna zaidi ya hapo... hakuna michango yoyote... shule itakayo changisha kufungiwa haraka sana
..

Serikali inafanya majaribio kwani ni ADA NI DAWA..? 😨😨
 
Kwa mtazamo wangu sidhani kama hili swala la karo elekezi linawezekana......kwani tution fee itakuwa ndogo.....ila ukiangalia gharama za maradhi na chakula sidhani kama hapo kunaweza kuwa na mjadala!!!!
Katika shule zilizo bora....mtoto anakula milo minne!! Anapata matunda,maziwa nk.....
Maradhi mtoto analala chumba kimoja watoto wawili.....bafu zuri na choo cha maji safi.......kwa mazingira kama haya ni bora kumuambia mwenye shule afunge shule afanye biashara nyingine........kinyume na hapo naamini haitawezekana.
 
Serikali ya JPM imeufyata kwa wamiliki wa shule binafsi. Hizo ni shule tu je madawa ya kulevya wataweza? Mikwara yote ile mumegeukia majaribio!!!? Hiyo sasa ndiyo imekufa kifo cha mende. Hakutakuwa tena na ada elekezi. Badala yake serikali ya JPM ndiyo itaelekezwa.
 
Kwa mtazamo wangu sidhani kama hili swala la karo elekezi linawezekana......kwani tution fee itakuwa ndogo.....ila ukiangalia gharama za maradhi na chakula sidhani kama hapo kunaweza kuwa na mjadala!!!!
Katika shule zilizo bora....mtoto anakula milo minne!! Anapata matunda,maziwa nk.....
Maradhi mtoto analala chumba kimoja watoto wawili.....bafu zuri na choo cha maji safi.......kwa mazingira kama haya ni bora kumuambia mwenye shule afunge shule afanye biashara nyingine........kinyume na hapo naamini haitawezekana.

Hapo ulipoandika "gharama za maradhi" umenichekesha sana!!
 
Eti MAJARIBIO....

Majaribiooooo.... 

Watoe Amri tu, hakuna majaribio...!!

Priveta schools fees... eg

Ada kwa day... Max. 500,000

Boarding, Max... 1,500,000

Hakuna zaidi ya hapo... hakuna michango yoyote... shule itakayo changisha kufungiwa haraka sana
..

Serikali inafanya majaribio kwani ni ADA NI DAWA..? 
kama mfumo hapa kazi tu wanaenda kujaribu nini? kinachotakiwa ni amri hawataki majengo wakafugie kuku.
 
Eti MAJARIBIO....

Majaribiooooo.... 

Watoe Amri tu, hakuna majaribio...!!

Priveta schools fees... eg

Ada kwa day... Max. 500,000

Boarding, Max... 1,500,000

Hakuna zaidi ya hapo... hakuna michango yoyote... shule itakayo changisha kufungiwa haraka sana
..

Serikali inafanya majaribio kwani ni ADA NI DAWA..? 
Nadhani majaribio ni CHANJO!
 
hapa kidogo naona kama kasi ya MH Magufuli, inaelekea kupunguzwa na vigogo wenye shule hizi.

Ni ukweli usiopingika kwamba shule hizi zimekuwa mzigo mzito kwa walaji, gharama wanazotoza haziendani na uduma na ubora wa shule husika.

Majengo hovyo. Mazingira mabaya kabisa, njoo kwenye Ada ni kubwa sana, hapa serikali isipepese Macho itoe hamri moja full stop.
 
Hamna kitu hapo, kwanini iwe majaribio na kwanini iwe kwa baadhi ya shule?

.....nilichokiona kuna shule zina sauti kuliko serikali....
Yaani kabisaaaaa.... ETI SHULE ZA SERIKALI ZOTE ELIMU BURE TOKA JANUARY 2016, LAKINI ZA BINAFSI BAADHI ADA ELEKEZI NA BAADHI ZITAACHWA NA MIADA YAO MIKUBWA..... Ipo namna
 
Hamna kitu hapo, kwanini iwe majaribio na kwanini iwe kwa baadhi ya shule?

.....nilichokiona kuna shule zina sauti kuliko serikali....

Tatizo wafanya maamuzi ndo wamiliki wa hizo shule au wana hisa kwenye hayo mashule, what do you expect my dear? Zaidi wanaharibu, utashangaa shule zilizokuwa chini kiada nazo wanapandisha hadi kwenye cap price
 
Hii ishu ni kizungumkuti. Huwa kila nikipita kwenye hizo shule binafsi napata maswali sana, hasa juu ya gharama walizowekeza, mfano Braedburn, Feza, IST, .....
Kwa nje, hizi shule ni bora kuliko halmashauri kibao, hasa za wilaya, hapa nchini.
Ada elekezi zilikuwa tangu 2008, hakuna utekelezaji. Kadiri ya habari hii, naona kizungumkuti, ikizingatiwa Januari imekaribia.
 
Kwa mtazamo wangu sidhani kama hili swala la karo elekezi linawezekana......kwani tution fee itakuwa ndogo.....ila ukiangalia gharama za maradhi na chakula sidhani kama hapo kunaweza kuwa na mjadala!!!!
Katika shule zilizo bora....mtoto anakula milo minne!! Anapata matunda,maziwa nk.....
Maradhi mtoto analala chumba kimoja watoto wawili.....bafu zuri na choo cha maji safi.......kwa mazingira kama haya ni bora kumuambia mwenye shule afunge shule afanye biashara nyingine........kinyume na hapo naamini haitawezekana.
Gharama za maradhi???labda alimaanisha malazi au gharama za matibabu..
 
Watoto wanalishwa wali maharage daily,vitafunio andazi za mia mia na chai ya strungi halafu ada milioni 10
 
Hizi shule ni chache sana zinazo hudumia wanafunzi kwa gharama halisi za ada wanazotoza nasema hivyo kutokana kuwa nina wadogo zangu mmoja yupo shule moja arusha mwingine Dar lakini nikiwauliza wanachokula hakiendani na ada yenyewe unakuta ada 2,998,000 lakini wanakula hadi makande, hawa jamaa wanapata faida kubwa kupitia migongo ya Wazazi wenye uchu wa kuwapa watoto wao elimu bora, mapendekezo kungekuwapo wakaguzi pamoja na kukagua taaluma wakague na swala la wanafunzi kupewa lishe inayolingana na pesa za chakula wanazotoa.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom