CRDB Bank hili suala halijakaa sawa

Slim

Senior Member
Nov 12, 2008
103
119
Habari Wakuu!

Leo katika harakati za kuweka mambo sawa nilienda Bank CRDB Bank main customer service desk pale nikakuta kuna mteja anataka kufanya account activation coz ilikuwa dormant sasa akawa hana kitambulisho ila ana copy tu ya kitambulisho cha Taifa.

Ikabidi wale wadada wamwambie ni lazima wafanye verification ya hiyo namba yake ya NIDA kama ni yeye kweli.

Sasa kilichonishangaza ilibidi jamaa aanze kuulizwa maswali pale mbele za watu na kujibu hayo mswali ambayo mtoa huduma alikuwa anaamuliza kwa sauti na watu wanasikia hizo details za huyo jamaa kwa mfano "jina la kati la mama yako? jamaa anataja.. Shule ya msingi uliosoma inaitwaje? ...

Maswali mengi kama hayo basi jamaa alikuwa anakosea mara kwa mara na yule mtoa huduma alipoteza muda mrefu sana kumhudumia mteja mmoja mpaka alipopatia maswali yote.

Kwa mtazamo wangu mimi binafsi naona utaratibu ule sio mzuri kabisa kumuuliza mtu his personal details mbele za watu na pia kupoteza muda mrefu kuhudumia mteja mmoja labda ungetengenezwa utaratibu mwingine mzuri wakuhudumia wateja kama hao ili kuokoa muda na usiri wa taarifa binafsi za wateja.

Utaratibu wa kuchukua namba ni mzuri lakini watu bado wanarundikana pale main customer service desk.

Nawakilisha.
 
Najiuliza kuna bank zinataka hadi leo ukitaka kufungua account au ku activate account hadi uende ofisni kwao. Nilitegemea aya mtu angeweza kufanya kwenye simu yake
 
Walichofanya sio sawa, ila mteja pia hasingekubali style wanayotumia kumuhoji maswali. Ingawa pia mara kadhaa customer care ya wanawake ni changamoto
 
Serikali ndio wapuuzi, kwanini wasitoe hard copy ya vitambulisho vyetu, hadi bank tunakutana na usumbufu kama huo
 
Serikali ndio wapuuzi, kwanini wasitoe hard copy ya vitambulisho vyetu, hadi bank kutanutana na usumbufu kama huo

Siyo bank tu
Kuna Office ya serikali nimeshindwa kuhudumiwa sababu Sina hard copy..

Kwani zile namba zinaingiliana?
 
Siyo bank tu
Kuna Office ya serikali nimeshindwa kuhudumiwa sababu Sina hard copy..

Kwani zile namba zinaingiliana?
Namba pekee sometimes haitoshi, inahitajika Copy ya kitambulisho chenyewe chenye Picha.
 
Kwa mtazamo wangu mimi binafsi naona utaratibu ule sio mzuri kabisa kumuuliza mtu his personal details mbele za watu na pia kupoteza muda mrefu kuhudumia mteja mmoja labda ungetengenezwa utaratibu mwingine mzuri wakuhudumia wateja kama hao ili kuokoa muda na usiri wa taarifa binafsi za wateja.
Ina maana CRDB pamoja na ukubwa wote wameshindwa kutengeneza vijumba kama vile vya kuungamia makanisani ili vitumike kwa kazi hiyo!!!!!!!
 
Habari Wakuu!

Leo katika harakati za kuweka mambo sawa nilienda Bank CRDB Bank main customer service desk pale nikakuta kuna mteja anataka kufanya account activation coz ilikuwa dormant sasa akawa hana kitambulisho ila ana copy tu ya kitambulisho cha Taifa...
Ni kama katika baadhi ya hospitali manesi au madaktari hawana weledi au hekima ya kumhoji mgonjwa.

Wanauliza maswali binafsi kwa sauti mbele za watu...umewahi kuugua ugonjwa flani? Kabila lako? n.k

Wajinga kabisa
 
Back
Top Bottom