Absalom Kibanda aaga rasmi Tanzania Daima

Status
Not open for further replies.
Duh! Alikuwa Balile, akaja Peter Nyanje (yeye alienda the Citizen kama sikosei). Pia kuna Kulwa Karedia alienda Habari corporation. Sasa Kibanda. Yangu macho.

Namwaminia Ansbert Ngurumo.
 
Kuna vitu naanza kuamini Zitto alikuwa sahihi,pengine kuna baadhi ya vitu anaweza kuja kutupruvu rongi(But not all!)
 
Last edited by a moderator:
Kumbeeeeee

watu walishamshtukia kwa Makala zake bora akae pembeni ili aweze piga manati mahali anapopaona panaharibika kuliko kukaa ndani ya Jahazi asilolielewa
 
"If you cant beat them join them"
Hakika na kesi inayomkabili itafutwa RA AND ER at work.
 
Hawawezi mkuu labda iwe ni mkakati wa kambi yao.Pengine mkakati wa kumshughulikia Mbunge wa mtama na kiongozi ajaye wa upinzani (baada ya uchaguzi mkuu 2015)Sasa huko alikoenda kuna changamoto gani?

Mkuu Ben Saanane Kibanda si mara ya kwanza anakuwa Mwajiriwa wa Rostam Aziz. Miaka kadhaa kabla hajaja Tanzania Daima alikuwa akifanya kazi na gazeti la Mwananchi lililokuwa na umiliki mkubwa wa RA na bado alizingatia taaluma, weledi na maadili ya Uandishi wa habari hadi Free Media chini ya Freeman Mbowe ikampa kazi.

Amefanya kazi kubwa sana na Tanzania Daima hadi kulifikisha hapo lilipo. Kwangu mimi Tanzania Daima ni kati ya magazeti ambayo yanaongoza kwa habari zilizofanyiwa analysis nzuri na makala nzuri za kisiasa. Kibanda anastahili pongezi.Nadhani apewe muda huko aendako pengine anaweza kuwa chachu ya kuigeuza New Habari

Najiuliza Tanzania Daima litabaki na nani? Maana Ansbert Ngurumo ni kama namuona anapiga jaramba kuwania Ubunge pande za Muleba. Pengine Kubenea anakabidhiwa mikoba hiyo.Huwezi jua.
 
Uraisi huwa unatafutwa kwa mipango na fedha na baadae damu za watu, hii ni upanda wa 1 upande 2 mangula ameletwa rasim akate jina la mtu, kana kwamba wanaomtuma ni wasafi vile, nasikitika kusema kuna watanzania wachache sana wanaoweza kuheshimu taaluma zao
 
Jamii Forum ni kiboko sana.
Kuna wadau walisema wiki tatu zilizopita kuwa huyu Kibanda anakwenda kuajiriwa Habari Cooperation, hivyo zile makala zake za kumsifia Kinana na kuwaponda Chadema zilikuwa ni chokochoko za kuanzisha bifu na mwajiri wake(Mbowe) ili aondoke kwa visa, lakini watu walimwangilia tu na sasa kaamua kuvaa magamba wazi.
 
Aliyekuwa mhariri mtendaji wa gazeti la Tanzania Daima Absalom Kibanda, leo ameaga rasmi na kuachia nafasi yake mhariri mtendaji, kwa maelezo kuwa anaenda kujiunga na kampuni ya New Habari Corporation 2006, inayochapisha zaidi ya magazeti manne hapa nchini.

Akiongea na wafanyakazi wa gazeti la Tanzania Daima leo asubuhi, kibanda alisema sababu kubwa ya kuondoka hapo ni kwa ajili ya kutafuta changamoto mpya katika majukumu yake ya uandishi.

Amewataka waandishi wa gazeti wanaobakia waendelee kufanya kazi kwa bidii, kwa ajili ya kulikomboa taifa kwa kuuanika ukweli pasipo kuogopa,


Hapo kwenye red: Anakokwenda hato thubutu kuandika huo ukweli maana anaingia kwenye chungu cha mapapa wa ufisadi.
 
Si maslahi na wala si bifu na muajiri wake huu ni uamuzi wake, tukijifunza kuheshimu uamuzi wa wengine tutakuwa katika njia sahihi tuitakayo, hata kama hatukubaliani nao.halikuwa bifu na waajiri wake wa awali kama inavyavysemwa hapa, ule ulikuwa mtazamo wake katika kuonyesha kile anachoamini ni jukumu la wale watakaoona ukumbusho ule unawafaa watumie na wasioutaka waache
Mtu kuhama kampuni au muajiri sio ajabu. Tabu ni vile kulazimisha bifu na muajiri wako wa sasa ili upate sababu ya kuhama.

Kibanda pale ulichemsha kaka!!
 
Last edited by a moderator:
Hii habari ilikuwa inategemewa kwa sababu kuna post iliwelwa humu kuwa atahamia Habari corp. siku za karibuni. Sishangai kuhama kwake kwa sababu hata uandishi wake ulishaanza kubadilika ukilinganisha na alichokuwa akiandika hapo awali. Hata hivyo itakuwa vizuri kuangalia kuwa akiwa huko uandishi gani utakuwa unaelekea upande upi na ni jinsi gani atakavyoweza kuwaaminisha wasomi wa habari zake ukulinganisha na hali halisi na jinsi wananchi wanavyo ihisi na kuielewa hiyo kazi. Binafsi nasema, kazi kubwa anayo, namtakia kila la heri.
 
Anawasisitiza waandishi kuandika ukweli?? Mbona haiingii akilini, yaani yeye anakwenda kwenye magazeti yanayo ficha ukweli na uandika uongo,n huku akiwaambia wenzeka kuandika ukweli?

Hii nchi itachelewa sana kukombolewa ikiwa ukoombozi huo unategemea akili za akina Kibanda!
 
Anawasisitiza waandishi kuandika ukweli?? Mbona haiingii akilini, yaani yeye anakwenda kwenye magazeti yanayo ficha ukweli na uandika uongo,n huku akiwaambia wenzeka kuandika ukweli?

Hii nchi itachelewa sana kukombolewa ikiwa ukoombozi huo unategemea akili za akina Kibanda!

Mkuu Yericko,

huu ndiyo unafiki wa hawa watu.Lakini katika safari ya mabadiliko ni lazima tupate moyo hasa tunapoona kasi ya usaliti inaongezeka.Kama mimi kadiri ninaposalitiwa ndivyo kasi yangu na ari ya kupambana inapokua juu.Let us move on comrade!
 
Mkuu Yericko,

huu ndiyo unafiki wa hawa watu.Lakini katika safari ya mabadiliko ni lazima tupate moyo hasa tunapoona kasi ya usaliti inaongezeka.Kama mimi kadiri ninaposalitiwa ndivyo kasi yangu na ari ya kupambana inapokua juu.Let us move on comrade!

Hakika mkuu!
 
Plz Tanzania Daima, hebu muweke Said Kubenea hapo, ongeza na safu ya akina Ndimara Tegambwage! Na yule mzenji
 
Ngoja abadilishe mazingira,na hivi ana kesi mahakamani..katoa mzigo kichwani kaweka begani..
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom