Acacia Yatutangaza Vibaya Duniani, Yadai Tanzania Kuna " risks to the safety and security of people"!, Mwekezaji Gani Ata Invest Kwenye Such Risks?!.

Mwekezaji gani atakuja na atawekeza katika Nchi ambayo tajiri wake mkubwa kabisa, anatekwa katika mazingira yanayoacha maswali millioni na Serikali haioneshi kushtushwa hata kidogo na tukio hilo la utekwaji na kuona ni kitu cha kawaida kabisa.....kiufupi it will take next 20 years to build that business trust.....
 
Nachokiona mbeleni Accasia watatushinda mahakamani then tuanze kuwalipa watakaolipa wakina nani wananchi wanyonge je walioingia mikataba ya kikoloni na Accasia wako wapi wako Masaki kwenye makasiri yao wanapunga upepo Afrika tuna laana ya asiri
 
Mayala, tumepoteza muda mwingi sana kwa kuhangaika na mambo ambayo hata yakipata ufumbuzi kilichobaki hakilingani na kilichopotea.
Aidha sijasikia tukichukua hatua za kusomesha watu wetu kuwa weledi katika sekta ya madini; bado soko la madini yote ni nje, bado teknolojia tunawategemea wao.
Kadhia hili linaloendelea halitusogezi hatua hata moja mbele- Mungu atusaidie tuchukue hatua sahihi zaidi
 
Ndugu paskali, nafikiri mambo ya mazungumzo kati ya serikali na Barrick ni siri.

Pia suala la majadiliano kukaa Muda mrefu, huku wenzetu wakienda mbali na kutaka kuuza hisa zake kwa China, ni kitendo ambacho kwangu nakiona kama ni dharau kwa nchi yetu, kukimbia tatizo na pia kuonyesha dhamira yao huko mbele ni kukimbia nchi na si vinginevyo.

Kishika uchumba hawajalipa, lakini kumbuka kuwa Barrick kaingia hapo kwenye majadiliano kwa sababu yeye ndo mwenye hisa nyingi hivyo kuna kupiga kura kwenye maamuzi yao. Mimi ninahisi pia accacia pamoja na makosa yao, watatumia uzungu wao, ujeuri wa pesa na nchi zao kutudharau. Kumbuka kuwa kuna hata uwezekano wa makampuni haya mawili kuingia kwenye vita ya wao kwa wao na kupelekana hata mahakamani kwa sababu ya majadiliano hayo.

Kwa kuwa hawajatimiza yale ya msingi katika malengo ya majadiliano, serikali hata hvyo ina ushahidi mwingi wa makampuni hayo kudanganya serikali kwa kupeleka under estimation ya mizigo yao, data, fraud, tax evasion na mengineyo, that's why wanakuja kwenye meza ya majadiliano wakijua kuwa wataweza kufanikiwa as usual na wakakuta tuko poa.

Kwa wale waliokamatwa viongozi wa accacia na serikali, kwa kusababisha hasara, na mengineyo, wanastahili Hilo baada ya uchunguzi wa PCCB, ila hofu kwao ni siri hizo kujulikana na si vinginevyo.

Nafikiri sasa serikali ipo makini na nasikia hata hao wazungu nao wakija watajumuishwa tu kwenye michezo yao michafu. Nakumbuka kuna siku kiongozi mkuu wetu alisema hadharani kuwa alituma mtu na kwenda kuchukua data zao huko na walivyojua wakadelete lakini tayari tunazo.

Kumbuka hata kiongozi wa Barrick juzi hapa aliwahi kusema kwenye press conference kuwa ni kweli wametuibia sana serikali yetu na wamekubali na hivyo that's why wako kwenye majadiliano.

Sijajua ripoti ya uchunguzi wa yale maji ya sumu kwenye mto tigiti nayo kama watakwepa.

