Access Bank -vs- BRELA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Access Bank -vs- BRELA

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Cotan, Mar 18, 2010.

 1. C

  Cotan Member

  #1
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 11, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Nimesikitishwa sana na kitendo nilichofanyiwa na hawa jamaa wa Access Bank.
  Mnanamo mwezi wa kumi na moja mwaka jana nilienda Access Bank kwaajili ya kufungua Account ya Kampuni, nilipofika niliwaona wahusika na wakanipatia taratibu zao za kufuata kwaajili ya kukamilisha zoezi la kufungua Account.

  Nami niliwaletea nyaraka zote walizozihitaji ktk mchakato mzima.Baada ya kukabidhi nyaraka hizo niliambiwa nisubiri baada ya siku tatu nitajulishwa.Baada ya siku tatu nilienda nikaambiwa kuwa nisubiri kidogo kwani nyaraka zangu zimepelekwa BRELA kwaajili ya uhakiki km kweli kampuni imesajiriwa.Jamaa akaniambia kuwa nitapigiwa simu wakati wowote pindi mambo yakiwa tayari.

  Jambo la ajabu nimesubiri kwa muda mrefu bila majibu duh nikaamua kwenda Internataional Commercial Bank kuanza zoezi jipya la kufungua Account, nimetumia km wiki mbili hivi Account ikawa imefunguliwa.Sasa nikabaki na maswali lukuki iweje hawa watumie wiki mbili tu kufungua Account ili hali Access Bank sasa ni miezi mitano bila jibu lolote!?.

  Ndipo nikaamua kurudi tena Access Bank, mhusika nikamuliza kwanini zoezi hili limechukua mda mrefu namna hii?, ili hali ICB wametumia wiki mbili tu?.jamaa akaniambia kuwa tatizo ni BRELA kwani mafairi yote yamekwisha pelekwa huko, lakini kila wakifuatiliwa wanaambiwa mafairi hayaonekani, wakati mwingine wanaabiwa njoo kesho bado tunatafuta mafairi.Pia akanitanabahisha kuwa ktk kila Bank kunatofauti wa kushughurika mambo eti kuna baadhi ya Bank wanatoa kitu kidogo kwa jamaa wa BRELA ili kurahisisha mambo.duh TZ kila kitu ni rushwa hata kufungua Account mnaomba rushwa.Duh kumbe ndo maana watu wa ICB waniliambia nitoe Tsh 15000/= ya kurahisisha mambo kule BRELA. duh watu wa BRELA acheni mambo hayo jamani munaturudisha nyuma kimaendeleo.
   
 2. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #2
  Mar 18, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,767
  Likes Received: 216
  Trophy Points: 160
  Rushwa kila kona - hizi idara za serikali nazo zinanuka rushwa tupu- visingizio eti mishahara midogo tuishi vipi.
   
 3. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #3
  Mar 18, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  hii kansa na haiwezi kuisha kwa mbwembwe za kitanzania kama tunanvyotaka iwe. Inabidi kuwa serious kama unavyoona sasa inakuwa institutionalised hali ni mbaya jamani. Tunaenda wapi?????
   
 4. NGULI

  NGULI JF-Expert Member

  #4
  Mar 18, 2010
  Joined: Mar 31, 2008
  Messages: 4,812
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Hapo bado....ukipata mkopo kuna stage ya registration of title deed/morgage pale arthi utarudi na thread nyingine hata Bank wenyewe wanaotaga rushwa.
   
 5. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #5
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,263
  Likes Received: 22,007
  Trophy Points: 280
  Nini kifanyike kuepukana na laana hii?
   
 6. M

  Mkorintho JF-Expert Member

  #6
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 17, 2009
  Messages: 353
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kaaazi kweli kweli, Tanzania zaidi ya uijuavyo
   
 7. Mponjoli

  Mponjoli JF-Expert Member

  #7
  Mar 18, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 668
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  BRELA wamelaaniwa wale,wanapoteza mafaili makusudi ili uwape kitu kidogo
   
 8. Tripo9

  Tripo9 JF-Expert Member

  #8
  Mar 18, 2010
  Joined: Sep 9, 2009
  Messages: 2,168
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Hakuna la kufanya hapa.

  We ukitinga sehem yoyote kufatilia mambo yako andaa fungu pembeni mambo yateleze.

  Ukijifanya mnoko utakonda buree. Hizo keshokesho utakazopewa uta-surrenda mwenyewe!

