Academics &Professional CV ya Deogratius Nalimi Kisandu

Academics &Professional CV ya Deogratius Nalimi Kisandu

Kwa Walimu wa akili ya Kisandu, tutafika kweli kwenye Tanzania ya Viwanda!?!
 
Sijawahi kuona,,, unahudhuria mafunzo ya kusahihisha mtihani wa darasa la nne na unaeleza kwenye CV.!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Mbona Kama umeshazeeka kabla ya wakati,pole Sana watu wa age huwezi kujifananisha nao kbs
 
Kwa CV yako Doooh, yaani JF burudani tupu mwanzo mwisho.
Hon Nawie hakiigusa hatatukosesha mengi sana!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Hii ndio Biograph ya Deogratius Kisandu.

Kuzaliwa: 28 Juni 1980. Siku ya Jumamosi.

1990-1994: Shule ya msingi Sunge, kata ya Busoka, Kahama, Shinyanga. Darasa la i-v.

1995-1996: Shule la msingi kahama, kahama, Shinyanga. Darasa la vi-vii.

1997: Kidato cha kwanza, Magu sekondari, Magu, Mwanza.(Evening Class-ODL).Niliishia Form one tu.

July 1998-April 1999: Mtawa shirika la Ndugu wadogo wa Afrika, Morogoro. Niliishia hatua ya Uaspiranti tu(Utakaji) hivyo sikutunukiwa cheti zaidi ya Kitambulisho.


April 1999-2002: Form i-iv, Kishimba sekondari, Kahama, Shinyanga.(Evening classes-ODL).

Desemba 2002-2003: ASTASHAHADA ya Uandishi wa habari, Chuo cha Royal College of Journalism, Dar es Salaàm.

2004: Mwandishi wa habari wa kujitegemea.

2007: Ku attend mtihani wa Kidato cha sita katika kituo cha kufanyia mtihani cha sekondari ya wasichana Tabora.(Cheti cha kidato cha sita)

April 2007-Juni 2007: Induction course for secondary school Teachers, Chuo cha ualimu Tabora(Leseni ya kufundishia 2007-2012).

2007-2012: Mwalimu, Shule ya sekondari Mwamala, Nzega, Tabora.

2008: Kurudia mtihani wa kidato cha sita (resitter), Kahama sekondari.

2008: Msimamizi Mkuu, mtihani kidato cha Pili, Mogwa sekondari, Nzenga.

April 2009: Msahihishaji wa Mitihani ya Mock kidato cha NNE, kanda ya Magharibi, Tabora.(Somo la kiswahili).

2009-2012: Shahada ya Elimu Maalum(Ndani yake nimesoma Political Science and Public Administration), Chuo Kikuu kishiriki cha Tumaini Makumira cha Sebastian Kolowa(SEKUCo), kwasasa SEKOMU.

2013 up to date: Mwalimu, Shule ya sekondari Mkolani, Mwanza.

2013: Mafunzo maalum ya Gesi asilia na madini, Mwanza, TEITI.

2014: Muwezeshaji Kongamano la KATIBA Mpya, Mwanza.

April 2014: Mafunzo maalum ya mahusiano ya Ndoa na Uchumba, JRC, Mwanza.

2016: Semina ya kusimamia mtihani na kusahisha kidato cha sita, Mwanza.

2016: Msimamizi wa mitihani kidato cha sita, Ngaza sekondari, Mwanza.

2016: Mafunzo maalum ya Imani Takatifu ndani ya Kanisa Katoliki(KATEKESI), Mwanza.

2012-2016: Nimeshiriki semina zote za JUKWAA LA KATIBA kupitia taasisi yetu ya JUKWAA la Mwalimu na Wanafunzi Tanzania (Teachers and Students Forum Tanzania).

Niliposahau nitaleta mwendelezo,

Wenu wa karibu:

Deogratius Nalimi Kisandu.

Please CC Prof Ndali nadhani hataifurahia sana hiyo CV kuliko sisi wana JF.
 
Mwenyekiti mtarajiwa asante sana,sasa ebu tuwekee na sera za chama chako!
 
Back
Top Bottom