Account zangu za CRDB hazijatumika tangu Desemba 2021

Melki Wamatukio

JF-Expert Member
May 3, 2022
5,854
10,110
Habari za muda huu wakuu,

Nina Account 2 za CRDB, ya kwanza niliifungua mwaka 2020 kwa kitambulisho changu cha utaifa, na ya pili niliifungua 2021 kwa kitambulisho changu cha chuo kikuu muda huo nilikuwa namalizia mwaka wa tatu wa masomo

Baada ya kumaliza chuo maisha yalinitwanga haswa kiasi kwamba nikakosa saving amount ya kudumbukiza kwenye tu account twangu. Hivyo nikabeba kadi zangu za benki na kuzitupa ndani ya begi, 2021

Mpaka sasa ni miaka mitatu hivi sijatumia akaunti hizo. Nahisi tayari zimekwisha uwawa, hivi utaratibu wa kuzifufua uko vipi? Je kuna kiwango cha pesa kinachotakiwa katika ufufuaji huo? Na je process zake ni changamano kiasi cha kupoteza muda mwingi ili nisisumbuke nifungue tu NMB?

Pia kadi zenyewe zina expire November. Utaratibu wa kuzirenew uko vipi?

Ni hayo tu wakuu...
 
Mkuu kwani hapo benki kunahitaji nauli,kwa kuwa watanzania ni watu rahimu sana weka namba upewe mchango wa nauli!
 
Simple, wapigie simu hao crdb uwaulize kama account yako ipo active.
Mbona mnashindwa kuzitumia social networks kwa uzuri, ishu simple kama hiyo ni ajabu kwa graduate kuomba msaada kama huo.
 
Mkuu kwani hapo benki kunahitaji nauli,kwa kuwa watanzania ni watu rahimu sana weka namba upewe mchango wa nauli!
Hapana mkuu, maboss wa kihindi ni nuksi sana mkuu, yaani ni mara mia anione nimeshika simu hivi ilihali niko kazini kuliko nisiwepo kabisa. Kazi yake haina kupumzika, labda Jumapili napo ni kuanzia saa 6 mchana
 
Ukideposit tu hela hata kama zimekuwa dormant zinafufuka, sema ni muhimu uende tawi lolote la crdb kwa kuwa kuna kipindi walikuwa wanahakiki taarifa za wateja.
 
Hapana mkuu, maboss wa kihindi ni nuksi sana mkuu, yaani ni mara mia anione nimeshika simu hivi ilihali niko kazini kuliko nisiwepo kabisa. Kazi yake haina kupumzika, labda Jumapili napo ni kuanzia saa 6 mchana
Pole sana kama nimekukwaza mkuu nilijua ni watoto wa 2000 hata kijiko asipokiona kwao wanapandisha uzi jf!
 
Back
Top Bottom