ACT (Alliance for Change and Transparency) kuisambaratisha chadema

Status
Not open for further replies.

thatha

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2011
Posts
15,340
Reaction score
1,573
Chama kipya cha Alliance for Change and Transparency(ACT-TANZANIA) ambacho tayari kimeshapata usajili wa Muda kinatarajiwa kuwa ndio tishio la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutokana na kuundwa na Idadi kubwa ya vigogo wa chama hicho ambacho kwa sasa kimo ndani ya mgogoro mzito na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wao, ZITTO ZUBERI KABWE.

Hatua hiyo imeonesha dalili za wazi za kukimaliza CHADEMA na kwamba huenda chama hicho kikafika mwaka 2015 kikiwa mahututi kutokana na kuondokewa na wanachama wake wote wenye mvuto.

Taarifa za uhakika zimebainisha kuwa safu ya uongozi wa chama hicho itaundwa na idadi kubwa ya wanachama kutoka CHADEMA ambapo Samson Mwigamba anatajwa kuwa Katibu Mkuu, huku ZITTO Kabwe akipewa nafasi ya kuwa Mwenyekiti wakisaidiwa kwa karibu na wanachama mahiri na wasomi kutoka CHADEMA.

ZITTO anatarajiwa kujiunga na chama hicho mara baada ya kumalizika kwa bunge la Katiba ambapo kama atakuwa amevuliwa uanachama atakuwa tayari kujiunga na Chama hicho.

Mkakati wa Chama hicho ni kuhakikisha wanakuwa mbadala wa CHADEMA na kwamba dhamira yao kubwa ni kuhakikisha wanaendesha siasa zao kwa kutumia demokrasia ya kweli na hawako tayari kukifanya chama hicho kuwa cha watu wachache.

Source: MTANZANIA

NB. Hii haijaandikwa ndani ya Gazeti hili la mtanzania, Nimeipata kwa juhudi zangu binafsi. Wengine wanaotarajia kujiunga na chama hiki ni Pamoja na Prof. Mweisiga Baregu(CHADEMA), Prof. Safari(CHADEMA), Hamad Rashid(CUF), KAFURIRA(NCCR-MAGEUZI), MABERE MARANDO(CHADEMA) na FILIKU NJOMBE kutoka chama Tawala.
 
Waunde tu kwani mbinu za CCM zimekwama kuimaliza CHADEMA na sasa wanaona bora kufadhili uanzishwaji wa ACT-Tanzania. CHADEMA ni chama imara kuliko vyama vyote vya siasa vikiongozwa na chama chakavu CCM.
 
Ningumu watu kutema ubunge eti wakaimalishe chama kipya!!!,hao watabanana kwenye vyama vyao hadi mwisho,posho kwanza!!!
 
Kwa hiyo hiki chama kimesajiliwa si kwa ajili ya kutaka kumkomboa Mtanzania masikini bali ni kwa ajili ya kuibomoa CDM? Poor them and you musukule.
Ndio maana kinapewa promo na Thatha (gamba) ikumbukwe wote waliotajwa ni wale ambao husemwa wanatumwa na ccem kuhujumu vyama na habari haijapelekwa bado kwenye gazeti lao ila itapelekwa lkn mwandaaji wa propaganda hizo mkuu thatha, akawashwa na kiherehere akavujisha jf. Nimeipenda ila itashindwa kwani ADC pamoja na kufananisha bendera wako wapi vile???
 
Upuuzi mtupu,unakuja na pumba humu asubuhi hii hujua kama jf ndo mswaki wangu.....zito ana roho ya usalt at any where atakapokua lazima roho ifanye kazi yake.
 
Kama ACT-Tanzania inaundwa kwa lengo la kuisambaratisha CHADEMA huku kikiongozwa na Mwenyekiti Zitto na Katibu mkuu Mwigamba, inanifanya niamini kuwa pesa zilizotolewa ili kuisambaratisha CHADEMA kwa kutumia mawakala wa CCM wakiongozwa na Zitto ndizo zitakazo tumika kusaidia mawakala hao wakiwa nje ya CHADEMA.

Kama walipokuwa ndani wameshindwa, je wakiwa nje wataweza kuisambaratisha CHADEMA?

Poor on you Team Zitto.
 
Kwa hiyo hiki chama kimesajiliwa si kwa ajili ya kutaka kumkomboa Mtanzania masikini bali ni kwa ajili ya kuibomoa CDM? Poor them and you musukule.

Inashangaza kweli.
yaani Jitihada zote ni kuiharibu cdm, Ni kichaa tu anayeweza kufanya vitu kama hivo,
Tanzania tuna Vyama Viwili tu,mbavyo ni Chadema na Ccm vingine ni Magumashi,
Chadema moto wa kuotea mbali yaani mpaka kuanzisha chAma kingine si mchezo.
 
kila rangi tutaiona mwaka huu,hicho kitakuwa ni chama cha wasaliti na mapandikizi na hakiwezi kudumu! CDM NI MPANGO WA MUNGU.
 
Waunde tu kwani mbinu za CCM zimekwama kuimaliza CHADEMA na sasa wanaona bora kufadhili uanzishwaji wa ACT-Tanzania. CHADEMA ni chama imara kuliko vyama vyote vya siasa vikiongozwa na chama chakavu CCM.

Tusubiri tuone uimara wa CHADEMA, kwa sasa hakuna kiongozi wa CDM anaweza kusimama na mke wake jukwaani na kusema huyu ndiyo mke wangu, maana wengine watajitokeza huku Mshumbuzi, kule Rose kamili, hapa Joyce Mukya pale sijui nani yule nimemsahau jina. Uimara wa siasa sasa zero kabisaaaa.
 
Chama kipya cha Alliance for Change and Transparency(ACT-TANZANIA) ambacho tayari kimeshapata usajili wa Muda kinatarajiwa kuwa ndio tishio la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutokana na kuundwa na Idadi kubwa ya vigogo wa chama hicho ambacho kwa sasa kimo ndani ya mgogoro mzito na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wao, ZITTO ZUBERI KABWE.

Hatua hiyo imeonesha dalili za wazi za kukimaliza CHADEMA na kwamba huenda chama hicho kikafika mwaka 2015 kikiwa mahututi kutokana na kuondokewa na wanachama wake wote wenye mvuto.

Taarifa za uhakika zimebainisha kuwa safu ya uongozi wa chama hicho itaundwa na idadi kubwa ya wanachama kutoka CHADEMA ambapo Samson Mwigamba anatajwa kuwa Katibu Mkuu, huku ZITTO Kabwe akipewa nafasi ya kuwa Mwenyekiti wakisaidiwa kwa karibu na wanachama mahiri na wasomi kutoka CHADEMA.

ZITTO anatarajiwa kujiunga na chama hicho mara baada ya kumalizika kwa bunge la Katiba ambapo kama atakuwa amevuliwa uanachama atakuwa tayari kujiunga na Chama hicho.

Mkakati wa Chama hicho ni kuhakikisha wanakuwa mbadala wa CHADEMA na kwamba dhamira yao kubwa ni kuhakikisha wanaendesha siasa zao kwa kutumia demokrasia ya kweli na hawako tayari kukifanya chama hicho kuwa cha watu wachache.

Source: MTANZANIA

NB. Hii haijaandikwa ndani ya Gazeti hili la mtanzania, Nimeipata kwa juhudi zangu binafsi. Wengine wanaotarajia kujiunga na chama hiki ni Pamoja na Prof. Mweisiga Baregu(CHADEMA), Prof. Safari(CHADEMA), Hamad Rashid(CUF), KAFURIRA(NCCR-MAGEUZI), MABERE MARANDO(CHADEMA) na FILIKU NJOMBE kutoka chama Tawala.

hata wakijiunga zitto atawasaliti tu. Zitto ni muhuni na msaliti kwa asili.
 
Upuuzi mtupu,unakuja na pumba humu asubuhi hii hujua kama jf ndo mswaki wangu.....zito ana roho ya usalt at any where atakapokua lazima roho ifanye kazi yake.

waambie Mtanzania siyo mimi bro.
 
Source: Gazeti la Mtanzania linalomilikiwa na CCM...................... Endelea kuamini hivyo hivyo
 
THIS IS AWKWARD, NIMEIPENDA HII HABARI, SASA TWAWEZA KUWAFAHAMU ZITO, MWIGAMBA KWA RANGI ZAO ZA KWELI, NI WAZI MAHAMUZI YA CHADEMA KUWATIMUA HAWA WASALITI YALIKUWA SAHIHI,

NA HATA WAFUASI WAO NI WAZ WATAKUA WAKIUNGA MKONO SI UKOMBOZ WA MTANZANIA BALi KUNDI LINALOPINGANA NA UKOMBOZ WETU.
KILA LA KHERI WAFUASI WATARAJIWA WA ACT
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom