ACT Wazalendo yakataa kushiriki Kikao cha Msajili

ACT Wazalendo

JF-Expert Member
May 5, 2014
499
1,000
TAARIFA KWA UMMA.

Tumepata taarifa kupitia vyombo vya habari kuwa kikao cha Jeshi la Polisi na Vyama vya Siasa kilichoitishwa na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa kimepangwa kufanyika tarehe 21 Oktoba 2021.

Baada ya tafakuri ya kina, ACT Wazalendo tumeamua kuwa HATUTASHIRIKI kikao hicho kwa sababu zifuatazo;-

1. Tarehe 21 hadi 22 Oktoba 2021, viongozi wakuu wa ACT Wazalendo watakuwa kwenye Mkutano Mkuu wa Kitaifa wa Haki, Amani na Maridhiano ulioitishwa na Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD). Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ndugu Samia Suluhu Hassan.

2. Baada ya Msajili wa Vyama vya Siasa kutangaza kikao cha Polisi na Vyama vya Siasa, Chama Cha ACT Wazalendo kupitia Kiongozi wa Chama Ndugu Zitto Kabwe, kilimwandikia Msajili kuwa kikao hicho kimjumuishe Waziri wa Mambo ya Ndani ambaye ndiye mwenye dhamana ya kisiasa ya Jeshi la Polisi. Hadi sasa hatujapata mrejesho wa suala hilo na mwelekeo ni kuwa kikao hicho kitakuwa Cha Polisi na Vyama vya Siasa pekee.

3. Matamshi ya IGP Simon Sirro baada ya kikao chake na Msajili wa Vyama vya Siasa hayaonyeshi nia njema ya kikao hicho. Kauli yake kuwa nchini Tanzania hakuna shida kuhusu mikutano ya nje na kwamba tatizo lipo kwenye mikutano ya ndani na inabidi sheria iwekwe sawa ni dalili ya wazi kuwa kikao hicho kinaweza kutumika kubinya zaidi shughuli za kisiasa nchini.


Imetolewa na:

Salim A. Bimani,
Katibu wa Habari, Uenezi na Mahusiano na Umma,
ACT Wazalendo.
26 Septemba, 2021.

Screenshot_20210926-090126_1.jpg
 

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
5,873
2,000
Nyie ni wanafiki, mlisema hamtambui uchaguzi wa 2020 mkasaini na CHADEMA sijui tamko lenu halafu iliishia wapi ?
 

Babu Ochu

JF-Expert Member
May 30, 2021
368
1,000
Big up ACT
Huyu msajilli na Sirro ni maadui wakubwa wa vyama vya upinzani ,sasa kikao wanachoitisha wao wenyewe kina maana gani?
 

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
15,235
2,000
... ni ujinga kukaa vikao vya kujadili utekelezaji wa Katiba na Sheria za nchi! Katiba na sheria sio suala la kujadili tutekeleze au la; ni utekelezaji tu hakuna option nyingine!
Hawa ATC Wazalendo waliambiwa tangu mwanzo hiki kikao ni cha kupumbavu lakini Zitto akawa anasisitiza kuwa watashiriki. Hata hizo sababu mbili za kwanza walizotoa hazina mantiki yoyote. Sababu ya mwisho ndiyo mzizi wa kila kitu. i.e. kushiriki hicho kikao ni ujinga uliopitiliza.
 

Vessel

JF-Expert Member
Aug 29, 2018
7,539
2,000
... ni ujinga kukaa vikao vya kujadili utekelezaji wa Katiba na Sheria za nchi! Katiba na sheria sio suala la kujadili tutekeleze au la; ni utekelezaji tu hakuna option nyingine!
Hivyo ni viwango vya weledi wao.
 

VAPS

JF-Expert Member
Jul 10, 2012
5,352
2,000
Hivi Sirro bado anahitaji hisani ya uteuzi baada ya kustaafu!?
 

Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Nov 28, 2020
1,858
2,000
Kwani sheria za nchi kupitia mama wa nchi katiba inazungumza nini kuhusu siasa ? Mbona tumekuwa wajinga kiasi hiki yaani Sasa sheria zifanyiwe mjadala badala ya kutekelezwa
 

Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
43,370
2,000
Hivi Sirro bado anahitaji hisani ya uteuzi baada ya kustaafu!?
Hawatoshekagi hao, anafikiria kuongezewa muda, kimsingi umri wa kustaafu ameshafikisha.

Astaafu sasa, mama ateuwe IGP mpya.
 

kwitao

Member
Apr 30, 2021
98
125
Huyu msajiri nadhani atakuwa na maslahi na ccm au Polisi.

Unawezaje kukaa na polisi mkaelewana kisha uje kutaka kukutana na Polisi,vyama vya siasa na msajiri. Vyama vya siasa msikubali kuhudhuria, nikihudhuria mmekwisha,mnajua akichoelewana na hao polisi! Sasa anakuja kwenu na polisi wakiwepo ili malengo yao yatimizwe.

Sioni haja ya vikao, mkutano ya siasa ya hadhara au ya ndani ipo kwa mujibu wa katiba, kwa kuzingatia taratibu fulafulani. Msajiri aanze na Rais kwa nini anazuia vyama vya siasa kufanya kazi yao? Kisha polisi.

Kwanini wanavunja katiba.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom