Academics &Professional CV ya Deogratius Nalimi Kisandu

Academics &Professional CV ya Deogratius Nalimi Kisandu

mbona siku ulizoingia darasani kufundisha huja orodhesha kwenye CV yako??
 
Yaani CV yako imepambwa na Elimu ya ngumbaru na kurisiti pepa, hata post zako humu zinathibitisha we ni ngumbaru
 
Hivi hii ni Cv au upupu? Watu tuna cv zenu tumehamua kutulia tu..
 
Hii ndio Biograph ya Deogratius Kisandu.

Kuzaliwa: 28 Juni 1980. Siku ya Jumamosi.

1990-1994: Shule ya msingi Sunge, kata ya Busoka, Kahama, Shinyanga. Darasa la i-v.

1995-1996: Shule la msingi kahama, kahama, Shinyanga. Darasa la vi-vii.

1997: Kidato cha kwanza, Magu sekondari, Magu, Mwanza.(Evening Class-ODL).Niliishia Form one tu.

July 1998-April 1999: Mtawa shirika la Ndugu wadogo wa Afrika, Morogoro. Niliishia hatua ya Uaspiranti tu(Utakaji) hivyo sikutunukiwa cheti zaidi ya Kitambulisho.


April 1999-2002: Form i-iv, Kishimba sekondari, Kahama, Shinyanga.(Evening classes-ODL).

Desemba 2002-2003: ASTASHAHADA ya Uandishi wa habari, Chuo cha Royal College of Journalism, Dar es Salaàm.

2004: Mwandishi wa habari wa kujitegemea.

2007: Ku attend mtihani wa Kidato cha sita katika kituo cha kufanyia mtihani cha sekondari ya wasichana Tabora.(Cheti cha kidato cha sita)

April 2007-Juni 2007: Induction course for secondary school Teachers, Chuo cha ualimu Tabora(Leseni ya kufundishia 2007-2012).

2007-2012: Mwalimu, Shule ya sekondari Mwamala, Nzega, Tabora.

2008: Kurudia mtihani wa kidato cha sita (resitter), Kahama sekondari.

2008: Msimamizi Mkuu, mtihani kidato cha Pili, Mogwa sekondari, Nzenga.

April 2009: Msahihishaji wa Mitihani ya Mock kidato cha NNE, kanda ya Magharibi, Tabora.(Somo la kiswahili).

2009-2012: Shahada ya Elimu Maalum(Ndani yake nimesoma Political Science and Public Administration), Chuo Kikuu kishiriki cha Tumaini Makumira cha Sebastian Kolowa(SEKUCo), kwasasa SEKOMU.

2013 up to date: Mwalimu, Shule ya sekondari Mkolani, Mwanza.

2013: Mafunzo maalum ya Gesi asilia na madini, Mwanza, TEITI.

2014: Muwezeshaji Kongamano la KATIBA Mpya, Mwanza.

April 2014: Mafunzo maalum ya mahusiano ya Ndoa na Uchumba, JRC, Mwanza.

2016: Semina ya kusimamia mtihani na kusahisha kidato cha sita, Mwanza.

2016: Msimamizi wa mitihani kidato cha sita, Ngaza sekondari, Mwanza.

2016: Mafunzo maalum ya Imani Takatifu ndani ya Kanisa Katoliki(KATEKESI), Mwanza.

2012-2016: Nimeshiriki semina zote za JUKWAA LA KATIBA kupitia taasisi yetu ya JUKWAA la Mwalimu na Wanafunzi Tanzania (Teachers and Students Forum Tanzania).

Niliposahau nitaleta mwendelezo,

Wenu wa karibu:

Deogratius Nalimi Kisandu.

KANJANJA aka KILAZA at work. Huoni hata aibu kujipambanua kuwa wewe ni Mbangaizaji wa elimu unayetaka kuwaaminisha wajinga wenzio kuwa nawe ni msomi.

Ninyi ndo wezi na walanguzi wa elimu mlioshindwa kusoma na badala yake mnataka kuonekana kuwa mmesoma.

Kwa hali hii, haustahili hata kupewa nafasi yoyote ya uongozi kwa sababu utatia najisi.

kwa kuanza, nikuulize swali ilikuwaje ukamalizia shule Kahama na ukachaguliwa kwenda Srkondari ya Magu Day?
 
Nahisi CCM wanamtumia huyu jamaa kupunguza kura za Upinzani maana hata sababu za msingi kuanzisha chama hana, anasema tu CCM ilimtesa sana, nachoshangaa zaidi ni yeye kusema anateswa huku bado ni Mtumishi wa serikali ya CCM, Unatesekaje sasa? Kwa CV hiyo wamekuvumilia unasahihisha mpaka mitihani, unapata ofa ya kuwa kwenye jukwaa la katiba, unashiriki siasa wakati wewe ni mwalimu na hawajakufukuza halafu unasema wanakutesa! Are you mad? What is wrong with you brother? I'm sorry to ask u these questions

Kuna watu wanasema huenda tayari akili yako ina dosari au umeamua kutuchekesha tu tupate faraja na ugumu huu wa maisha.

Mimi binafsi nahisi wewe unatumika kutekeleza kanuni ya DIVIDE AND RULE
 
imhotep undugu ni kufaana na si kufanana. Nimekukubali sana kwa jinsi unavyompiga tafu ndugu yako na kumpa mawazo kuntu. Nashangaa kwa nini asikupendekeze uwe Katibu Mkuu wa ACA!
 
imhotep undugu ni kufaana na si kufanana. Nimekukubali sana kwa jinsi unavyompiga tafu ndugu yako na kumpa mawazo kuntu. Nashangaa kwa nini asikupendekeze uwe Katibu Mkuu wa ACA!
Mimi ni mwanachama wa chama cha mapinduzi,na nimeona nimsaidie ili ndoto yake itimie,lakini najua ana safari ndeefu yenye milima mikali na makorongo mareefu,ila never underestimate anyone.
 
What is your intention for all this...sijakusoma bado unachojaribu kukileta humu JF!someone help plzz
Naona na sisi tulete zetu ili utofauti uonekane , naona anayo bahati ajamkuta Prf.Ndalichako
 
Back
Top Bottom