ACT (Alliance for Change and Transparency) kuisambaratisha chadema

ACT (Alliance for Change and Transparency) kuisambaratisha chadema

Status
Not open for further replies.
Kwa hiyo hiki chama kimesajiliwa si kwa ajili ya kutaka kumkomboa Mtanzania masikini bali ni kwa ajili ya kuibomoa CDM? Poor them and you musukule.

Mkuu huko ndiko tunasema ni kuona mbele zaidi. Kwa hiyo kuundwa kwa ACT hiyo ni kuua CDM. Yale yale aliyosema yule Mnyama wa msituni juzi alipokuwa kabugia whisky za Ikulu alizofakamia za bure. Akajikuta anasema CDM haikufa 2013 lakini haivuki Pasaka. Oh! Poor Wasira. Kumbe alikuwa anamaanisha kwamba baada ya kumkingia kifua ZZK asifukuzwe uanachama akakosa ubunge basi ataingia kwa njia hii ya ACT?
Tanzania ya leo sio ile ya miaka ile. Waje tu, lakini tumechoka tunajua kuwa hilo ni tawi lingine tena la CCM. Limeletwa ili kutugawa tupunguze kura 2015 ili wapite. Nasema CDM hamtaiweza. CDM sio mtu, si Mh. Mbowe, Dr. Slaa wala yeyote. CDM ni Taasisi nayo inapendwa na watu, inaaminika na watu. Tutashinda tuu.
 
ACT ! hah hah hah hah!,

Chama cha kupambana Na Chadema!

Hiki ni CCM-C, Chama cha Masalia

Kwa kiingereza Anti-democratic Change in Tanzania-ACT
 
Sio kenge maji...huyu atakua kenge mfa maji...

wote mmekosea.angalieni jina lake linaonekana kuwa na herufi sita lakini ukichunguza utagundua ni tatu tu t.h.a,na yeye yuko hivyo hivyo,bichwa kuubwa limejaa mate,kamasi na machozi na chama chao cha Lumumba kiko hivyo pia,kina watu weengi lakini wote wamegawanyika makundi matatu tu,"wataalam wa michongo(mafisadi),wataalam wa meno(majangili,sijui na ule wa Ulimboka ni ujangili?) na wataalam wa milipuko(magaidi)!
 
La lini?au hili nlilonalo apa lina mis page?tatzo ht kwenye magazeti nao wamekua km vilaza wa JF wanaandika unverified story bila kuangalia implication zake...habari iliyokamilika lazma iwe na pande mbili bt za wa tz utaskia hadi tunaingia mitamboni simu yake ilikua haipatikani...ndivyo walivyofundishwa vyuoni?na hadi ukweli uje ufahamike the damage has already been done...na ss wa tz tumekua km bendera fata upepo kwa kufuata na kushabikia chochote kinacholetwa mbele yetu..na wana siasa wamelishalitambua hilo...full kutuyumbisha na kututoa kwenye mambo ya msingi na kutu keep bze na mambo ya hovyo hovyo tu....

Mkuu, labda nimsaidie Lizaboni habari ya chama hiki iliwahi kuripotiwa na Mtanzania. soma hapa chini.
[h=2] Chama kipya chaja [/h] Jumapili, Januari 12, 2014 07:46 Na Agatha Charles

*Chadaiwa kuundwa na waliofukuzwa upinzani
WAKATI fukuto la kufukuzwa uanachama kwenye Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) likiwa bado bichi, chama kipya cha siasa kimeanzishwa na watu wanaodaiwa kuwa ni muungano wa wanachama waliofukuzwa kutoka vyama vya upinzani nchini.

Taarifa zilizolifikia gazeti hili na kuthibitishwa na Ofisi ya Msajili wa vyama vya siasa nchini, zinakitaja chama hicho kuwa ni African Alliance for Change and Transparence (AACT) na kwamba mipango ya usajili wa muda wa chama hicho inadaiwa kuanza kuratibiwa kwa takribani mwezi mmoja sasa.

MTANZANIA Jumapili limedokezwa kuwa, tayari chama hicho kimekamilisha baadhi ya taratibu na kinatarajiwa kupewa usajili wa muda na Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa siku ya Jumanne, wiki ijayo.

Gazeti hili limedokezwa kuwa iwapo chama hicho kitapata usajili huo, upo uwezekano wa wanachama waliofukuzwa uanachama kutoka Chadema hivi karibuni kujiunga na chama hicho.

Wanasiasa wengine wanaotajwa ama kuwa nyuma ya kuanzishwa kwa chama hicho au wanatarajia kujiunga, ni wale waliofukuzwa kutoka CUF, nia ikiwa ni kuendeleza harakati zao za kisiasa.

Mmoja wa watu wanaounda chama hicho alilidokeza gazeti hili kuwa endapo chama hicho kitapata usajili baada ya hapo, taratibu na harakati za kuanza kukitangaza zitafanyika katika maeneo mbalimbali nchini.

