Chama cha ACT Wazalendo kimetangaza kushtushwa na kuhuzunishwa na kifo cha aliyekuwa mwanachama wake, Seleman Bungara maarufu Bwege, kilichotokea ghafla asubuhi ya Machi 30, 2026, alipokuwa akipatiwa matibabu ya kusafisha figo jijini Dar es Salaam. Chama hicho pia kimeahidi kugharimia mazishi ya marehemu.
Taarifa iliyotolewa na kiongozi wa chama hicho, Dorothy Semu, imeeleza kuwa kifo cha Bungara ni pigo kubwa kwa familia yake, chama pamoja na wafuasi wa siasa za upinzani nchini. Semu amesema chama kimepokea taarifa hizo kwa mshtuko na huzuni kubwa, kikikumbusha kuwa Bungara alikuwa mwanachama wao kabla ya hivi karibuni kutangaza kuhama chama.
Aidha, Semu ametoa pole za dhati kwa mke wa marehemu, Mwanawetu Said Zarafi, ambaye pia ni mjumbe wa Bodi ya Wadhamini ya ACT Wazalendo, pamoja na familia, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huo
Soma pia TANZIA - Seleman Said Bungara (Bwege) afariki dunia