ngungwangungwa
JF-Expert Member
- Jul 23, 2013
- 649
- 587
Km itatokea hata professor mwesiga baregu,prof.safari na mabere malando nao wakajiunga,ntakuwa nimethibitisha pasi na shaka kuwa nchi hii haina wasomi bali wachumia tumbo.
Umeumbuka wewe na magamba wenzio,, Zito nimsaliti tuu hafai ktk jamii y a mageuzi katuabisha vijana kuendekeza siasa za kizee.
Chama kipya cha Alliance for Change and Transparency(ACT-TANZANIA) ambacho tayari kimeshapata usajili wa Muda kinatarajiwa kuwa ndio tishio la Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) kutokana na kuundwa na Idadi kubwa ya vigogo wa chama hicho ambacho kwa sasa kimo ndani ya mgogoro mzito na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wao, ZITTO ZUBERI KABWE.
Hatua hiyo imeonesha dalili za wazi za kukimaliza CHADEMA na kwamba huenda chama hicho kikafika mwaka 2015 kikiwa mahututi kutokana na kuondokewa na wanachama wake wote wenye mvuto.
Taarifa za uhakika zimebainisha kuwa safu ya uongozi wa chama hicho itaundwa na idadi kubwa ya wanachama kutoka CHADEMA ambapo Samson Mwigamba anatajwa kuwa Katibu Mkuu, huku ZITTO Kabwe akipewa nafasi ya kuwa Mwenyekiti wakisaidiwa kwa karibu na wanachama mahiri na wasomi kutoka CHADEMA.
ZITTO anatarajiwa kujiunga na chama hicho mara baada ya kumalizika kwa bunge la Katiba ambapo kama atakuwa amevuliwa uanachama atakuwa tayari kujiunga na Chama hicho.
Mkakati wa Chama hicho ni kuhakikisha wanakuwa mbadala wa CHADEMA na kwamba dhamira yao kubwa ni kuhakikisha wanaendesha siasa zao kwa kutumia demokrasia ya kweli na hawako tayari kukifanya chama hicho kuwa cha watu wachache.
Source: MTANZANIA
NB. Hii haijaandikwa ndani ya Gazeti hili la mtanzania, Nimeipata kwa juhudi zangu binafsi. Wengine wanaotarajia kujiunga na chama hiki ni Pamoja na Prof. Mweisiga Baregu(CHADEMA), Prof. Safari(CHADEMA), Hamad Rashid(CUF), KAFURIRA(NCCR-MAGEUZI), MABERE MARANDO(CHADEMA) na FILIKU NJOMBE kutoka chama Tawala.
Hata CHAUMA kilikua na malengo haya
kweli cdm inainyma ccm usingzi
Alliance for Cowards and Traitors