Alisema pia wamepanga kuendesha siasa zenye upinzani, ikiwa ni pamoja na kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa na Uchaguzi Mkuu wa 2015 iwapo kitakuwa tayari kimejiimarisha.

MTANZANIA Jumapili limedokezwa kuwa mchakato wa kuanzisha chama kwa wanachama waliofukuzwa upinzani, ulianza kitambo, ukilenga nia yao ya kuhakikisha wanashiriki katika chaguzi hizo.

Hivi karibuni Kamati Kuu Chadema, iliwavua uanachama aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha, Samson Mwigamba na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk. Kitila Mkumbo, huku Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe, akikimbilia Mahakamani kuomba zuio la kutojadiliwa uanachama wake na kikao hicho.

Zitto, Dk. Kitila na Mwigamba walituhumiwa na uongozi wa juu wa Chadema kuandaa waraka wa siri wenye lengo la kufanya mabadiliko ya uongozi ndani ya chama, hali iliyoibua mgogoro mzito hadi kufikia uamuzi wa kuwavua uanachama baadhi yao.

Aidha taarifa nyingine ambazo MTANZANA Jumapili limezipata zinaeleza kuwa mbali na AACT, chama kingine kilichopata usajili wa muda hivi karibuni ni Chama cha Wananchi na Demokrasia (CHAWAD).

Gazeti hili lilimtafuta Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Francis Mutungi, kujua iwapo kuna chama kilichoanzishwa na wanachama waliofukuzwa upinzani, alisema hana taarifa hizo, ingawa kuna chama ambacho kimepata usajili wa muda na kingine kipo kwenye mchakato huo.

MTANZANIA Jumapili lilimtafuta Mwigamba ili kujua kama anafahamu kuhusu uanzishwaji wa chama hicho, ambapo alisema hivi sasa bado hawajakaa pamoja na wenzake kujadili suala la kuanzisha chama, kutokana na kila mmoja kuwa mbali.

"Tangu maamuzi ya Kamati Kuu hatujakutana, hii ni kwa kuwa tuko mbalimbali, mimi niko Arusha na nashauriana kwanza na familia yangu nijue nini cha kufanya," alisema Mwigamba.

Alisema hivi sasa anachokifahamu ni kwamba Dk. Mkumbo anarudi kwanza kwenye kazi yake ya awali na Zitto anasubiri uamuzi utakaotolewa dhidi ya uanachama wake.

Alipoulizwa Dk. Kitila kama ameshiriki na wenzake kuanzisha chama cha siasa, alishindwa kukataa wala kukubali, kwa kusema kuwa ukweli ama uongo wa habari hiyo utajulikana.

Alipotajiwa chama hicho na kwamba kinatarajia kupata usajili wa muda, alisema hafahamu hilo na hawezi kuzungumzia.

"Sina cha kuzungumza juu ya swali lako, kuwapo kwa chama kipya au la, nadhani ukweli utajiweka wazi nanyi mtabaini tu, hata hilo jina la chama kipya kuitwa AACT sijui," alisema Dk. Kitila.

Mpaka sasa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu nchini ni 23, ambavyo ni CCM, CUF, Chadema, UMD, NCCR-Mageuzi, NLD, UPDP, NRA, Tadea.

Vingine ni TLP, UDP, Demokrasia Makini, Chausta, DP, APPT-Maendeleo, Jahazi Asilia, Sau na AFP, UMD, FORD, CCK, ADC na Chaumma.



Chama kipya chaja
 
Hivi ule wimbo wa CCM Nambari One ulijua maana yake?

Don't talk about the past,let us talk about present and future. Tatzo lako unakariri badala ya kuelewa. CCM siyo tishio tena kwa CHADEMA and the vice versa is true.
 
wale waliokuwa wanasema kuwa ZITTO anatumika na CCM sasa wameumbuka

Umeumbuka wewe na magamba wenzio,, Zito nimsaliti tuu hafai ktk jamii y a mageuzi katuabisha vijana kuendekeza siasa za kizee.
 
Mkuu, mbona habari hii imeandikwa sana na Mtanzania? Au hujawahi kuisoma?

La lini?au hili nlilonalo apa lina mis page?tatzo ht kwenye magazeti nao wamekua km vilaza wa JF wanaandika unverified story bila kuangalia implication zake...habari iliyokamilika lazma iwe na pande mbili bt za wa tz utaskia hadi tunaingia mitamboni simu yake ilikua haipatikani...ndivyo walivyofundishwa vyuoni?na hadi ukweli uje ufahamike the damage has already been done...na ss wa tz tumekua km bendera fata upepo kwa kufuata na kushabikia chochote kinacholetwa mbele yetu..na wana siasa wamelishalitambua hilo...full kutuyumbisha na kututoa kwenye mambo ya msingi na kutu keep bze na mambo ya hovyo hovyo tu....
 
hawatamaliza mwaka bila kuvunjiana viti.Kama zitto atabahatika kuwa mwenyekiti wa chama chochote,tutashuhudia sarakasi maradufu ya zile za NCCR,kila kitu anajua yeye!
 
Chama kinaundwa ili kukisambaratisha chama kingine cha upinzani kisichokuwa na dola! Chama mamluki hicho!
 
Upuuzi mtupu,unakuja na pumba humu asubuhi hii hujua kama jf ndo mswaki wangu.....zito ana roho ya usalt at any where atakapokua lazima roho ifanye kazi yake.

Teh, teh! nimependa hiyo kauli yako et "JF NDO MSWAKI WANGU" Hapo umetugusa wengi. Sasa hapo mwisho ndo umemalizia na PUMBA yaan KA-UHARO. Eti "Zitto ni msaliti" prove it. Au kashakumegea mke?!!
 
wale waliokuwa wanasema kuwa ZITTO anatumika na CCM sasa wameumbuka

Kw hiyo zitto anatumika na nani??
Mnajidanganya sana nyie CCM.
Kwa akili zenu za panzi hicho chama cha Zitto ni maalum kwa kupambana na CDM au ni cha kumkomboa mtanzania toka kwa mkoloni mweusi??
 
Last edited by a moderator:
"Team Zitto" historia na vitabu inaonesha hakuna DOUBLE AGENT aliyewahi kuachwa na Dola akafaidi pesa za u-double agent bila kuwa assassinated. You're real for it!
Its a matter of time.
 
Chadema ni Mpango wa Allah kuwa chama tawala

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Chama kipya cha Alliance for Change and Transparency(ACT-TANZANIA) ambacho tayari kimeshapata usajili wa Muda kinatarajiwa kuwa ndio tishio la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutokana na kuundwa na Idadi kubwa ya vigogo wa chama hicho ambacho kwa sasa kimo ndani ya mgogoro mzito na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wao, ZITTO ZUBERI KABWE.

Hatua hiyo imeonesha dalili za wazi za kukimaliza CHADEMA na kwamba huenda chama hicho kikafika mwaka 2015 kikiwa mahututi kutokana na kuondokewa na wanachama wake wote wenye mvuto.

Taarifa za uhakika zimebainisha kuwa safu ya uongozi wa chama hicho itaundwa na idadi kubwa ya wanachama kutoka CHADEMA ambapo Samson Mwigamba anatajwa kuwa Katibu Mkuu, huku ZITTO Kabwe akipewa nafasi ya kuwa Mwenyekiti wakisaidiwa kwa karibu na wanachama mahiri na wasomi kutoka CHADEMA.

ZITTO anatarajiwa kujiunga na chama hicho mara baada ya kumalizika kwa bunge la Katiba ambapo kama atakuwa amevuliwa uanachama atakuwa tayari kujiunga na Chama hicho.

Mkakati wa Chama hicho ni kuhakikisha wanakuwa mbadala wa CHADEMA na kwamba dhamira yao kubwa ni kuhakikisha wanaendesha siasa zao kwa kutumia demokrasia ya kweli na hawako tayari kukifanya chama hicho kuwa cha watu wachache.

Source: MTANZANIA

NB. Hii haijaandikwa ndani ya Gazeti hili la mtanzania, Nimeipata kwa juhudi zangu binafsi. Wengine wanaotarajia kujiunga na chama hiki ni Pamoja na Prof. Mweisiga Baregu(CHADEMA), Prof. Safari(CHADEMA), Hamad Rashid(CUF), KAFURIRA(NCCR-MAGEUZI), MABERE MARANDO(CHADEMA) na FILIKU NJOMBE kutoka chama Tawala.

chama cha wasaliti,hovyo kabisa
 
Hao wasomi ni akina nani?

Bado vyama vinavyoanzishwa kwa itikadi ya "Hasira" na sera za "Kukomoa" vipo?

Maana hakuna sera wala itikadi iliyowaunganisha.

Dogo sumu vipi kumbe upo?!

Zitto ni mzito kwelikweli kwenu chadema,kazi uliyopewa nasikia umeshindwa na sasa hali ni tete kwako?!

Bora huyu zitto ungemmaliza tu kwa sumu wakati ule ulipokuwa unamsakua hadi baa,saivi ni ngumu sana!!Tehe tehe tehe tehe tehe tehe tehe tehe!
 
Acha upimbi,kwa hiyo unakataa? J.Mbilinyi,D.Silinde na Msigwa,hao je,wanatoka Pwani? Jitambue wewe K.

bado ujanitajia chama kp chenye idadi kubwa ya wabunge kutoka huko na kama ni magamba sasa kvp useme makamanda wanakubalika huko? Kaka hata picha umeshindwa kuona?
NB;kaka eeh pole ka umekushnda usitaarabu ndo mpaka unitusi...?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom