Account za Benki za Mange Kimambi zazuiliwa

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Aug 2, 2021
1,026
1,622
Anaandika Mange Kimambi kupitia ukurasa wake wa Instagram

1649167736934.png



PART 1. Chama changu pendwa, chama bora hakijapata tokea tangu dunia iumbwe. Naomba mnisaidie kwenye hii vita polisi waliyonayo na mimi.

Nimeona niwaombe msaada huku kwa social media maana sina namba zenu za kuwapata, otherwise ningewatumia message mmoja mmoja.

Kwanza kabisa kabla sijawaomba misaada viongozi wangu naomba kwanza niwaadithie watanzania kilichotokea siku mdogo wangu amepewa dhamana.

Jamani polisi walitaka kucheza mchezo mbaya sana ila Mungu akawaumbua. Sasa si mimi nilimlilia mama kuwa mdogo wangu na wenzie wawili wanashikiliwa na polisi bila dhamana kinyume na sheria.

Basi wakaona watoe lawama wafate sheria kwa kumfikisha mdogo wangu mahakamani ila mpango ulikuwa wampeleke Segerea sio kupewa dhamana.

Sasa wamakonde (ndugu zangu walikuwa wanashinda pale polisi na barua za dhamana ya polisi au Mahakamani walikuwa nazo wanatembea nazo.

Basi siku ya tukio kama Mungu tu ndugu zangu ile wanaingia ndani central kupeleka chakula ndo wanakutana na polisi wanamwingiza mdogo wangu kwenye unmarked car wakawauliza polisi mnampeleka wapi?

Polisi wakasema tunaenda nae kwenye ofisi zao kuna ushahidi tunaenda kuchukua tunarudi nae sasa hivi. So wamakonde wakaendelea kukaa central. We mara mke wa mdogo wangu anapigiwa simu na rafiki yake mdogo wangu anamwambia wewe mbona Allen yupo Kisutu hana mwanasheria wala nini? Anakaribia kupandishwa kizimbani?

OMG ndo mkewe na familia kuchanganyikiwa unaambiwa walipanda bolt bila kurequest, huku wanampigia simu mwanasheria . Bahati vizuri mwanasheria ofisi yake ni 10 mins from Kisutu. Mwanasheria akaacha gari yake akapanda boda boda. Tai kaivalia Kisutu pale nje. Yani lawyer na familia wanafika Allen ndo anapandishwa kizimbani. Yani polisi hawajaamini, mpelelezi wa kesi anaitwa Agatha hajaamini macho yake anauliza hawa nani kawastua?

Basi walivyoona mpango wao umefeli na mdogo wangu kaachiwa na mahakama ikabidi wawaachie na Rehema na mwenzie maana wale walikuwa wanawashikilia kama danganya toto tu. Shida yao ilikuwa mdogo wangu tu.

Yani ni hivi kama sio kudra za mwenyezi Mungu mdogo wangu angekaa Segerea mpaka kesi yake iitwe tena.

Hivi kweli hili ndo jeshi la polisi tulilonalo Tanzania?? 😭😭

PART 2. Mwanzoni nilikuwa naamini ni Sirro tu ndo ananifanyizia ila Sio Sirro peke yake, kumbe nimenyea kambi central nzima pale . Sasa hamuwezi amini kumbe baba yake Nabii Shila ndo ZCO? Yes ZCO ni baba yake mzazi Nabii na mama yake mzazi Nabii Shila ni afande pia pale pale Central.

Posti zote za mtoto wao nilizokuwa naandika wazazi walikuwa wanasoma wanasubiri tu nibonyeze kidude waninyooshe, uwiiii 😭😭😭😭. Ila sasa mtoto wao anatapeli watu kupitia dini watu tusiseme?

Tumwogope mtoto wao ambae ni nabii feki kisa baba ZCO na mama ni Afande? Tutasema tu! Na hata kesho App ikisharudi hewani Nabii Shila tutaandika tu utapeli wake anaofanyia wananchi.
.
.
Na Sirro ule mchakamchaka niliompaka 2017-2018 bado hajausahau hadi leo. So hapo jumlisha IGP anataka kunila nyama, ZCO anataka kunila nyama, basi balaa tupu.

Basi story haijaishia hapo, sasa ile hasira ya kushindwa kumfikisha mdogo wangu Segerea mnajua wamefanyaje jana? Wame freeze bank account zangu zoote.

Hii vita sasa hivi wala haihusiani tena an clip ya Professor Jay hii ni vendetta tu. Maana mpaka kufreeze bank account za mtu ni kupitiliza mipaka

Viongozi wangu pendwa wa chama pendwa tafadhali naomba muangalie huu uonevu wa polisi. Nilikuwa nausikia tu kwa watu ila sasa nimeuona kwa macho yangu mwenyewe. Naomba haki itendekeee.

Nchi ina wauwaji, majambazi, huyo Sirro na huyo ZCO wana kesi kubwa hadi leo hawaja solve kama Lissu kupigwa risasi eneo la bunge, au Mo Dewji kutekwa ila wana freeze bank account sababu ya video clip? Hapo ndo unapojua Issue sio video clip, Issue ni kwamba walikuwa wanasubiria niwape sababu wazae na mimi.

Nime attach na email kutoka CRDB inayoniarifu kuwa polisi wame freeze account yangu ya bank kwa wiki 2.
 
Back
Top Bottom