Abubakary Liongo: Taarifa zinazosambazwa kuhusu ziara ya Mzee Lowassa Ikulu sio rasmi kutoka ofisi ya Lowassa

Taarifa rasmi ni zipi sasa, maana muda unazidi kuyoyoma na makamanda wanazidi kuchanganyikiwa.
 
Kwa nini wakati wa kwenda hakuaga? Tunaaminije alichomwambia mbowe ndo alichokisema ikulu? Lowasa umenichafua sana!
Kweli mkuu lowassa must go, chadema wasimwonee haya na hili litakuwa funzo kwa wanachama wengine wanaofikiri wapo juu zaidi ya chama
 
Dar es Salaam. Waziri mkuu wa zamani Edward Lowassa amekutana na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ili kumpa mrejesho ya alichozungumza na Rais John Magufuli.

Taarifa iliyotolewa leo Alhamisi na Msemaji wa Lowassa imeeleza kuwa kumekuwa na waraka na taarifa nyingi za kupotosha umma kuhusu ziara ya Lowassa kwenda Ikulu na nyingine zikisemwa zimetoka kwa msemaji wake.

“Taarifa zote hizo siyo kweli na wala siyo rasmi kutoka ofisini kwa Mh Lowassa. Baada ya ziara ile, Mhe Lowassa alikutana na mwenyekiti wa chama chake, Mhe Freeman Mbowe na kumpa mrejesho wa yaliyojiri Ikulu.”

“Kumekuwa na taarifa nyingi kwenye mitandao zikiwemo kufunguliwa kwa akaunti mbalimbali feki , taarifa zote hizo zipuuzwe kwani zina lengo la kupotosha kwa malengo wanayoyajua wapotoshaji hao pamoja na mawakala wao,”

“Taarifa rasmi zitatolewa kwa njia rasmi na watu wenye mamlaka hiyo.poleni kwa usumbufu wote.”

Chanzo: Mwananchi
 
Back
Top Bottom