Mi nafikiri hawawez kwenda mahakamani kwani wanajua kuwa serikali ipo, ina watu makini na kwa sasa timu yote inayofanya kazi hiyo ipo chini ya ulinzi mkali na hivyo hawawez kuwapa rushwa au kuwapa ushawishi wa aina yoyote kama zamani

Heko Rais, pia hawa watu wana mtandao mkubwa wa kidunia na hvyo hizo PROPAGANDA ZA KUTUCHAFUA HAWAWEZ NA PIA WAWEKEZAJI WENGI WAMEAMUA KUJA NCHINI NA KUFUATA TARATIBU NA HAWASUMBULIWI. WAKIAMUA KUONDOKA BASI MCHINA ABAWE HELA MFUKONI ANASUBIR AONDOKE, THAT'S WHY HAWEZ
Unapenda kujifariji ndugu yangu
 
Wanabodi,
Naendelea na zile mada zangu za kuangazia maslahi kwa taifa.
Mambo ya Acacia kututangaza vibaya duniani yanaendelea, kati ya juzi, na leo, wameishatoa press releses 3 kuizungumzia Tanzania, ikiwemo hii ya leo ambazo zote wanalalamikia watu wao kukamatwa na kushitakiwa.
Press Release Item
Juzi waliotoa press releases mbili
Press Release Item
Press Release Item

Kwenye hii press release yao ya leo, wamesema na hapa ninanukuu
Peter Geleta, Interim CEO of Acacia stated: “Against this strong operating performance, I am, however, deeply concerned about the increasing risks to the safety and security of our people and the increasingly challenging operating environment in Tanzania which could impact the outlook for the business".

Wamesema kwanza wataishitaki Tanzania kwa baba yao Barrick, kushinikiza madai yoyote ya serikali dhidi ya Acacia, yajumuishwe kwenye mazungumzo yanayoendelea, pili watafanya majadiliano na serikali, kuachana na hizi kamata, kamata, sweka ndani na shitakiana shitakiana za watumishi wao, serikali yetu isipowasikiliza, then watatushitaki MIGA!.

My Take.
1. Kwa serikali yetu: kwa vile tunamazungumzo yanayoendelea kati ya serikali yetu na Barrick kuhusu Acacia, na msingi mkuu wa mazungumzo hayo ni Trust and Transparency, yaani kuaminiana na uwazi, kitendo cha kuwashitaki Acacia kwa jambo linalozungumzika mezani, ni breach of trust, kwa nini matatizo yote kabisa ya Acacia na serikali yetu yasiwe consolidated na kupelekwa kwenye meza ya mazungumzo?. Na kama haya mashitaki ni hasira tuu za kucheleweshewa kila kishika uchumba chetu, simamisheni kwanza kila kitu, kishika uchumba kitoke, ndipo mazungumzo yaendelee!.

2. Kitendo cha wanasheria wetu nguli, kukubali kufanya mazungumzo na Barrick bila mhusika mkuu Acacia kushirikishwa, ni udhaifu mkubwa, kwa sababu chochote kitakachokubaliwa, the final ni Acacia na sio Barrick, its not too late kuwakaribisha Acacia now, ili chochote kitakacho fikiwa na mazungumzo yale kiwe ni final and conclusive.

3. Pia tumeonyesha udhaifu kwenye composition ya timu yetu ya mazungumzo, kumbe hatuna watu wa PCCB mule?!, ndio maana huku serikali yetu inazungumza na Barrick kuhusu Acacia, huku BCCB wako busy kuwafungulia mashitaka, tuiongeze timu yetu tuwaweke watu wa kila sekta, ili kila kitu kiwekwe mezani, likiisha liishe jumla.

4. Kwa Acacia: Unapokuwa kwenye nchi ya watu, ukijivunia rasilimali za nchi hiyo, inakubidi uwe na adabu na heshima, sometimes unaweza kulazimika kukaa kimya tuu hata kama unaonewa, ili uzimuudhi mwenye mali!, huwezi kuutangazia ulimwengu kuwa Tanzania ni nchi yenye safety and security risk, kwa sababu tuu watu wako wameshitakiwa!.

5. Mwisho: Serikali yetu iwe wazi, truthfully na very transparently kinachoendelea kwenye mazungumzo yetu, its not fair, hata sisi Watanzania wenyewe, tunapata updates kutoka Barrick au Acacia, tungependa kupata taarifa rasmi kutoka kwetu.

Paskali
Serikali ya awamu ya tano haiupendi uwazi na haitaki kuwa wazi.
Kuthibitisha hilo ilijitoa kwenye OGP.
Ili ifanye kila baya inaloliweza.

Shetani ni shetani tu.
 
5. Hakuna mwenye uthubutu wa kutoa updates, mambo siyo mambo... utoe updates hujitakii mema...

Tulishakosea, inabidi tujiokote na kurekebisha mambo yakae sawa...

Cc: mahondaw
 
Pascal acaccia kutusema vibaya ughaibuni ni sawa. Usalama uko wapi kama tajiri na 1 anatekwa ki madoido ?!.
Lakini kubwa ni kuwa awamu ya tatu chini ya BWM iliirudisha Tanganyika utumwani kwa kuiingiza kwenye mikataba, ambayo haiwezi kujinasua. Tutawatafuta wachawi sana lakini tatizo ni sisi wenyewe.
Jinsi mnavyo rusha lawama kuhusu kutekwa MO utafikiri yeye ndio bilionea wa kwanza duniani kutekwa.
Mwaka 1983 mwezi Novemba Bilionea Freddy Heineken mmiliki wa bia ya Heineken wadhamini wa UEFA Champions League alitekwa kwa siku kadhaa huko kwao Uholanzi, mbona nchi yake haikutangazwa sio mahali salama?!
 
Wanabodi,
Naendelea na zile mada zangu za kuangazia maslahi kwa taifa.
Mambo ya Acacia kututangaza vibaya duniani yanaendelea, kati ya juzi, na leo, wameishatoa press releses 3 kuizungumzia Tanzania, ikiwemo hii ya leo ambazo zote wanalalamikia watu wao kukamatwa na kushitakiwa.
Press Release Item
Juzi waliotoa press releases mbili
Press Release Item
Press Release Item

Kwenye hii press release yao ya leo, wamesema na hapa ninanukuu
Peter Geleta, Interim CEO of Acacia stated: “Against this strong operating performance, I am, however, deeply concerned about the increasing risks to the safety and security of our people and the increasingly challenging operating environment in Tanzania which could impact the outlook for the business".

Wamesema kwanza wataishitaki Tanzania kwa baba yao Barrick, kushinikiza madai yoyote ya serikali dhidi ya Acacia, yajumuishwe kwenye mazungumzo yanayoendelea, pili watafanya majadiliano na serikali, kuachana na hizi kamata, kamata, sweka ndani na shitakiana shitakiana za watumishi wao, serikali yetu isipowasikiliza, then watatushitaki MIGA!.

My Take.
1. Kwa serikali yetu: kwa vile tunamazungumzo yanayoendelea kati ya serikali yetu na Barrick kuhusu Acacia, na msingi mkuu wa mazungumzo hayo ni Trust and Transparency, yaani kuaminiana na uwazi, kitendo cha kuwashitaki Acacia kwa jambo linalozungumzika mezani, ni breach of trust, kwa nini matatizo yote kabisa ya Acacia na serikali yetu yasiwe consolidated na kupelekwa kwenye meza ya mazungumzo?. Na kama haya mashitaki ni hasira tuu za kucheleweshewa kila kishika uchumba chetu, simamisheni kwanza kila kitu, kishika uchumba kitoke, ndipo mazungumzo yaendelee!.

2. Kitendo cha wanasheria wetu nguli, kukubali kufanya mazungumzo na Barrick bila mhusika mkuu Acacia kushirikishwa, ni udhaifu mkubwa, kwa sababu chochote kitakachokubaliwa, the final ni Acacia na sio Barrick, its not too late kuwakaribisha Acacia now, ili chochote kitakacho fikiwa na mazungumzo yale kiwe ni final and conclusive.

3. Pia tumeonyesha udhaifu kwenye composition ya timu yetu ya mazungumzo, kumbe hatuna watu wa PCCB mule?!, ndio maana huku serikali yetu inazungumza na Barrick kuhusu Acacia, huku BCCB wako busy kuwafungulia mashitaka, tuiongeze timu yetu tuwaweke watu wa kila sekta, ili kila kitu kiwekwe mezani, likiisha liishe jumla.

4. Kwa Acacia: Unapokuwa kwenye nchi ya watu, ukijivunia rasilimali za nchi hiyo, inakubidi uwe na adabu na heshima, sometimes unaweza kulazimika kukaa kimya tuu hata kama unaonewa, ili uzimuudhi mwenye mali!, huwezi kuutangazia ulimwengu kuwa Tanzania ni nchi yenye safety and security risk, kwa sababu tuu watu wako wameshitakiwa!.

5. Mwisho: Serikali yetu iwe wazi, truthfully na very transparently kinachoendelea kwenye mazungumzo yetu, its not fair, hata sisi Watanzania wenyewe, tunapata updates kutoka Barrick au Acacia, tungependa kupata taarifa rasmi kutoka kwetu.

Paskali
Ungeamua kuwa mkweli ungeisha kubali tuliingia wenyewe kwenye mtego aina ya mgono kwa sheria na mikataba ya hovyo tulioingia.
Walotuonya na kushauri namna njema ya kujitoa waliitwa wasaliti na kupigwa risasi kama wanyamapori. Katika jitihada za kuficha nyuso zilizojaa aibu.
Hao jamaa bado wameshika kisu kwenye mpini na wataendelea kusumbua sana. Hawalazimiki kulipa chochote kama tulivyojidanganywa baada ya vikao vya makinikia. Ndg Paschal, makala zako zitakosa uhalisia kama utaendelea kuukwepa ukweli huo. Amen
 
Mimi natetea maslahi ya nchi lakini ninyi mnakuwa na akili mbovu kama farisayo aliyenyimwa mvinyo.
Nimekuuliza toa ushauri wa hoja ambao uko tofauti na ule wa Tundu Lissu lakini wewe unakwepe na kuishia kuniambia Lissu was Right. Nikakuambia kwamba Lissu huwa anakosea mara nyingine na mnapigia makofi bila kufikiria. Sasa kama huleti hoja bali ushabiki wa kisiasa unataka mimi nisemaje mkuu wangu ?

Raisi Magufuli anakosea sana lakini hii isiwe sababu ya kutaka nchi yako iabike bwana. Hebu kueni basi!
Hamuitendei haki nchi yenu wala kusadia vizazi vijavyo kwa huu ushabiki usio na mantiki. Ndiyo maana kuna mabwana wadogo humu ndani huwa nakwaruzana nao kuhusu kutetea kila kitu cha Raisi Magufuli hata kama kinavuruga nchi. Huu siyo Uzalendo mzee!
Kama wewe unatetea maslahi ya nchi ni jambo jema, lakini sijui ni kwa vipi ?!. Lakini kwa viongozi wa taifa hili, hasa ukiacha awamu ya kwanza, hakuna mtetezi wa maslahi ya nchi!! .
Zaidi ni kujilimbikizia mali wao na wana wao. Pia ni kujiimarisha mamlakani kama kina Mobutu walivyokosea. Ni Nyerere tu na kina Kawawa ndio hawakuwa na tamaa ya kujilimbikizia chochote bali utaifa. Kwao madini na mamlaka lilikuwa swala la utaifa kwanza .

Umezungumzia mkuu kuwa kuna baadhi ya mambo anakosea, Je nani au taasisi gani inaweza kumkosoa mkuu akabaki salama ?! Kwa hali ya leo ambapo hata bunge halipewi nafasi hiyo. Bali ni kusifu na kuabudu !!. Je ndiyo aina ya uongozi wa nchi usiotaka ukosolewe. Kwa nini tunavuruga mfumo uliokwishajengwa kwa gharama kubwa kwa ajili ya binaadamu anaeishi na kwisha kufa ?! Mfumo huu ulitakiwa uwe endelevu kwa wajukuu zetu.

Umezungumza kuhusu kumuunga Rais Maghufuli mkono. Mimi binafsi nimemuunga mkono 200%/ kwa baadhi ya mambo e.g. Kuhamia Dodoma, ununuzi wa ndege japo style aliyotumia siyo !!, elimu ya msingi kwa watoto wetu japo simuungi mkono kubagua waTz ktk mikopo ya elimu ya juu. Kuna vitu wapinzani walivipigania awamu ya nne na anafanyia kazi, lakini safari hii hataki wapinzani wake wafanye siasa. Hamtakiwi kulishabikia hili na bahati mbaya katiba imemfanya mkuu wa nchi mungu mutu.

"Katiba mpya ni suluhisho kama hakuna unafki "
 
Jinsi mnavyo rusha lawama kuhusu kutekwa MO utafikiri yeye ndio bilionea wa kwanza duniani kutekwa.
Mwaka 1983 mwezi Novemba Bilionea Freddy Heineken mmiliki wa bia ya Heineken wadhamini wa UEFA Champions League alitekwa kwa siku kadhaa huko kwao Uholanzi, mbona nchi yake haikutangazwa sio mahali salama?!
Na kwanini wafuasi wa mtu fulani, mna halalisha utekaji huo ?!
Kumbuka hata Zakaria asingefurukukuta leo angekuwa historia. Mambo maovu kama haya, si ya kushabikia na hasa vyombo vyetu vinaposhutumiwa !!!
 
Mimi siyo mwanasheria wala mfanyabiashara, so please correct me if I am wrong.

Nilishawahi kuambiwa kuwa hakuna kipengele muhimu kwenye mikataba kama eneo linalozungumzia migogoro na hatua za kuvunja mkataba huo. Pande mbili au zaidi zinapoingia kwenye mkataba, na katikati ya muhula kukatokea tatizo, upande wowote unaweza kutoa lalamiko au kutaka kuvunja mkataba.

Hapo kipengele cha majadialiano, mapatano na usuluhishi (negotiation, mediation & arbitration) hutumika. Kama katika kipindi cha mkataba upande mmoja una ushahidi kuwa upande mwingine umedhulumu au kutekeleza uhalifu uliogusa makubaliano ya mkataba huo, wanayo fursa ya aidha kuvunja mkataba na kudai fidia au kusuluhisha kwa kudai fidia na kubadili mkataba. Mara nyingi hili huletwa kwenye meza ya majadiliano na mapatano (amicable resolution) kabla ya kufikishwa mahakama za usuluhishi.

Sasa, ikiwa sisi kama nchi tunao ushahidi kuwa Barrick/Acacia wamevunja makubaliano au kwenda kinyume na mkataba kwa kutakatisha fedha, kukwepa kodi na rushwa, kwa nini tusiutumie ushahidi huu katika majadiliano tukidai fidia? Au kama tumeshindwana mezani kwa nini tusichukue hatua nyingine katika mkataba ya kushitaki mahakamani ilhali ushahidi tunao?

Hata kama dunia inajua kuwa Barrick/Acacia wametuibia sana tatizo linakuja jinsi tunavyokabiliana na hili. We are setting precedence on any other contracts in the mining or extractive industries. Wawekezaji duniani wanaangalia au wataangalia mikataba yetu iliyotangulia na jinsi tumeikabili na maamuzi yao yatategemea na utekelezaji wetu. Sawa inawezekana kwa kukataa usuluhishi kwenye mahakama za kimataifa (international arbitration) tunawapa wakati mgumu Acacia kuuza hisa zao wakimbie, lakini pia tunajiumiza na sisi. Itakuwa vigumu sana kwa mwekezaji wa kimataifa kukubali kuingia mkataba na sisi ikiwa tumekataa international arbitration. Labda bidhaa iwe bei ya madafu kiasi kwamba wanauwezo wa kufyonza hasara yoyote watakayopata.

Kingine, mikataba yote inayohusu rasilimali za nchi haiingiwi na mtu binafsi, ni serikali ndio inaingia mkataba kwa niaba ya nchi. Kama awamu ya kwanza waliingia mkataba na X, awamu ya pili inapoingia haiwezi kumwambia X kuwa "siutambui mkataba huu kwa kuwa ulisaini na flani wa awamu ya kwanza". Tutafeli sana tukifanya hivyo. Hayo ya nani alikosea tushikane humu humu ndani ya nchi bila kuathiri mikataba nje ya utaratibu wa mikataba hiyo.

Ila kama tunaamua kuyafukia madini hadi pale tutakapokuwa na uwezo wa kuyachimba na kuyafua wenyewe, basi tujiandae kwa hilo na lolote lijalo. Pasi na hayo, tunaweza kujiharibia kwenye uwekezaji wa nje.
Nimehifadhi busara hizi kwenye Archive yangu .
 
Na kwanini wafuasi wa mtu fulani, mna halalisha utekaji huo ?!
Kumbuka hata Zakaria asingefurukukuta leo angekuwa historia. Mambo maovu kama haya, si ya kushabikia na hasa vyombo vyetu vinaposhutumiwa !!!
Hapa tuna tofautiana mtazamo.
Mimi nawaza kuitetea nchi yangu na sio mtu fulani asichafuliwe.

Naheshimu mawazo yako.
 
Back
Top Bottom