ACT Tanzania: Taarifa kwa umma

ACT Tanzania: Taarifa kwa umma

Tatizo la Kitila Mkumbo na Mwigamba ni njaa kali walizonazo,badala ya kufikiri kwa kutumia kichwa wao wanatumia tumbo kufikiri!
 
Makatibu wenezi wa nchi hii shida tupu. Sasa hiyo press rease ndiyo mdudu gani?
 
Nimeanza kuamini katika majina sasa, kama ilivyo kwa Hawa 'Ghasia', na Kitila 'Mkumbo' na sasa huyu bwana Thomas 'Matatizo'. Sidhani kama hawajakaribisha matatizo.
Ova
 
huu mkumbo wa kitilia mkumbo utamgarimu sana anafuata mkumbo wa vijana ambao wamejitoa ufahamu watamharibia sana aliyemwita mkumbo
 
ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY
ACT- TANZANIA.
MAKAO MAKUU OFSI YA UENEZI NA MAHUSIANO YA JAMII

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT-Tanzania, Kadawi Lucas Limbu, kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya ACT-Tanzania, ametengeua uteuzi wa Thomas Matatizo, kuwa mwanasheria wa chama kuanzia leo, tarehe 1 Januari 2015.

Mwenyekiti wa ACT-Taifa, amefuta uteuzi huo kwa kutumia ibara ya 37(w) (vi) ya Katiba ya ACT-Tanzania.

Bw.Thomas Matatizo ametenguliwa uteuzi wake kutokana na kujipa mamlaka ya kufanya kazi asizotumwa na chama, kushirikiana na wanaokidhoofisha chama na kudhihaki maamuzi halali ya kikao yaliyofanyika jana tarehe 31 Desemba 2015 lakini atabaki kuwa mwanachama na mjumbe wa kamati.

Katika kikao hicho, Kamati ya watu 11 iliyopewa mamlaka ya kuongoza chama kwa mujibu wa sheria Na. 5 ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, iliamua kumvua uwanachama, aliyekuwa Katibu Mkuu wa ACT, Samson Mwigamba, Mshauri wa chama Prof. Kitila Mkumbo na wanachama wengine kutenguliwa nafasi walizokabidhiwa kwa nia ya kukieneza chama lakini badala yake wanatumia nafasi hizo vibaya kukigawa na kukihujumu chama

Kwa taarifa hii, tunawaomba umma wa Watanzania kokote waliko, kutosikiliza kauli na vijineno vitakavyotolewa na Bw. Matatizo au Mwigamba. Kauli halali na thabiti ya chama itatolewa na mwenyekiti au yule ambaye amempa mamlaka.

Aidha chama chetu hakijampa mamlaka ya kuthibitisha wala kubatilisha maamuzi ya vikao mtu yeyote, bali sheria mama ya chama yaani katiba ndiyo inaelekeza mamlaka yenye uwezo wa kufanya hivyo.

Grayson Nyakarungu,
Katibu Mwenezi - ACT, Tanzania.
0755 023 503
Amefukuzwa tangu January 1, 2015 na kikao kilichokaa December 31, 2015😳. Hawa ndio viongozi wetu wa baadaye!
 
ringamoto njoo utoe ufafanuzi kwa hili suala

 
Last edited by a moderator:
Akina kitila na mwigamba wana upendo wa mshumaa kwa nyepesi. Nyepesi ni mjanja sana amempoteza mpaka prof kitila na sasa heshima ya prof kwa jamii ni zero. Nyepesi anazidi kunawiri na kubadilika badilika kama kinyonga. Mara aibukie Cuf mara aibuke cd za uzalendo. Mara awatumie akina msendo na vivian kupiga mpunga wa escrow. Mara apige mpunga toka magamba. Mara apige mpunga wa mashirika ya hifadhi za jamii. Kitila amekuwa na upendo kwa nyepesi kama vile nyepesi ni mke wake. Ni muda muafaka ss prof na mwl wangu wa kuachana na nyepesi
 
Tunamuunga mkono Mwenyekiti wa ACT kwa hatua kali alizochukua dhidi ya wahuni wa kisiasa.

Hawa ni wachumia tumbo.Ukiona mtu aliyeshindwa kukaa Chadema jua huyo ni mwizi na tapeli tu.

ACT mmeonyesha mfano mzuri sana.Tuko pamoja na nyie.
 
Hata hivyo, ACT ni chama cha wasaliti. Hata siku moja wasaliti hawawezi kuacha tabia za kusaliti. Nasubiria wengine pia wasaliti na kupigwa chini. Nyakarungu Upo???

Once a traitor always a traitor...!!!
 
Akina kitila na mwigamba wana upendo wa mshumaa kwa nyepesi. Nyepesi ni mjanja sana amempoteza mpaka prof kitila na sasa heshima ya prof kwa jamii ni zero. Nyepesi anazidi kunawiri na kubadilika badilika kama kinyonga. Mara aibukie Cuf mara aibuke cd za uzalendo. Mara awatumie akina msendo na vivian kupiga mpunga wa escrow. Mara apige mpunga toka magamba. Mara apige mpunga wa mashirika ya hifadhi za jamii. Kitila amekuwa na upendo kwa nyepesi kama vile nyepesi ni mke wake. Ni muda muafaka ss prof na mwl wangu wa kuachana na nyepesi

At least umekuja na argument tofauti segwanga ZZK ni mjanja sana na anajua kucheza na karata zake ameona sasa majeraha yake ya kisiasa yanapona na anaanza tena kukubalika CDM/UKAWA ameamua kukiua ACT na kuwatosa wale wote aliokuwa nao tangu mwanzo

Amesoma upepo na ameona yeye kung'ara nje ya CHADEMA ni ngumu kaamua kutengeneza mazingira ya kikiua chama na afanye patano na chama CHADEMA for his future political life
 
Last edited by a moderator:
Wamefukuzwa tar 31/12/2015, Bandiko limetoka 01/01/2015.

Haya ni maajabu.
 
Back
Top Bottom