ACT Tanzania: Taarifa kwa umma

ACT Tanzania: Taarifa kwa umma

ringamoto njoo utoe ufafanuzi kwa hili suala


Mkuu.... Nguruvi3..nilitaka kukuuita bahati....nzuri umefika karibu sana...Naukumbuka mjadala uliouongoza kule kwenye JUKWAA LA GT wachache tulikuelewa lkn kuna watu watoa Povu nyingi natamani utupie Link tujikumbueshe....!!
 
Last edited by a moderator:
ALLIANCE FOR CHANGE AND TRANSPARENCY
ACT- TANZANIA.
MAKAO MAKUU OFSI YA UENEZI NA MAHUSIANO YA JAMII

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha ACT-Tanzania, Kadawi Lucas Limbu, kwa mamlaka aliyopewa na Katiba ya ACT-Tanzania, ametengeua uteuzi wa Thomas Matatizo, kuwa mwanasheria wa chama kuanzia leo, tarehe 1 Januari 2015.

Mwenyekiti wa ACT-Taifa, amefuta uteuzi huo kwa kutumia ibara ya 37(w) (vi) ya Katiba ya ACT-Tanzania.

Bw.Thomas Matatizo ametenguliwa uteuzi wake kutokana na kujipa mamlaka ya kufanya kazi asizotumwa na chama, kushirikiana na wanaokidhoofisha chama na kudhihaki maamuzi halali ya kikao yaliyofanyika jana tarehe 31 Desemba 2015 lakini atabaki kuwa mwanachama na mjumbe wa kamati.

Katika kikao hicho, Kamati ya watu 11 iliyopewa mamlaka ya kuongoza chama kwa mujibu wa sheria Na. 5 ya vyama vya siasa ya mwaka 1992, iliamua kumvua uwanachama, aliyekuwa Katibu Mkuu wa ACT, Samson Mwigamba, Mshauri wa chama Prof. Kitila Mkumbo na wanachama wengine kutenguliwa nafasi walizokabidhiwa kwa nia ya kukieneza chama lakini badala yake wanatumia nafasi hizo vibaya kukigawa na kukihujumu chama

Kwa taarifa hii, tunawaomba umma wa Watanzania kokote waliko, kutosikiliza kauli na vijineno vitakavyotolewa na Bw. Matatizo au Mwigamba. Kauli halali na thabiti ya chama itatolewa na mwenyekiti au yule ambaye amempa mamlaka.

Aidha chama chetu hakijampa mamlaka ya kuthibitisha wala kubatilisha maamuzi ya vikao mtu yeyote, bali sheria mama ya chama yaani katiba ndiyo inaelekeza mamlaka yenye uwezo wa kufanya hivyo.

Grayson Nyakarungu,
Katibu Mwenezi - ACT, Tanzania.
0755 023 503

Huwa nasikia huyu kadawi limbu eti ni katibu pia wa ADC ni kweli wana bodi?
 
Nimeanza kuamini katika majina sasa, kama ilivyo kwa Hawa 'Ghasia', na Kitila 'Mkumbo' na sasa huyu bwana Thomas 'Matatizo'. Sidhani kama hawajakaribisha matatizo.
Ova

naona umeamua kudukua mambo
 
At least umekuja na argument tofauti segwanga ZZK ni mjanja sana na anajua kucheza na karata zake ameona sasa majeraha yake ya kisiasa yanapona na anaanza tena kukubalika CDM/UKAWA ameamua kukiua ACT na kuwatosa wale wote aliokuwa nao tangu mwanzo

Amesoma upepo na ameona yeye kung'ara nje ya CHADEMA ni ngumu kaamua kutengeneza mazingira ya kikiua chama na afanye patano na chama CHADEMA for his future political life

Tafadhali Zito rudi zako chadema
 
Last edited by a moderator:
Mkuu.... Nguruvi3..nilitaka kukuuita bahati....nzuri umefika karibu sana...Naukumbuka mjadala uliouongoza kule kwenye JUKWAA LA GT wachache tulikuelewa lkn kuna watu watoa Povu nyingi natamani utupie Link tujikumbueshe....!!
Ha ha ha ha!Nashukuru mimeshaitika wito nipo.
Kimantikitunataka tumsikilize msemaji Rangimoto ili tujadiliane vema. Tumetoa nafasi yayeye kutioa ufafanuzi kabla hatijamwaga mtama.

Kamahatafika kwa wakati mahususi tutaendelea na kazi

Kuna nyuzitatu kuhusu hawa waungwana kule mahali.
Na kamaulivyosema, wengi walituita wehu, wababishaji, vigagula n.k.

Hatukubadilishamwelekeo wala kujibu matusi.
Tulisimamakatika ukweli, na leo ukweli unatutetea wenyewe.

Ngojanipekue pekue, link zitakuwa updated soon


https://www.jamiiforums.com/great-t...a-cha-act-mpini-wa-ccm-kumaliza-upinzani.html

https://www.jamiiforums.com/great-thinkers/558343-duru-za-siasa-special-mgogoro-kambi-ya-upinzani-chadema.html

cc dolevaby
 
Last edited by a moderator:
Kuna kirusi kinasafishwa, hii ni baada ya failed plan A, then kinaletwa UKAWA, huku kwa kushirikiana na mmoja wa mhimili mkuu wa UKAWA, kazi imekwisha October,2015.
 
Zitto mjanja sana.......usikute anagonga zake Wiski na Mbowe kila jioni alafu mchana anawachora akina Kitila Mkumbo .........
 
Last edited by a moderator:
Mtangazaji wa Clouds kashindwa kuuliza maswali ya msingi Kitila leo.......mtu anasema mimi bado mwanachama kisheria....alipaswa kuulizwa sheria ipi wakati yeye ni mwanachama wa kawaida na ametimuliwa na kamati ya uongozi inatambulika na msajili? kwanini hawa watangazaji hawawezi kuuliza maswali ya msingi?
 
Hawa ACT hawana tofauti na wajomba zao Chadema.
 
Hawa ACT hawana tofauti na wajomba zao Chadema.

Hawa ndio walijiona wajuaji na mabingwa wa sayansi ya siasa.......aibu sana..... Zitto kawaacha yatima.....duh siasa hizi......
 
Last edited by a moderator:
Kuna kirusi kinasafishwa, hii ni baada ya failed plan A, then kinaletwa UKAWA, huku kwa kushirikiana na mmoja wa mhimili mkuu wa UKAWA, kazi imekwisha October,2015.

Afadhali umefikiri nje ya Box Mkuu....this is a planned thing...wameamua wenyewe kuiua hii ACT ili wa opt for another plan...You are right
 
Wamefukuzwa tar 31/12/2015, Bandiko limetoka 01/01/2015.

Haya ni maajabu.

walikuwa wanalinda taarifa isiibiwe. by the way Jamii forums haikuwa hewani kwa zaidi ya 36 hrs ingawa walitangaza 48hrs. usambaaji wa taarifa ulisimama lkn mie niliambiwa kufukuzwa kwa kitila na mwigamba 31.12.2014 na aliyenieleza alisema kwenye taarifa ya hbr itatangazwa lkn haikutangazwa.

kwa taarifa hii imekuwa ni kweli tena na mwanasheria wa chama kafukuzwa.
 
Wapo waliomtukana moja kwa moja Kubenea kule kwenye forum yake aliposema haya yaani kuhusu fukuto lililopo act na hatma yake, sasa kwa kuwa hao watu wapo pia kwenye forum hii wamuombe radhi Kubenea said.
 
Back
Top Bottom