  The last date of last year nilijikuta nagawa pesa nono kupush ishu yangu flan. Na thank god mambo yalifanyika kwa kasi nnayotaka.
  Kabla ya hapo nilijifanya mlokole nikaangukia pua.

  Hii ndo Tanzania bwana amani jingiii!
   
 9. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #9
  Mar 19, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Awali ya yote, niseme wazi kwamba mimi si mwajiriwa wa ICB kwahiyo isionekana kwamba nawatetea kuhusu hiyo sh. 15,000/=.. Kuhusu sh.15,000/=, hiyo ni ada pale BRELA. Limited company ni sh. 15,000/= na kwa just registered business ni sh. 1,000/=. Tatizo mkuu ni BRELA. Kuna wakati nami niliwahi fanya kazi kwenye benki moja hapa jijini na hicho kilikuwa ni kitengo changu. Sio siri, ilikuwa akija mteja kwa ajili ya kufungua business account nilikuwa nakaribia kukata roho kila nilipoukumbuka usumbufu wa BRELA. Nini miezi mitano mkuu, staff wa benki wakizubaa inachukua hata mwaka na zaidi pale BRELA bila kupata taarifa. Bila shaka wanachofanya ICB ni kufuatilia hizo documents physically na kuwaghasi kila siku. Lakini ukiwasubiria BRELA wenyewe ndio warudishe basi inaweza kuchukua hata mwaka mitatu na zisirudi.
   
 10. Injinia

  Injinia JF-Expert Member

  #10
  Mar 19, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 850
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0

  Mimi nina principle ambayo bado ni mpya kidogo: kuanzia sasa nikiwa naenda kwenye ofisi za serikali au zinginezo ninakohitaji huduma nitakuwa naenda na chombo cha kurekodia (vipo vingi tu vidogo, size ya flash disk/ memory stick)

  Nitahakikisha narekodi mtu yeyote anayenitaka rushwa/ chai etc.

  Hata kama mahama zetu hazina utaratibu wa kukubali ushahidi wa namna hii (kama ambavyo MKJJ aliwahi kunijibu hapa JF), nitaweka hata hapa JF watu wasikie.
   
 11. jossey1979

  jossey1979 Senior Member

  #11
  Mar 19, 2010
  Joined: Apr 28, 2008
  Messages: 168
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Watanzania!! Watanazinia!! Watanzania!!
  Naomba tusiwalaumu hawa jamaa hata chembe. Tena naona kama hiyo 15,000 bado ni ndogo.
  msha wa TGS D ambaye ni graduate ni shilingi ngapi?
  we m2 mwenye Degree anapata take home salry ya 250,000. how do you expect him to survive.
  Watu wengi wanaokimbilia kufanya kazi serikalini. Sababu kubwa ni rushwa na bila rushwa ni vigumu ku-sirvive!!

  1.kodi ya nyumba ya kawaida hapa Dar ni shilingi ngapi?
  2.nauli kwa mwezi ni shilingi ngapi?
  3.wewe na familia yako kwamwezi mnatumia kiasi gani kwenye chakula?
  4.Ada ya watoto/mtoto ni shilingi ngapi kwa mwezi?
  5.Bia je?
  ----
  ----
  ----
  Kama 250,000 inatosha kwa m2 kusurvive mambo yote hayo basi siwezi kumtofautisha na yule mwanamke kwye bibilia alimsadia Elisha, chombo chake kikiwa hakiishi unga.

  Ningefurahi Tukalaumu mfumo wa hii serikali. They have to look again kwenye hiliswala la TGS zao na viwango wanavyotoa
   
 12. kilemi

  kilemi JF-Expert Member

  #12
  Mar 19, 2010
  Joined: Mar 13, 2009
  Messages: 520
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Kama hukuwapa Eccess Bank hiyo 15, basi usiwalaumu!!
   
 13. Z

  Zamazamani JF-Expert Member

  #13
  Mar 22, 2010
  Joined: Jun 13, 2008
  Messages: 1,621
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  mi nilishawahi kuandika kuhusu usumbufu nilioupata wakati nataka kufungua akaunti pale Barclays mpaka nikatoa rushwa/chai...ingawa mwisho wa siku mpaka leo haijafunguka bado..tukajaribu Access Bank ambako ilichukua kama miezi miwili na nusu kufungua akaunti kwa mbinde sana ..watu walipiga kelele wee humu kwamba sikutakiwa kutoa kitu kidogo(niliwashangaa sijui kipi cha ajabu)..nafikiri wana ukana utanzania wao...nafikiri tatizo hawaishi hapa au wamesahau 'ngoma zetu' baada ya kukaa nje miaka mingi...LAKINI HII NDIO HALI HALISI.....ukitaka huduma yeyote hata kama haki yako lazima uwe na chochote kitu kabisa..mambo yatakwenda mswano,ukijifanya mbishi utaozea mbali...
  ONYO:pamoja na yote,inatakiwa uwe mwangalifu wakati wa kutoa chai manake wengine ni matapeli tu ,unaweza ukatoa rushwa kwa wrong person,then utakesha.......hakikisha unampa rushwa the right person ili ufanikiwe...!!!Bongo zaidi ya uijuavyo....
   
 14. d

  dixon Member

  #14
  Mar 22, 2010
  Joined: May 13, 2009
  Messages: 7
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ....majibu haya hapa ...hilo tatizo sio la access bank tatizo lipo brela mimi ni mwajiliwa wa bank moja hapa dsm huwezi hamini tangu 2009 hadi leo hatuja fungua account tatizo lipo huko brela,maombi ni mengi hapa kwenye tawi letu ya kutaka kufungua akaunti za kampuni lakini brela wamekuwa si wepesi wa kujibu,
  kutoa 15000 ni sawa kwani ni "search fee"
  udhaifu ninao uona ni huu...nimeshawahi kwenda hapo brela jinsi wanavyo tunza mafaili yao kuyapata si rahisi,pia bado wanatumia mtindo wa "manual work"hawajaweka faili zao kwenye mtindo wa electronics,sasabasi hayo yote yanachangia kuwepo kwa mianya ya rushwa.si hayo tu hata kupeleka faili lithibitishwe kama kampuni ipo au laa,kuna foleni isiyo na msingi inayo tengeneza mazingila ya rushwa.yapo mengi wanajamii.
   
 15. m

  mwanza JF-Expert Member

  #15
  Jun 16, 2010
  Joined: May 7, 2009
  Messages: 508
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 60
  Problem sio kupata shilingi ngapi, inatakiwa tunawabana waache rushwa ili waungane na TUICO wakadai maslahi zaidi. nchi za wenzetu wamekataa rushwa ila wanawajibika kudai mishahara ya kutosheleza mahitaji.

  Hata Serikali inakuwa na kiburi kwa sababu wanajua wafanyakazi 80% ya maisha yao yanategemea rushwa kwa hiyo hawana uwezo wa kuacha kazi au kusimama na kudai maslahi. Ni waalimu tu ndio ambao rushwa sio kubwa ndio wanaweza kudai na serikali inalijua hilo ndio maana wakitishia inaongea nao.
   
 16. Ntemi Kazwile

  Ntemi Kazwile JF-Expert Member

  #16
  Jun 16, 2010
  Joined: May 14, 2010
  Messages: 2,145
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Mimi mbona nimefunga account ya kampuni CBA haijachukua hata wiki???????? Au ndo kila benki na utaratibu wake. Lakini pia naomba kuwatetea BRELA, mimi mwaka jana nilisajili kampuni na wala sikutoa hata senti na faili lilikwenda bila kukwama popote. Ingawaje kweli inahitaji mtu ufuatilie kwa karibu
   
 17. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #17
  Jun 16, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,502
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Au wagome kufanya kazi au wasituombe kitu kidogo.

  Dawa ni kuwarekodi tu. Maadamu YOUTUBE ipo, tuwatundike wala rushwa (njoo kesho) woteeee.
   
 18. Drifter

  Drifter JF-Expert Member

  #18
  Jun 16, 2010
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 1,968
  Likes Received: 668
  Trophy Points: 280
  Huu ndio mtindo wa maisha uliojengeka Tanzania kwa miaka mingi unaowafanya wengi kutokuwa na utashi wa kujenga taifa lenye misingi inayoeleweka lenye mfumo bora wa uongozi. It is a system corrupted through and through from the top to bottom. Not even education or religion can help.
   
 19. Eng. SALUFU CA

  Eng. SALUFU CA Senior Member

  #19
  Jun 16, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 146
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  No comments
   
 20. N-handsome

  N-handsome JF-Expert Member

  #20
  Jun 16, 2010
  Joined: Jan 23, 2008
  Messages: 2,317
  Likes Received: 128
  Trophy Points: 160
  Tumukodishe Kagame for 2 years
   
Loading...