Acha uogaaa...

Acha uogaaa...

Ndibalema

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2008
Posts
10,955
Reaction score
4,664
Kajamaa kafupi kembamba na jitu la miraba minne wamekutana kwenye lifti kwenda gorofa ya kumi na sita. Wako wawili tu. Kajamaa kafupi kakawa kanaliangalia lile jitu kwa muda, bonge akaongea: Kilo mia na 20, urefu futi 7, maeneo fulani inchi 15, Gwaka Nyambawa.

Kajamaa kafupi ghafla kaanguka kakazimia. Bonge akamnyanyua akamuuliza kwa sauti ya upole: vipi ndugu yangu? Una tatizo gani?

Jamaa akaji...bu: Kwani we umeniambiaje?
Bonge akajibu: Niliona unaniangalia sana nikaone nikupe jibu ambalo kila mtu huwa analitaka akiwa ananiangalia sana. Nina kilo mia na 20, urefu futi 7, maeneo fulani inchi 15, jina langu naitwa Gwaka Nyambawa.

Jamaa akajibu: Duh! Basi sawa, hapo kwenye jina mimi nikajua umesema "Geuka Nyuma"
 
Kwa maelezo hayo lazima kajamaa kaanguke tu. Imetulia mkuu!
 
Back
Top Bottom