Ada elekezi shule binafsi tayari

Ada elekezi shule binafsi tayari

Mhhh

Hapa inaleta shaka

Rais wangu Ndugu JPM tafadhali sana iweke hii sawa.

Shukran

Respect !!!
 
Hii ya Ada elekezi kwa baadhi ya Shule eti kama sehemu ya majaribio huu ni upuuzi mkubwa, ingekuwa hivyo hata SUMATRA wangetoa Bei elekezi kwa majaribio kwa baadhi ya Vituo vya Mafuta tu.

Waandishi wa Habari waupeleke huu mjadala mbele zaidi ili sauti zetu ziweze kusikika hata kama ni Petition iandaliwe Wadau wa Elimu tumwage Wino huyo Katibu Mkuu ana beep lazima tumpigie.

Nafahamu Waheshimiwa Wabunge wengi waliwekeza kwenye Shule kama plan B ya kuingiza kipato kwahiyo tusitegemee usaidizi wa haraka kutoka kwao.

Ifike mahali tuwe na mfumo rafiki wa kuhoji matendo na maamuzi ya Viongozi wetu kwa njia rahisi zaidi, siku hizi kuna DUBWASHA linaitwa NENDA MAHAKAMANI hata jambo dogo la uamuzi wa dakika 5 utaambiwa hii nchi inafuata utawala wa Sheria nenda Mahakamani ukapinge. Kiuhalisia ukienda kwenye Mahakama zetu nyingi zina sifa ya kutaja tarehe za kwenda na kurudi Mahakamani
 
Kwa mtazamo wangu sidhani kama hili swala la karo elekezi linawezekana......kwani tution fee itakuwa ndogo.....ila ukiangalia gharama za maradhi na chakula sidhani kama hapo kunaweza kuwa na mjadala!!!!
Katika shule zilizo bora....mtoto anakula milo minne!! Anapata matunda,maziwa nk.....
Maradhi mtoto analala chumba kimoja watoto wawili.....bafu zuri na choo cha maji safi.......kwa mazingira kama haya ni bora kumuambia mwenye shule afunge shule afanye biashara nyingine........kinyume na hapo naamini haitawezekana.

Mfano wa shule zenye huduma hizo ni kama shule gani?
 
Eti MAJARIBIO....

Majaribiooooo.... 😨😨😨💀👊👌

Watoe Amri tu, hakuna majaribio...!!

Priveta schools fees... eg

Ada kwa day... Max. 500,000

Boarding, Max... 1,500,000

Hakuna zaidi ya hapo... hakuna michango yoyote... shule itakayo changisha kufungiwa haraka sana
..

Serikali inafanya majaribio kwani ni ADA NI DAWA..? 😨😨

Cjawai ona kitu kama hichi jaman et bei ya majaribio
 
[QUOTE

Ni ukweli usiopingika kwamba shule hizi zimekuwa mzigo mzito kwa walaji,
ulilazimishwa umpeleke mwanao huko? Shule za kata hukuziona?
 
wewe siumeshalipa milion 8 kula feza sec?

Hamna kitu hapo, kwanini iwe majaribio na kwanini iwe kwa baadhi ya shule?

.....nilichokiona kuna shule zina sauti kuliko serikali....
 
Leo nimesikia kitu redioni eti Serikali ya Magufuli inataka mtoto atakapofika darasa la 3 awe amejua kusoma na Kuandika la
sivyo huyo mwalimu aache kazi mwenyewe! Nimejiuliza na je kwa wale walimu wanaofundisha darasa moja lenye wanafunzi 100 itakuwaje?
 
Hizi shule ni chache sana zinazo hudumia wanafunzi kwa gharama halisi za ada wanazotoza nasema hivyo kutokana kuwa nina wadogo zangu mmoja yupo shule moja arusha mwingine Dar lakini nikiwauliza wanachokula hakiendani na ada yenyewe unakuta ada 2,998,000 lakini wanakula hadi makande, hawa jamaa wanapata faida kubwa kupitia migongo ya Wazazi wenye uchu wa kuwapa watoto wao elimu bora, mapendekezo kungekuwapo wakaguzi pamoja na kukagua taaluma wakague na swala la wanafunzi kupewa lishe inayolingana na pesa za chakula wanazotoa.

Mkuu, mwanangu yupo st Joseph millennium pale goba juzi kati kanilalamikia sana kuwa anataka kuhama sbb msosi ni ndondo kwenda mbele yaani balaa. Nimekomaa kibaba baba tu kwamba nooo! Lknni kaja kugundua kuwa ile fees wazazi tukilipa haiendi straight shuleni kumbe akaunti ni ya dayosisi ya dsm so mpaka kamati ikae ndo hela iende shule. Ada ni mil 3.2 kwa mwaka. Hii haki kweli?
 
Mkuu, mwanangu yupo st Joseph millennium pale goba juzi kati kanilalamikia sana kuwa anataka kuhama sbb msosi ni ndondo kwenda mbele yaani balaa. Nimekomaa kibaba baba tu kwamba nooo! Lknni kaja kugundua kuwa ile fees wazazi tukilipa haiendi straight shuleni kumbe akaunti ni ya dayosisi ya dsm so mpaka kamati ikae ndo hela iende shule. Ada ni mil 3.2 kwa mwaka. Hii haki kweli?

Hawa watu ndo zao.
 
Ndugu rais,elimu ni huduma na elmu ni biashara,wawekezaji wapewe hyo ada,akiona haina maslah abinafsishe,hyo ada inalipa
 
Hakuna cha feza wala nani,wale wanaotoza zaid ya mil 3 warud 2.5,wakiona ngumu waende nchi nyngne,msimamo uwe hvo tuone
 
Hakuna cha feza wala nani,wale wanaotoza zaid ya mil 3 warud 2.5,wakiona ngumu waende nchi nyngne,msimamo uwe hvo tuone
Hii 2.5 unapendekeza kwa ajili ya vyuo gani? Alafu ni kwa diploma, bachelor na kundelea au?
 
peleka mwanao shule za serikali... ya ngoswe mwachie ngoswe
 
Huyo Katibu anazungumza ada elekezi leo wakati watoto wake wamesoma na bado wadogo wanasoma private za bei mbaya. Toka ameingia wizarani analipa mamilioni ya ada. Tayari keshalipia za mwakani pia. Hapo hamna elekezi wala pelekezi, wanacheza na akili zetu watanzania sababu tunaishi kwa hope tu.
 
Back
Top Bottom