Ada elekezi shule binafsi tayari

Ada elekezi shule binafsi tayari

tatizo sio ada ila michango ni mingi na haina kichwa wala miguu na haikwepeki, unamlazimshaje mzazi achangie ujenzimwa shule wakati mwanawe anasoma miaka minne kisha anaondok? serikali iangalie hili suala kwa jicho la tatu wazazi wanaumia sana na hawana pa kusemea
 
Serikali ni lazima iwe imara.Inaelekea inayumbishwa na wamiliki wa shule ambao wengine labda ni watu wakubwa serikalini au ambao wana ushawishi mkubwa serikalini.Kusiwe na kubembelezana.Kuwe na basic fee kwa watoto wote,kwenye shule binafsi,it doesn't matter who.Huku kuanza kutengeneza madaraja ndiko kunako haribu nchi.Ambaye anajiona ana hela apeleke mtoto wake nje ya nchi.Na ambaye anaona shule yake haiwezi kutoza ada hiyo afunge.
TUME ya wataalamu waliokuwa wanakusanya maoni ya wadau wa elimu na kukokotoa ada elekezi kwa shule za msingi na sekondari zisizo za Serikali, wamemaliza kazi yao na tayari wamekabidhi ripoti hiyo kwa Serikali.

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Sifuni Mchome amethibitisha kukamilika kwa kazi hiyo na sasa kinachofuata ni uchambuzi wa ripoti pamoja na kuangalia miongozo ya Serikali kabla ya ada elekezi kutangazwa na kuanza kutumika kwa majaribio mwakani Januari.

Wataalamu hao walipewa kazi na Serikali kuandaa ada elekezi baada ya kupata maoni ya wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo wazazi, wananchi, wamiliki wa shule binafsi, walimu, asasi zisizokuwa za kiserikali, taasisi mbalimbali za umma na wadau wengine ambao wanaweza kusaidia katika ukokotoaji huo wa ada.

Katika ukokotoaji huo, wizara inaandaa mchanganuo wa gharama za kumsomesha mwanafunzi kuanzia elimu ya awali, darasa la kwanza hadi kidato cha sita kwa nia ya kutoa ada hiyo elekezi ambazo zitaendana na huduma itolewayo kwa shule zisizo za Serikali.

Alisema shule zitakazoteuliwa kuanza kutumika kwa ada hizo zitatangazwa pia na wizara hiyo baada ya kukutana na wamiliki wa shule hizo na kufanya nao mazungumzo.

Alisema majaribio hayo yatafanyika katika baadhi ya shule Tanzania nzima na sio katika baadhi ya mikoa tu.
 
....................................

Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Sifuni Mchome amethibitisha kukamilika kwa kazi hiyo na sasa kinachofuata ni uchambuzi wa ripoti pamoja na kuangalia miongozo ya Serikali kabla ya ada elekezi kutangazwa na kuanza kutumika kwa majaribio mwakani Januari.

...............................Alisema shule zitakazoteuliwa kuanza kutumika kwa ada hizo zitatangazwa pia na wizara hiyo baada ya kukutana na wamiliki wa shule hizo na kufanya nao mazungumzo.

Alisema majaribio hayo yatafanyika katika baadhi ya shule Tanzania nzima na sio katika baadhi ya mikoa tu.

Kwa ufupi tu, binafsi siamini kama tunaye mtu sahihi ktk nafasi hiyo. Huyu alikuwa Katibu mkuu wa Wizara ya Elimu na Ufundi. Sasa hivi wizara ni Elimu Sayansi,Teknolojia na ufundi, katibu mkuu bado hajulikani ni nani baada ya wizara mbili kuwekwa pamoja, yeye huyu amejiteua au ni makosa ya waandishi wa habari?. Natumaini sana huyu aliyejitangaza ataondolewa, he is a non-starter with reference to his previous action.

Pili anawezaje kututangazia uozo kama huu. Serikali inafanya majaribio! Eti, itazungumza na wamiliki wa shule, no logical move. Unawapa leseni na vibali watu ukiwaambia wanatakiwa watoe huduma ya elimu, wao wanafanya biashara ya elimu, halafu unayejiita katibu mkuu unasema tunakaa na ,........ Yaani hata hajui pa kuanzia.

My simple approach would have been to itemize non-educational payments ambazo zinawafanya watu waumizwe. Acha ,mambo ya kulazimisha wazazi kulipia tours, kulipia kufuliwa nguo, kulipiwa first aid kit kwa mamilioni kadhaa utadhani watafanyiwa surgical operation, kulipiwa uniform, kulipiwa wafagiaji darasani, etc, haya yote yanawekwa ili kupata nafasi ya kupanga gharama watakazo. Hawa watoto ni wa TZ na kuna mambo tuataka wafanye kwa mikono yao. There must be TZ kid values.
 
Katika Kero niliyonayo ni hili la michango tena ya kulazimishwa na wamiliki wa shule
Nikawa na Mtoto shule moja ya msingi iliyopo Dodoma, Kero kubwa zaidi na kinachonikwza ni shule hiyo kutumia mgogongo wa Dini, jina la shule na Kujenga kanisa kubwa mkoa mzima na kuweka msalaba mwekundu mrefu ili kila anayeingia Dodoma aone. amejenga majengo mazuri sawa, ila

Tunalazimishwa kununua sokisi zilizowekwa alama yao kwa 5000, mtaani tunanunua 1500
Tunalazimishwa kununua tracsuit, mjini inauzwa 18,000 hdi 20,000, wao wauza 30,000 na lazima ununue kwao. sweeta 30,000/=

watoto walinaopata kipaima na graduation lazima uchange 220,000/=
ameweka term 3 kwa makusudi ili anapokwambia ada ya bweni ni 3M--Hii ndio bei mpya ya kuanza January) from 2.7M, term 3 ili utoe 1M kila baada ya miezi 3

term 3 hizo wanafunga mara 3, na kila term week hazipungui 4, hivyo kwa mwaka watoto lazima wafunge miezi zaidi ya mitatu, mwaka jana December wlifunga 8 weeks, that means walifunga over 4 months. hapa issue ni kupunguza msosi

I am sincerely sick and tired with Martin Luther anatumia jina vibaya... dada mtu anasoma the best secondary boarding tuna;ipa 1.8M ila mdogo mtu tumeandikiwa 3M plus malosoloso mengine
 
Una point ila kiswahili sahihi ni malazi sio maradhi.
Kwa mtazamo wangu sidhani kama hili swala la karo elekezi linawezekana......kwani tution fee itakuwa ndogo.....ila ukiangalia gharama za maradhi na chakula sidhani kama hapo kunaweza kuwa na mjadala!!!!
Katika shule zilizo bora....mtoto anakula milo minne!! Anapata matunda,maziwa nk.....
Maradhi mtoto analala chumba kimoja watoto wawili.....bafu zuri na choo cha maji safi.......kwa mazingira kama haya ni bora kumuambia mwenye shule afunge shule afanye biashara nyingine........kinyume na hapo naamini haitawezekana.
 
Yaani kabisaaaaa.... ETI SHULE ZA SERIKALI ZOTE ELIMU BURE TOKA JANUARY 2016, LAKINI ZA BINAFSI BAADHI ADA ELEKEZI NA BAADHI ZITAACHWA NA MIADA YAO MIKUBWA..... Ipo namna

Hakuna kitu kama elimu ya bure, inagharimiwa kwa kodi unazotoa serkalini. Kwa maana katika shule za serkali walimu wanalipwa mishahara, vitabu vinanunuliwa, huduma yote ya elimu inalipiwa gharama kubwa na hazina. hivyo ili na shule za binafsi kutoa elimu "bure" au kwa "ada ndongo sana" inabidi hazina ya serkali igharamie huduma hizi! Hapo elimu itakuwa bure!!!
 
Tujiulize shule za serikali uwezo wake ni kuchukua wanafunzi wangapi? itapendeza kama ziwe na uwezo wa kuwa accomodate wanafunzi wote wenye sifa lakini wao waamue kwenda private. lakini kama nafasi ni chache huko serikalini hao wanaobaki ni watanzania pia,wanahitaji hiyo elimu ya bure. je,waende huko kusoma kwa masononeko? tusije tengeneza tabaka huko mbele kwa sera zetu za kukurupuka.
 
