Odhiambo cairo
JF-Expert Member
- Jul 11, 2015
- 15,989
- 22,057
Mbaya zaidi na sijui kama ina ukweli. Ni kuwa mikataba hii haiwezi kuangaliwa upya au kurekebishwa, mpaka ipete miaka 60 kati ya miaka 100 ya mkataba .Mimi siyo mwanasheria wala mfanyabiashara, so please correct me if I am wrong.
Nilishawahi kuambiwa kuwa hakuna kipengele muhimu kwenye mikataba kama eneo linalozungumzia migogoro na hatua za kuvunja mkataba huo. Pande mbili au zaidi zinapoingia kwenye mkataba, na katikati ya muhula kukatokea tatizo, upande wowote unaweza kutoa lalamiko au kutaka kuvunja mkataba.
Hapo kipengele cha majadialiano, mapatano na usuluhishi (negotiation, mediation & arbitration) hutumika. Kama katika kipindi cha mkataba upande mmoja una ushahidi kuwa upande mwingine umedhulumu au kutekeleza uhalifu uliogusa makubaliano ya mkataba huo, wanayo fursa ya aidha kuvunja mkataba na kudai fidia au kusuluhisha kwa kudai fidia na kubadili mkataba. Mara nyingi hili huletwa kwenye meza ya majadiliano na mapatano (amicable resolution) kabla ya kufikishwa mahakama za usuluhishi.
Sasa, ikiwa sisi kama nchi tunao ushahidi kuwa Barrick/Acacia wamevunja makubaliano au kwenda kinyume na mkataba kwa kutakatisha fedha, kukwepa kodi na rushwa, kwa nini tusiutumie ushahidi huu katika majadiliano tukidai fidia? Au kama tumeshindwana mezani kwa nini tusichukue hatua nyingine katika mkataba ya kushitaki mahakamani ilhali ushahidi tunao?
Hata kama dunia inajua kuwa Barrick/Acacia wametuibia sana tatizo linakuja jinsi tunavyokabiliana na hili. We are setting precedence on any other contracts in the mining or extractive industries. Wawekezaji duniani wanaangalia au wataangalia mikataba yetu iliyotangulia na jinsi tumeikabili na maamuzi yao yatategemea na utekelezaji wetu. Sawa inawezekana kwa kukataa usuluhishi kwenye mahakama za kimataifa (international arbitration) tunawapa wakati mgumu Acacia kuuza hisa zao wakimbie, lakini pia tunajiumiza na sisi. Itakuwa vigumu sana kwa mwekezaji wa kimataifa kukubali kuingia mkataba na sisi ikiwa tumekataa international arbitration. Labda bidhaa iwe bei ya madafu kiasi kwamba wanauwezo wa kufyonza hasara yoyote watakayopata.
Kingine, mikataba yote inayohusu rasilimali za nchi haiingiwi na mtu binafsi, ni serikali ndio inaingia mkataba kwa niaba ya nchi. Kama awamu ya kwanza waliingia mkataba na X, awamu ya pili inapoingia haiwezi kumwambia X kuwa "siutambui mkataba huu kwa kuwa ulisaini na flani wa awamu ya kwanza". Tutafeli sana tukifanya hivyo. Hayo ya nani alikosea tushikane humu humu ndani ya nchi bila kuathiri mikataba nje ya utaratibu wa mikataba hiyo.
Ila kama tunaamua kuyafukia madini hadi pale tutakapokuwa na uwezo wa kuyachimba na kuyafua wenyewe, basi tujiandae kwa hilo na lolote lijalo. Pasi na hayo, tunaweza kujiharibia kwenye uwekezaji wa nje.
POOR WE