ACT - Wazalendo Wamnyooshea kidole Zitto!

ACT - Wazalendo Wamnyooshea kidole Zitto!

zitto mwami ayyatollah mmeshaambiwa ni supreme leader alaf mnataka mjadili hoja zake??kwan iran hoja za khamenei zinajadiliwa??
 
Sikatai wazo lako nakubaliana nawewe nilichokua najiuliza kwanini watumie garama kubwa kubandika kubandika bango la zito mikoani wakati yeye hagombei uraisi? Mathalan Mbowe anagombea ubunge jimbo la hai then mabango yake yanabandikwa mwanza au sumbawanga kuna faida gani hapo?
Hakuna faida na ndio maana nikasema vyama vyote wanafanya makosa makubwa katika kuwanadi wagombea wao. Ni mfumo wa Kiumla unatumika kote nchini kiasi kwamba wakubwa wa kamati kuu, watatangazwa zaidi na kutembea nchi nzima kujiuza wakati wagombea wadogo kama wabunge wanamezwa hata katika maeneo yao. Bado vyama vinajiuza vyenyewe (watu wake) badala ya kugombea kuchukua nchi na hii inaonyesha wazi kuwa vyama n ahaswa vya Upinzani bado kabisa havijajiandaa kuongoza bali wanajitangaza.

Inavyotakiwa Kila jimbo linamtangaza zaidi mgombea wake (Mbunge na madiwani) mtaa kwa mtaa sio mgombea Urais kwa sababu rais anajitangaza live katika vyombo vya habari kwa kuzungumzia ILANI ya chama na SERA zake, wapi anataka nchi ielekee na mambo gani kayapa Kipaumbele na yatawekana vipi. Na rais atapata wasaa wa kuja kuwanadi wagombea wake ktk jimbo hilo. Kwa hiyo utaona kwamba wagombea wote wanatoa ahadi majukwaani tu wakinadiwa na rais na kutoa ahadi za kitaifa zisizo za jimboni kwake. Haya na hao Marais utasikia Mtu akisema atasambaza Umeme nchi nzima kwa siku 100!..Watu wanapiga makofi lakini wanashindwa kuuliza HOW! Je inawezekana? Hiyo Fedha itatoka wapi ikiwa pato la serikali halitoshelezi hata matumizi yake ya kawaida tu! Tuna walimu na watumishi wa serikali hadi leo wamelimbikizwa mishahara yao..

Lakini kama NEC wangekuwa na sheria ama utaratibu unaowataka wagombea wote wa Urais wapambane ktk midahalo Mitatu ama minne kisheria kabisa inayohusu 1. Huduma na USTAWI WA JAMII 2. UCHUMI 3. MIUNDOMBINU na Kadhalika. Wananchi wangeweza sana kuyapima maneno yao kutokana na hoja zitakazo andaliwa dhidi ya Hutuba walizokwihsha toa ama ahadi wanazosambaza. Pengine sisi bado wachanga lakini Midahalo nchi za wenzetu ni LAZIMA ukijitoa ndivyo unavyopoteza support ya wananchi. Haiwezekani sisi sote tunamjua Magufuli ama Lowassa kwa kujinadi tu, inatakiwa ajieleze atafanya nini na sheria (policies) gani zitatumika huku akibanwa na maswali!

Lakini wapi leo wananchi wanachagua viongozi wao kwa picha za mabango! sijui nani kapendeza zaidi ama rangi gani nzuri kwa sababu wananchi hawana historia kamili ya Mgombea zaidi ya kumtambua kuwa ni mtoto wa mzee fulani, kwao mtaa fulani, alisoma shule fulani, ni dini fulani, kabila fulani hizi ndizo sifa za mbombea!.. Mtapata kweli viongozi wazuri? sii ndio hadithi ile ile ya Ukweli ulofunikwa ungo!
 
Back
Top Bottom