Access Bank -vs- BRELA

yani ukiwa auna rushwa mafaili yanapoteaga kimuujiza ila ukitoa rushwa tu hapo hapo linaonekana yani cjui kinatokeaga nn hapa ata kama unaliona hapo mezani ukamwonyesha samani si hilo hapo anakwambia siyo lako lakwako silioni ukimpa rushwa macho yanafunguka

yani no wonder bibilia inasema rushwa upofusha macho unakuwa uone kabisa angalia ata matrafiki magari mabovu kabisa yani uitaji ata kukagua lakini awayaoni why rushwa
 
Watanzania m-badilike sasa, mapambano dhidi ya rushwa sio ya PCCB peke yake ni ya watanzania wote kama kweli tuna nia ya kuiondoa hii Rushwa sio kulaumu tu kwamba serikali haifanyi chochote. sasa hii taarifa/thread yako ulipaswa kuipeleka PCCB ishughulikiwe, sio kubaki kulaumu tu.
 
Hili mi sikubaliani nalo, Nina account ya kampuni BOA, EXIM na CRDB sijawahi Sikia mambo ya Brela, nilipomaliza tu taratibu za documents account ilifunguliwa Papo hapo bila shida, hivi vitakuwa vibank Mahabad $&@&$$$&&&


QUOTE=Cotan;850007]Nimesikitishwa sana na kitendo nilichofanyiwa na hawa jamaa wa Access Bank.
Mnanamo mwezi wa kumi na moja mwaka jana nilienda Access Bank kwaajili ya kufungua Account ya Kampuni, nilipofika niliwaona wahusika na wakanipatia taratibu zao za kufuata kwaajili ya kukamilisha zoezi la kufungua Account.

Nami niliwaletea nyaraka zote walizozihitaji ktk mchakato mzima.Baada ya kukabidhi nyaraka hizo niliambiwa nisubiri baada ya siku tatu nitajulishwa.Baada ya siku tatu nilienda nikaambiwa kuwa nisubiri kidogo kwani nyaraka zangu zimepelekwa BRELA kwaajili ya uhakiki km kweli kampuni imesajiriwa.Jamaa akaniambia kuwa nitapigiwa simu wakati wowote pindi mambo yakiwa tayari.

Jambo la ajabu nimesubiri kwa muda mrefu bila majibu duh nikaamua kwenda Internataional Commercial Bank kuanza zoezi jipya la kufungua Account, nimetumia km wiki mbili hivi Account ikawa imefunguliwa.Sasa nikabaki na maswali lukuki iweje hawa watumie wiki mbili tu kufungua Account ili hali Access Bank sasa ni miezi mitano bila jibu lolote!?.

Ndipo nikaamua kurudi tena Access Bank, mhusika nikamuliza kwanini zoezi hili limechukua mda mrefu namna hii?, ili hali ICB wametumia wiki mbili tu?.jamaa akaniambia kuwa tatizo ni BRELA kwani mafairi yote yamekwisha pelekwa huko, lakini kila wakifuatiliwa wanaambiwa mafairi hayaonekani, wakati mwingine wanaabiwa njoo kesho bado tunatafuta mafairi.Pia akanitanabahisha kuwa ktk kila Bank kunatofauti wa kushughurika mambo eti kuna baadhi ya Bank wanatoa kitu kidogo kwa jamaa wa BRELA ili kurahisisha mambo.duh TZ kila kitu ni rushwa hata kufungua Account mnaomba rushwa.Duh kumbe ndo maana watu wa ICB waniliambia nitoe Tsh 15000/= ya kurahisisha mambo kule BRELA. duh watu wa BRELA acheni mambo hayo jamani munaturudisha nyuma kimaendeleo.[/QUOTE]
 
Back
Top Bottom