Serikali iachane na suala LA ada elekezi ya SHULE binafsi cha msingi iimarishe SHULE zake ziwe na kiwango safi madawati,mabweni,chakula kizuri,maabara,maktaba zenye vitabu,walimu wapewe mishahara na haki zao stahiki bila vikwazo hakuna mzazi au mlezi aache bure ampeleke mtoto private?tuache siasa ktk elimu na division za ajabu ajabu.Jemedari JPM hili kwako jepesi acha private watambe SHULE za serikali zikiwa bora private wataisoma namba
 
Usanii mwingine huu, wizara ya wasomi wasio na elimu . Hivi mnafanya majaribio gani?

Fanyeni hivi, chukua gharama inayomsomesha mwanafunzi ktk shule ya vipaji maalum ndiyo iwe ada katika shule binafsi.
 
Da yaan ada ya primary unafkr ni chuo..... Siwez Lipa m3.2 kwa secondary hata kama hiyo ninazo
 
Hakuna Majaribio!..unapotaka kuzima moto unauzima tu na si kufanya majaribio..
 
Majaribio ili shule za wakubwa zisihusike
 
Suluhisho ni serikali kuboresha shule zake. Hili likifanyika shule binafsi kwa aslimia kubwa watarekebisha ada zao.

Mkuu nakubaliana na wewe kwani kinachotufanya kupeleka watoto huko ni ubora wa mazingira na elimu,serekali wakiboresha hatutakuwa na sababu ya kupeleka watoto huko maana ni bure kabisaa!lkn kuwapangia bei ni vigumu kutokana na tofauti kubwa ya huduma wanazotoa.
 
hapa kidogo naona kama kasi ya MH Magufuli, inaelekea kupunguzwa na vigogo wenye shule hizi.

Ni ukweli usiopingika kwamba shule hizi zimekuwa mzigo mzito kwa walaji, gharama wanazotoza haziendani na uduma na ubora wa shule husika.

Majengo hovyo. Mazingira mabaya kabisa, njoo kwenye Ada ni kubwa sana, hapa serikali isipepese Macho itoe hamri moja full stop.

Hivi kizazi hiki mnafundishwa nini huko shuleni? pumbavu kabisa wewe, hiyo herufi "h" mbona unaifanyia ufisadi. ndio mnataka watoto wetu wakasome shule zinazofundisha hivi kiswahili?
 
Hakuna haja yakufanya elimu bure wala ada elekezi mfumo ndio unatuongoza yaan ubepari.... Kla mtu apambane awezavyo kulingana na uwezo wake.... Mambo ya bure nikudekezana yaandaliwe mazngira ya kla mtu kufanya kazi apate kipato kuendesha maisha.... Serikal iboreshe mazngira ya shule zake kuvutia wasiosoma kwenye shule hzo mbona zamani ilikuwa ni ufahari kusoma shule za Serikal kuliko private...? Kila kitu kinawezekana hao wa private chamsingi walipishwe kodi ikiwezekana wapewe zle machine za Efd.
 
Hivi kizazi hiki mnafundishwa nini huko shuleni? pumbavu kabisa wewe, hiyo herufi "h" mbona unaifanyia ufisadi. ndio mnataka watoto wetu wakasome shule zinazofundisha hivi kiswahili?
Mkuu nashukuru sana kuliona hili. Na kuna hili tatizo la "r" na "l" limekuwa kero.
 
Hakuna kitu kama elimu ya bure, inagharimiwa kwa kodi unazotoa serkalini. Kwa maana katika shule za serkali walimu wanalipwa mishahara, vitabu vinanunuliwa, huduma yote ya elimu inalipiwa gharama kubwa na hazina. hivyo ili na shule za binafsi kutoa elimu "bure" au kwa "ada ndongo sana" inabidi hazina ya serkali igharamie huduma hizi! Hapo elimu itakuwa bure!!!
Ni kweli mkuu, lakini ukumbuke hata kabla hawajasema elimu bure,
1. Kodi ilikuwepo
2. Ada tumelipa
3. Michango mbalimbali tumelipa

Kwa kuangalia hilo unaweza ukasema elimu ni bure...
 
Back
Top Bottom