Acheni kujichubua

Kwani wanaelewaga sasa
Waonewe huruma, mkorogo ni kama madawa ya kulevya, kuingia rahisi kutoka ni mtiti

Kuna siku nimeenda dukani nikamwambia mwenye duka nataka lotion ya kunifanya niglow....Mimi ni maji ya kunde...hapo Kuna lotion inatangazwa na dada wa mjini nimetumia naona inanitoa sugu

Basi nikapewa face cream, napaka kweli nikaanza kung'aa.....miezi 6 naona naanza kuwa mwekundu usoni, mara mishipa ya damu inaonekana🤣🤣🤣 ilibidi niache, Ile nimeacha nikawa mweusiii kama nimepigwa bomu.....Kwa kuwa nilikuwa likizo nikakomaa sitoki nje, mwendo wa scrub na mafuta ya Nazi.....sasa ngozi imerudi normal

Sio kazi rahisi kuacha hizo cream, ni uraibu.
 
weka picha
 
Hapa mnaponda mikorogo, halafu mki log out mnawapigia simu wauza mikorogo wawaletee..!!! Mnaojichubua mchubue na matraako jamni, mdada sura imeshine kibinda nyuma cheusi tii km tumbili wale wanaoomba chakula mlima Kitonga
Wengine tushakimbia mrembo wakati wa chuma mboga!
Kule mkorogo haufiki! Maana kote kweupe ila pale panapotenganisha makalio peusi kama MKAA!
Panatisha!
 
Wadada wengi wanajichibua ni kwasababau hawajiamini. Kwanini usiiringie rangi yako ulopewa na Mungu tangu kuzaliwa. Halafu nani aliwaambia weupe ndo uzuri.Mwisho wa siku kama ni kupendwa kila mmoja anataste yake hapa duniani. Kuna wanaopenda wanawake weusi na kuna wanaopenda wanawake weupe. Kaa na rangi yako jipende ulivo.
 
Watu wanang'aa Kwa mafuta ya Nazi ya 2,000 ndio iwe 20,000
me nazungumzia wanaojichubua mkuu, mwenyewe mbona niko na vaseline yangu for men sina mambo mengi 😃😃😃... Hao wanaotaka kubadili rangi na wanapaka vya bei rahisi lazima wewe na rangi mbili mbili
 
Uko sahihi kbsa ,ni kama uraibu

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
Sahihi kbsa

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
 
 

Attachments

  • Screenshot_20240116-180956.jpg
    177.3 KB · Views: 15
  • Screenshot_20240116-180947.jpg
    163.3 KB · Views: 13
So sad
Ila wapunguze kiukweli
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…